L'AMOUR
Senior Member
- Mar 8, 2011
- 110
- 24
Naomba watahalamu wa sheria mnijuze,hivi kwenye tuhuma za murder mtu kumtetea kuwa ana miaka 17 na sio 18 inamsaidia kweli?umri wa mtu kuwajibika kisheria kwa kosa la jinai ni miaka mingapi?je mtu wa miaka 17 anaweza kusemwa kuwa hakujua aanallofanaya wakati wa kutenda kosa?mbona sheria inaruhusu mtoto wa miaka 16 kuolewa?Je mtu mwenye miaka 17 anapelekwa mahakama ya watoto?
Mtoto kama ikijulikana kuwa alikuwa anajua alichokuwa anakifanya wakati wa tukio sheria inamhukumu kama kawaida. Hapa napata wasiwasi kuwa mtoto Lulu kumbe alikuwa gereza la wakubwa kinyume cha sheria itabidi haraka sana aende kukaa gereza la watoto wenzake. Lakini ni kwa vipi pia mtoto aliiingia mikataba mbalimbali ya kibiashara wakati umri haumruhusu? Nadhani ni wakati muafaka kwa wafanyabiashara kudai mamilioni yao kwa kudanganywa na mtoto huyu kwani mikataba yao ni batili abi initio wajameni. Kweli hapa kuna mambo mengi yanaweza kuibuka upyaaaa kisheria na kimahakama kwa ajiri ya usanii wa LULU