Hotuba ya Rais Kikwete kuuaga mwaka 2011

Usiwe wa kupinga tu kila kitu cha JMK ukweli unabaki kuwa ukweli. Hakuna Rais yoyote aliyefanya mengi zaidi ya Kikwete kwa kipindi chake kifupi cha miaka 6. Mambo mengi sana (karibu yote ya muhimu) hata uwachanganye wote hawafikii aliyoyafanya Kikwete kwa muda mfupi. Lakini hamuyaoni mnabaki kulalama na mnacholalama hamkisemi. Wewe nitajie moja ambalo Kikwete hajafanya zaidi ya Rais yeyote aliyepita.

Sure ninakubaliana na wewe especially nikiangalia mfumuko wa bei, uwekezaji uchwara etc!
 
Mwanakijiji, hiyo hotuba ni utumbo mtupu,(excuse my language) sijui nani anamwandikia, ukitaka kuikosoa na hata kujibu hoja yake utagunduwa ni watu gani wanamzunguka huyu mkulu!

Kwanza unaweza kunisaidia alimanisha nini hapo chini? Ama kulikuwa hakuna njia nyingine ya kuelewesha?

Really? Yani kumbe chanzo cha umasikini wetu ni kutokuwepo na uwekezaji wa kutosha na wakati nchi ishanza kuacha mashimo na polutions huku madini yakiwa hayana manufaa kwa mwananchi, na imeshauzwa hadi mbuga za wanyama na maasai ndani? halafu eti anasema shamba halijalimwa?Gimme a break! Mbona tayari kuna wanaovuna? Ama misimu yetu imekaa tofauti na yao?lol

Nimechoka!

Tatizo la nchi yetu kutokujua mipaka ya siasa taaluma na upashanaji habari; mwandishi anaweza chukua kazi hizo zote na kumpa Rais kuisoma ili mradi tu in sound good into his ears bila kuangalia contradictions na professionalism; politics na communication yenyewe..So utaona huyo mwandishi alizingatia the way of communicating bila kuangalia hicho alicho communicate kinaji contradict kiasi gani..Mfano huwezi sema eti mtu anashamba la msitu anataka kulibadili eti alime anahitaji kulifyeka and so forth....Bila kuangalia what that means economically na how the concept communicated conradicts the principles or theories of development.....Kwanza huwezi kuwa na msitu wenye miti hiyo ukashindwa kununua nyezo za kufyekea ambazo bei yake ni ndogo kuliko thamani ya huo msitu kwa size yeyote ile; hapo mwandishi anachanganya mambo kwakua hajui mahindi; viazi; mchele na vingine ni bidhaa za kilimo kama ilivyo miti na katika hizo miti inathamani kubwa zaidi (cash) kuliko hizo alizo maanisha kuzitaka kuzilima in the place of hiyo miti.

Siyo hivyo tu thamani ya msitu siyo tu katika cash bali na ecosystem services hasa Rais akizingatiwa amesha ingiza miradi nchini kwake yenye hadhi ya kimataifa ambapo misitu inathamanishwa na watu kulipwa kwa uwepo wake tu ambapo value yake per hectar inaweza kuwa kubwa kuliko kulima mahindi maharage and so on. Hapo tayari wamemfanya Rais aonekane mjinga kwa werevu kwani ataonekana haelewi anachokifanya kwani siku nyingine atasiamama kwenye jukwaa akihimiza raia kutunza mazingira na huku alishawaonyesha ni jinsi gani kilimo cha mazao ya chakula kilivyo muhimu kuliko kilimo cha misitu.

So you can easly see kwanini watu wa mataifa wanavyoweza kutuona watanzania wote tukiwa hatuna akili kwani Rais ni symbo ya Taifa. Akikosea hilo kosa ni la kila mtanzania na siyo yeye kama JK. Inatupasa tuelewe sasa umuhimu wakutumia wataalaamu kuandika hotuba ya Rais na hao waandishi wakaweka tu luga iliyo nyooka bila kubadili maana ya kilichoandikwa na uzito wake. Na kama wataalamu wameandika hiyo hotuba inabidi Rais awawajibishe kwakumfanya aonekane kuwa mjinga kwakutozingatia taaluma zao. Hotuba ya Rais haisikilizwi na Raia tu bali na watu wa mataifa mengine na kama alivyo mzazi basi watoto (raia) tukishiriki kumvua nguo hadharani mzazi wetu basi ujue aibu hiyo si yakwake peke yake bali familia nzima. Majirani wakiona watoto wanajitahidi kumhifadhi mzazi wao ila yeye tu ndo anashindwa kujiheshimu basi watajua mwenye matatizo ni baba na siyo watoto kuliko ilivyo sasa ambapo utashangaa hao wanao itwa wataalamu watakuja public kutetea utumbo na badala ya kumfunika Rais wamwanika ni kwakiasi gani ana watu wasio na ufahamu na ndivyo tutakavyochukuliwa na mataifa ya nje kuwa watanzania ni wajinga kama alivyo sema Ehud Barak.

