Hoteli za Double Tree na Slip Way, zawekewa alama ya "X"

Wakabomowe shoppers plaza na my fair plaza wabomoe na dar villa na nyumba zte zile ...eneo lile si mkondo wa maji kuelekea baharini

Ovaaaa
 
Kama issue ni kuchafua mazingira kwa maana ya kumwaga maji-taka baharini; hapo kiulihalisia hotel nyingi sana kando kando ya bahari ya Hindi zitavunjwa, hasa maeneo ya Jangwani Beach. Ni kweli DT walifungiwa na kisha kupewa karipio wakati wa JK na kama bado wameendelea kukiuka agizo la serikali hapo hakuna utetezi. Je hizi hotel zingine ambazo zinafanya mchezo huo na bado dola haijawafikia nao wakavunjiwe? Je hakuna njia mbadala ya kuzifanya zisimwage majitaka baharini?

Tuachane na hotels, nyumba za watu zilizojengwa wakati Wizara na Mipango miji hawakuwahi kutamka lolote unazisemeaje? Iweje leo serikali inataka kuzibomoa kwa sababu ati wamiliki hawakuwahi kupewa kibali cha kujenga? Na kibali cha kujenga unakipataje kwenye eneo ambalo halijapimwa? Na je unajua gharama za kupimiwa kiwanja? Na hapo bado hujaingizwa mjini na masurveyor wenye kila aina ya njaa na solution hewa! Bado kuna umuhimu wa Manispaa kuweka nakala ya ramani ya Mipango miji katika Ofisi za Serikali ya mtaa nchi nzima. Hii itatusaidia sana kupunguza kulaumiana na kuoneana. Nasema kuoneana nikiwa na maana kwamba, endapo mimi mwananchi kwa maksudi najenga eneo hatarishi, na huku mchoro uliopo S/mtaa unanitaka nisifanye hivyo basi kimsingi naionea serikali kwa ukaidi. Vivyo hivyo serikali nayo ikiendelea kubomoa majengo ya watu katika maeneo ambayo sio hatarishi, na wala hakuna jitihada zozote zilizofanywa kuwataka watu wasijenge, then serikali itakuwa inawaonea watu wake.

Sisi kama taifa, tuna haja ya kupunguza kutafuta solution nyepesi kwenye mambo mazito. Hizi bomoa bomoa zina domino effect ya kutosha, hasa katika maisha yetu ya kibongo.Personally, nitaelewa pale tu serikali itakapobomoa makazi ambayo yako katika maeneo hatarishi (and mark my word - mahekalu yaliyopo kwenye mkondo wa maji karibu na TMJ kuelekea baharini hayataguswa, ila sisi wananchi tusiokuwa na nguvu ndio tutaendelea kuathirika na zoezi hili), na wamiliki walishapewa onyo/taarifa lakini bado wakakaidi au wakapeleka shauri mahakamani. Nazidi kusisitiza kwamba ubomoaji wa makazi ya watu waliojenga pasipo permits or title deed uamuzi utumie busara zaidi.
 
Lini inabomolewa? Nataka kushuhudia sheria inavyosimamiwa.

Wakimaliza hapo waende mwembechai, kituo cha mafuta kimejengwa eneo la shule. Waende Tabata Muslim, kituo cha mafuta kimejengwa katika kiwanja cha soko la umma.

Wenzangu tajeni maeneo ya wazi tuyarudishe na siyo kupiga kelele kutetea uvunjifu wa sheria.

Kwa wenzetu wa mabondeni mimi nakawia kidogo kusema.
 
Hivi hawa viongozi wanafikiri Dar ndiyo Tanzania pekee??? Mbina matamko hayo na hizo X Sijazisikia mikoa kama Arusha ambayo sasa hakuna kiwanja cha wazi hata kimoja, watu wamejenga kwenye vyanzo vya maji, mitoni, nk. Lakini kila siku Dar tu!! Mnakera hili zoezi litapendeza likiwa la kitaifa na siyo Dar peke yake.
Subiri wakimaliza dar watapiga hodi na Arusha, ila msilie kwamba ccm inawabomolea kwa sababu hamkuwapa kura.
 
What is this? A language similar to English or what....! Ni heri kuandika Kiswahili utaeleweka, sasa hiki sijui ndio kitu gani!!!
matokeo ya shule za kujifundisha wanafunzi kwa wanafunzi! anasema should thinks twices dah hadi huruma.
 
Inasikitisha kama viongozi wetu wataona ni busara kubomoa hotel kama double tree na majengo mengine makubwa. Wakati huu ambao kila mtu ana pambana na umaskini wengine wana ukumbatia. Serikali ilikuwa wapi hadi investment kubwa kama double tree ikajengwa?

Mkuu tulikuwa hatuna serikali kwa miaka kumi iliyopita.
Imerudi, inafanya usafi halafu ianze kazi.
 
zivunjwe tu ati kama masikini waonekane wachafua jiji wenye pesa waitwa wawekezaji hapana bomoeni tu!
 
NEMC wanatakiwa kuliangalia upya suala la ujenzi wa hotels ufukweni. Hotel nyingi zipo zero distance toka baharini. Km ni kutunza eneo oevu la bahari bas wamefeli coz nilishawahi kufanya kaz kwenye hotel fulani ipo oysterbay mbele ya ufukwe wa coco beach; kilichokuwa kinafanyika usiku ni hatari coz uchafu mwingi ulikuwa unamwagwa baharin!
 
Heshima ya nchi yetu inazidi kuimarika sasa sheria kuheshimiwa bila ubaguzi safi sana.
 
What is this? A language similar to English or what....! Ni heri kuandika Kiswahili utaeleweka, sasa hiki sijui ndio kitu gani!!!
tihi....ukiona hivyo ujue mwenzio hajui kama hajui kwa hiyo ukishamaliza kushangaa umsaidie kunyoosha.
 
Back
Top Bottom