Hotuba ya Rais Kikwete Sept 30, 2012

Ameelezea siasa za vyama vingi zisiwe ndiyo chachu kuvunja amani. Jee, hukubaliani na hilo?

Uvunjifu wa amani uliasisiwa na CCM kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995. Nakumbusha tu upinzani ulishinda majimbo yote Dar mwaka huo. Serkali ya chama tawala kupitia mamlaka ya kusimamia uchaguzi wakaamua uchaguzi urudiwe kwa sababu ya kutaka wapinzani wasusie uchaguzi utakaporudiwa. Wakafanikiwa kwa hilo, ila pia walifanikiwa kupanda mbegu ya kutoaminiana na kuasisi kauli zinazopalilia uvunjifu wa amani.

Nakubaliana na wengi huyu rais wa tume ya uchaguzi hakuwa tayari kuainisha mvunjifu wa amani ni nani kwa jina. HUO NI UDHAIFU
 
TUESDAY, OCTOBER 2, 2012

RAIS Jakaya Kikwete amezungumzia mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel 10, Daudi Mwangosi na kusisitiza umuhimu wa haki kutendeka katika suala hilo.


Akizungumza katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi uliopita, Rais Kikwete alisema mauaji hayo ni ya kusikitisha na kuongeza; "Jambo la msingi ninalotaka kusisitiza ni polisi na kutendewa haki. Asiwajibishwe asiye husika."


Mbali na kusisitiza umuhimu wa haki kutendeka katika mauaji hayo, aliliagiza Jeshi la Polisi, pale panapotokea malumbano kati yake na wafuasi wa kikundi cha kijamii au vyama vya siasa au wananchi, lazima wahakikishe hawatumii nguvu kupita kiasi.


"Polisi lazima wahakikishe kuwa hawatumii nguvu kupita kiasi. Wao wenyewe wanatambua vyema maana yake. Wanapofanya kinyume chake na ikathibitika hivyo nao pia huchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Haipendezi mbele ya macho na mioyo ya askari wetu lakini lisilobudi, hutendwa," alisema Rais Kikwete.


Hata hivyo, Rais Kikwete alifafanua kuwa moja ya mambo yanayozua migongano kati ya Polisi na baadhi ya viongozi na wafuasi wa baadhi ya asasi za kijamii na vyama vya siasa, ni mamlaka ya Polisi kutoa ushauri au hoja pingamizi kwa vikundi vya kijamii au vyama vya siasa kufanya maandamano au mikutano.


Alifafanua kuwa mamlaka hayo yametolewa kwa Polisi kwa nia njema ili kuhakikisha kuwa shughuli za kisiasa zinafanyika katika mazingira ya amani na utulivu bila migongano baina ya makundi au vyama wala bila kuathiri shughuli za jamii.


"Mamlaka waliyonayo polisi hapa nchini hata nchi nyingine duniani iko hivyo hivyo. Hata hayo mataifa maarufu kidemokrasia duniani hufanya hivyo hivyo. Hakuna anayefanya mkutano au maandamano bila ya ridhaa ya Polisi," alisema Rais Kikwete.


Katika mamlaka hayo, Rais Kikwete alisema Polisi huelekeza njia za kupita katika maandamano na kuzuia nyingine. Aidha, huelekeza wapi mikutano ifanyike na wapi isifanyike na kuongeza; "pale wahusika wanapokaidi makubaliano, hutokea athari na sote ni mashuhuda wa athari hizo kwa pande zote. Demokrasia bila ya utaratibu ni fujo."


Ili kuepuka fujo hizo, Rais Kikwete aliwataka wanasiasa kuendelea kutofautiana na kukosoana bila kutukanana wala kugombana. Wavumiliane kwa fofauti zao za itikadi na mitizamo ya kisiasa bila ya kuchochea chuki baina ya watu na watu au baina ya wafuasi wa vyama tofauti vya siasa au baina ya wananchi na Serikali, au vyombo vya Serikali.
 
Back
Top Bottom