Kwakuzingatia hilo hotuba ya Rais inatakiwa kuandikwa na washauri wote wa Rais walio katika taaluma zote na kama ndiyo walioshiriki kuandika hii basi tuombe Mungu Tanzania inashida kubwa sana!
 
Wakuu mnasumbua sana vichwa vyenu lakini ukimsikia rais amnasema hajui kwa mimi kuna malimbikizo ya mishahara ndio ujumbe wa hotuba yake badala ya kutafuta sababu kabla ya kuhutubia.. Ukimsikia rais anasema walitakiwa watu wahame Jangwani kwa sababu alishatoa amri hiyo na hawakuhama hivyo yalowakuta ni Asiyesikia la Mkuu huvunja guu... Hapo inabidi wewe ujiulize vizuri nini wajibu wa rais!..

Yaani huyu anayemwandikia rais hizi hotuba afadhali mara kumi aandike Mwanakijiji au hata mimi Mkandara hapa nitajua namna wa kudanganya inapobidi lakini sii uzushi uloandikwa. Na kwa yeyote aloisoma hiyo hotuba na akakubaliana nayo 100 ana matatizo maana maneno haya ya kumwezesha mwananchi kayasema toka 2006 lakini tunayoyaona ni tofauti kabisa na kauli ile...

Kinachofanyika kwa mifano mingi wananchi wamefukuzw akatika maeneo ya wakawekwa wawekezaji wa nje toka Bulyanhulu hadi Loliondo na sisi kina Mkama tumepoteza urithi wa ardhi kubwa ya mababu na mababu Pasiansi Mwanza kwa ujenzi wa bwawa la majitaka just few meters kutoka ziwa victoria, sielewi anachoongea zaidi ya kufikiria hayo majitaka haya contaminate na drinking water ya ziwani..maana tumeshakubali kurudishwa nyuma.

With the growing number of unemployment, upungufu mkubwa wa uwekezaji toka ndani kwa fikra za kwamba wananchi wanaweza kuwa manamba au machinga kwa biashara za wageni sijui tunakwenda wapi...Tuombe Mungu salama tu.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Maskini Gordon Brown aliukosa uwaziri mkuu kwa kumwita mwanamama 'Bigot" au king'ang'anizi kwa lugha yetu adhama ya Kiswahili, Lakini hapa Rais wa nchi anasema "asiyesikia la Mkuu huvunjika guu" kwa wale ambao hawataweza kuhama mabondeni na bado yuko Magogoni anakula wali samaki.

Tatizo la watu wa mabondeni siyo viwanja pekee kama anavyofikiri, bali hata uwezo wa kujenga kwenye ughali wa vifaa vya ujenzi kama huu. Anawasaidiaje kupata vifaa kwa bei nafuu au kwa mkopo?
 
Acha uwezo wa hao jamaa wewe kama rais kweli unaishia kusema asiyesikia la mkuu huvunjika Guu?... Wananchi wako wamekufa badala ya kuonyesha uchungu mkubwa na kuuliza sababu gani wale watu hawakuhamishwa kama alivyoagiza? kutambua kwanza nani hasa ni victims hapa, leo unawatukana wao kwa matusi ya Umaskini wao wakiwa makaburini..Kusema kweli kama mimi ndiye ningekuwa JK, huyo aliyeandika hiyo hotuba ningemwita na kucharaza bakora kwanza kabla sijamweka Keko kwa wiki halafu unamfukuza na kazi..

