Hapo kwenye wawekezaji wa ndani amepapasa papasa tu..
Halafu vitu vingine kama hivyo sijui huwa vinakuwa kama siri ya baadhi ya watu?
Maana hii kitu kwangu sounds "french"
It is not french at all. Nikupe mwanga kidogo.....leo hii vyama vya ushirika vya mikoa ya mtwara na lindi, kutokana na export guarantee scheme hiyo, vimeweza kununua korosho za wakulima kwa bei nzuri ambayo haijawahi kutokea in decades....kilo mwaka jana iliuzwa hadi sh 1700 kutoka shilingi 400 ya mwaka juzi. Na kubwa zaidi malipo kwa wakulima yalifanyika on time ( sio kama zamani walikuwa wanakopwa). Hayo ni matunda ya wazi ya schemes hizo....leo hii wakulima wa korosho wanaweza kupeleka watoto wao shule, wakakarabati nyumba zao, na kununua trekta kwasababu ya faida waliyopata. By the way kwa item hiyo tu watu zaidi ya laki mbili wanaolima korosho wamebenefit