Hotuba ya rais jk kuhusu madaktari ni janga la kitaifa

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Kauli ya rais na amiri jeshi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya mgomo wa madaktari ni janga la kitaifa.Hatukutegemea kwa kiongozi mkuu kama huyu kufikia kutoa kauli kama hiyo na kuwalaghai Watanzania kuwa serikali imetekeleza makubalianao saba kati ya kumi na mbili ilihali hali ya hospitali zetu inatisha kutokana na kukosa vitendea kazi.

Udhaifu wa uongozi wake umezidi kujidhihirisha kwa kubali kupokea taarifa ambazo hajazifanyia uchunguzi,hali kama hii imepelekea madaktari mabingwa kuitisha mgomo kuwa support madaktari wenzao.Inatisha kuona rais ana kubali ushauri mbovu na kuacha kuwaita madaktari na kutafuta suluhu nao.

Madai mengine yamebambikwa tu,wakati hayakuwa madai yao.Imekuwa ni desturi kwa viongozi wetu kila mara kulipotosha taifa kwa taarifa ambazo hazina ukweli.Hali kama hiyo imepelekea waziri mkuu kusutwa mara kwa mara kwa kusema uongo bungeni unaoweza kuliangamiza taifa.

Suluhu hapa ni muafaka juu ya afya ya Watanzania,kauli ya kuwaambia kama hawaridhiki na mshahara waache kazi ni kauli mbaya sana kwa kiongozi wa nchi ambaye amechaguliwa na wananchi kwa maslahi ya wananchi.Tuna uhaba mkubwa madaktari nchini mwetu lakini hata hawa wazalendo wachache waliokubali kufanya kazi katika mazingira magumu nao tuna wapuuza,wapi tunaelekea!


Kauli ya rais JK ni kauli ya kibabe na vitisho kwa afya ya Watanzania,uko wapi usikivu wako,hatukukuchagua ili uwe sababu ya vifo vyetu.Boresha mazingira ya hospitali zetu uone kama kutakuwa na mgomo.Mbona una safiri kuliko rais yeyote duniani,hizo safari zako hazina gharama au kuwaongezea wabunge mishahara ni sawa ilihali wengi wao hawana zaidi ya kusinzia tu bungeni na sababisha kuuzwa kwa nchi hii na kukiukwa misingi ya haki za binadamu kwa kupitisha hoja dhaifu zisizo na tija kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu.

Tulianza kidharura awamu ya nne,tutamaliza kidharura.Hivi hii mipango zimamoto ya serikali itaishia wapi.Kwa kauli kama hii uliyoitoa si tu kuwa ina katisha tamaa bali ni kauli ya uchochezi na uvunjivu wa amani ya nchi.Wananchi nasi tunapima tuone kama tuigomee serikali iliyosababisha mgomo wa madaktari ili Watanzania tufe.Tutaingia barabarani kutumia haki yetu ya msingi kudai haki yetu ya kuishi


Serikali ni yetu sote,kutibiwa kwenu nje ya nchi isiwe sababu ya kutoboresha hali bora na mazingira salama ya hospitali zetu.Kura zetu mlizipenda,zitumieni kura zetu katika kuhakikisha ustawi na maendeleo yetu na taifa kwa ujumla bila kuwatoa kafara Watanzania wasio na hatia.
 
Back
Top Bottom