Hotuba imejaa usanii wa ajabu ajabu kama vile anajibu tetesi za kimjini.. come on he could have done it better kama angeongea yeye mwenyewe kama rais na kuwapata wananchi matumaini na kicheko kidogo badala ya utumbo uloandikwa maana unamshusha zaidi JK na kuenyesha ujinga wake. hili ndilo liliuwa kusudio la mwandishi na sii salaam za mwaka mpya kwa wananchi..
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wakuu mnasumbua sana vichwa vyenu lakini ukimsikia rais amnasema hajui kwa mimi kuna malimbikizo ya mishahara ndio ujumbe wa hotuba yake badala ya kutafuta sababu kabla ya kuhutubia.. Ukimsikia rais anasema walitakiwa watu wahame Jangwani kwa sababu alishatoa amri hiyo na hawakuhama hivyo yalowakuta ni Asiyesikia la Mkuu huvunja guu... Hapo inabidi wewe ujiulize vizuri nini wajibu wa rais!..

Yaani huyu anayemwandikia rais hizi hotuba afadhali mara kumi aandike Mwanakijiji au hata mimi Mkandara hapa nitajua namna wa kudanganya inapobidi lakini sii uzushi uloandikwa. Na kwa yeyote aloisoma hiyo hotuba na akakubaliana nayo 100 ana matatizo maana maneno haya ya kumwezesha mwananchi kayasema toka 2006 lakini tunayoyaona ni tofauti kabisa na kauli ile...

Kinachofanyika kwa mifano mingi wananchi wamefukuzw akatika maeneo ya wakawekwa wawekezaji wa nje toka Bulyanhulu hadi Loliondo na sisi kina Mkama tumepoteza urithi wa ardhi kubwa ya mababu na mababu Pasiansi Mwanza kwa ujenzi wa bwawa la majitaka just few meters kutoka ziwa victoria, sielewi anachoongea zaidi ya kufikiria hayo majitaka haya contaminate na drinking water ya ziwani..maana tumeshakubali kurudishwa nyuma.

With the growing number of unemployment, upungufu mkubwa wa uwekezaji toka ndani kwa fikra za kwamba wananchi wanaweza kuwa manamba au machinga kwa biashara za wageni sijui tunakwenda wapi...Tuombe Mungu salama tu.

Hao hao ndiyo wanoandika policies documents zinazo pelekewa wabunge ambao wengi wao ni kupiga meza na kusema imepitaaaaaa! Mpinzani anayeshugulisha akili yake kidogo kwa kuangalia context anaambiwa anataka kuvuruga amani and there we go na amani (sijui tofauti yake na ujinga) yetu ambayo hata siku moja haijawahi kumpelekea mtu sahani ya chakula mezani na watoto wake; matokeo yake ni policies zetu kuwa kama nyimbo za bongo flavour na background zake za kisanii ambapo mwimbaji akitoka hapo anaenda kwake kukutana na reality huko Mbagala; Manzese; Magomeni Mburahai etc ambapo mlango wa chumba chake unaelekea kwenye bafu la jirani yake ( I dont be-little them; nawaheshimu sana na kuwathamini lakini ndo ukweli wenyewe) ...Sorry nimetumia luga mbaya kidogo ili kuwa provoke wasika waone jinsi wanvyoendelea kuiharibu nchi.
 
Salamu za mwaka mpya ambazo kwanza hazina hata mvuto wa kuitwa hivyo, maybe thats the biggest dissapointment to begin with!

Salamu za mwaka mpya zilitakiwa zijikite kwenye kuelezea ni kwa jinsi gani tutakabiliana na changamoto kwa namna ya tofauti ili kuepuka hayo ambayo ndo kwanza kayaorodhesha utadhani ni mafanikio ie mafuriko na milipuko ya mabomu.

Haina mantiki...
yaelekea mwezetu uliandika haya 01.01.2000 na kupost hapa hata bila ya kusoma hotuba ya mheshimiwa rais. prejudice per se.
 
Bado ningependa kujua imekuwaje tena kuwe na malimbikizo makubwa kiasi hiki. Mambo haya tulikwishaelewana kuhusu namna ya kuepuka malimbikizo. Kulikoni? Je lini tabia hii ya kulimbikiza madeni itakoma? Nataka majibu toka kwa wahusika.

Hivi kwa nini hakutafuta majibu kabla ya kuleta hotuba?? Ok, then next time atuletee hayo majibu kutoka kwa wahusika tuyasikie!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom