Ni kweli kwamba shida yetu ya umasikini ni wawekezaji?
Maana naona keshalipatia jibu tayari lile swali la kwanini sisi masikini lol
He is right, the only way kuondokana na umasikini ni through uwekezaji wa ndani na nje plus uwezeshaji....issues ambazo amezi address soon baada ya huo mfano ulio u quote.....
"Katika kuwahamasisha wawekezaji, tunatambua fika umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wananchi wa Tanzania. Wanahitaji upendeleo maalum na wanahitaji kuwezeshwa na tumekuwa tunafanya hivyo. Ndiyo maana kuna maeneo na shughuli zilizotengwa maalum kwa ajili ya wawekezaji wazawa pekee. Aidha, umewekwa ukomo wa kiwango cha chini cha mtaji ambacho wawekezaji wageni lazima wawe nacho ili watambuliwe kuwa wawekezaji. Tusipofanya hivyo uchumi utatawaliwa na wageni.
Lakini hatukuishia hapo tu, tumelitazama suala la uwezeshaji wa wazawa ili waweze nao kushiriki katika fursa zilizopo nchini mwao. Tumechukua hatua za makusudi kufufua Benki ya Rasilimali kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wawekezaji wazawa kwa shughuli za viwanda na biashara. Pia tunakamilisha mipango ya kuanzisha Benki ya Kilimo kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wakulima wazawa. Benki hizo mbili hazitatoa mikopo kwa wawekezaji wageni.