Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Huduma The Best Kwa Cheapest Price! .

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,634
Wanabodi,
Declaration of Iterest.
Mimi ni mhanga wa ajali mbaya ya pikipiki na kutibiwa Muhimbili, ila nilitibiwa private na kuhudumiwa kama mfalme hivyo ushuhuda wangu huu uko based kwenye Private na sio Public.

Jee wajua kuwa huduma zinazotolewa na hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni huduma the best zenye gharama ndogo kuliko hospitali nyingine zozote? .

Uthibitisho kuhusu gharama za Muhimbili kuwa ni the best na cheapest, umetolewa leo na Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bw. Aminiel Algaisha kufuatia hoja zilizoibuliwa humu Jf katika bandiko hili la Mkuu The Boss likihoji
https://www.jamiiforums.com/threads/yanayotokea-muhimbili-ni-kweli.
Humu ndani tuna waandishi wa habari na watu wengine wafanyakazi wa Muhimbili ninaomba watueleze kama niliyosikia huko ni kweli.

Kuna taarifa huko Muhimbili sasa huduma zote ni za kulipia na gharama ni juu kupita hospitali za binafsi.

Mfano huduma ya wamama wajawazito ambayo ilikuwa bure kabisa sasa naambiwa lazima walipe laki tatu na ishirini..320,000/- na vipimo kama CT scan ni kulipa kuanzia laki sita.

Kuna vipimo ambavyo hospitali binafsi wana charge elfu 40 Muhimbili unalipa laki nne 400,000/ na kwamba mgonjwa akilazwa tu siku moja lazima alipe
na chakula ni kununua.

Nimejiuliza hizi taarifa ni za kweli au uzushi?

Kuna watu ambao mmekwenda Muhimbili hivi karibuni mtusaidie?

Pascal Mayalla Manyerere Jackton
Salary Slip

==================
Maoni ya wadau wengine
Mkuu The Boss, japo hili sijalifuatilia ila nilisikia wamebinafsisha huduma zote kwa wale wanaokwenda Muhimbili by choice ambao sio referral. Wanautumia mtindo wa CCBRT wenye pesa walipe, na wasio na pesa wataendelea kuhudumiwa bure na kwa kuchangia. Kuna wagonjwa kibao wa rufaa za mikoani au accident victims wanaotibiwa bure 100%. Wagonjwa wenye ndugu waletewe chakula wenye, pesa walipe chakula, dawa na matibabu, wasio na pesa, wasio na ndugu kila kitu ni bure.

Kitu ambacho sijajua ni kriteria tuu. Mimi nilipopata ajali ya piki piki nililazwa Moi Private by choice unalipia kuanzia room, chakula, service charges ya services zote, consultations, madawa, vifaa tiba, na kila kitu, tena wakati huo CT Scan name MRI zilikuwa mbovu hivyo unalipa 1.M Regency, ambulance 100,000 per trip, and that was 8 years ago name kulipia ilikuwa ni by choice sasa ambapo ni lazima sijui hali itakuwaje.

Paskali.
Bandiko hili lilimuibua Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bw.Aminiel Algaesha

Kitendo cha mwana Jf The Boss kuibua hoja yenye concerns kwa jamii, ni cha kupongezwa ila pía Kitendo cha Afisa Uhusiano wa Muhimbili kujibu ni cha kuungwa mkono na kupongezwa kwa sababu uongo ukisemwa na kuachwa bila kukanushwa kunapelekea watu kuuamini huo uongo, hivyo PRO wa Muhimbili amefanya vyema kujibu, ila asiishie kujibu tuu bali sasa ajiunge JF ili kukitokea uongo mwingine wowote, unajibiwa pale pale ila pia kwa vile JF inawanachama wengi, then sio vibaya Muhimbili ikiitumia JF katika uelimishaji masuala mbalimbali ambayo ni muhimu kwa umma.

Hizo ndio gharama za kutibiwa Muhimbili. Kama kuna yeyote aliyetibiwa hospitali nyingine yoyote yenye madaktari wa ubingwa kama wa Muhimbili na zenye vifaa kama vya Muhimbili, ajitokeze.

Ila pia kama kuna mtu alilipishwa viwango zaidi ya hivi vilivyoonyeshwa hapa na kupewa risiti, pia ajitokeze, ila kama umelipishwa zaidi na hukujali kuhusu risiti, naomba nikupe pole yako kwa sababu wale watumishi wa Muhimbili, nao pia ni binaadamu na sii malaika.

Nilipotibiwa Moi, Muhimbili miaka 8 iliyopita CT scan na MRI zilikuwa mbovu hivyo ikabidi nipelekwe Regency kwa vipimo hivyo, kila kimoja ni 500,000. Lakini leo MRI Muhimbili ni 210,000, CT Scan 150,000, Ultra Sound 25,000, X Ray 18,000, zunguka ukikuta popote huduma hizo ni nafuu kuliko Muhimbili, tujulishe tukimbilie hapo.

Baada ya Muhimbili nilikwenda Apollo India, nikilinganisha vifaa vya kule Apollo na vile vya Moi, kiukweli Moi wanavifaa bora kuliko Apollo. Kipimo cha pressure Moi ni cha umeme, Apollo nI kile cha kubonyeza. Vitanda Moi ni vya umeme, Apollo ni vile vya kunyonga, etc hivyo kiukweli tuna kila kitu ila basi tuu.

Tofauti pekee kati ya Muhimbili na Apollo ni customer care services, kule unahudumiwa kwa kunyenyekewa kama mfalme, jinsi manesi wanavyokuchangamkia na kukusmile, mgonjwa unajisikia nafuu na baadhi ya mgonjwa madogo madogo yanajiponea yenyewe.

Wenzetu kule wanafanya biashara ya tiba, huku tunatoa tuu huduma za tiba.

Hivyo hatua za Hospitali za umma kutoza gharama za kuchangia matibabu zina lengo jema la kuiwezesha Muhimbili kuboresha huduma zake. Yule nesi kule India anayekusmilea hadi kuchanganyikiwa, anakuwa alipata mlo asubuhi, anakula vizuri, anaishi mahali pazuri, ana usafiri wa uhakika na analipwa vizuri, kwa nini wasi smile hadi jino la mwisho?, vivyo hivyo huko kuchangia gharama kutawafanya wahudumu wa Muhimbili kusmile.

Kwa wenye uwezo tuchangie, penda chako, jenga chako.
Muhimbili ni yetu, tuipende, tuichagie kuiwezesha, tuijenge, tuitumie, itutumikie.

Paskali
 
Attachments

  • GHARAMA HALISI ZA VIPIMO MNH .pdf
    187.4 KB · Views: 128
"....Tofauti pekee kati ya Muhimbili na Apollo ni customer care services, kule unahudumiwa kwa kunyenyekewa kama mfalme, jinsi manesi wanavyokuchangamkia na kukusmile, mgonjwa unajisikia nafuu na baadhi ya mgonjwa madogo madogo yanajiponea yenyewe...." Hili nilijionea katika hospital moja ya Apollo iliokuwepo New Delhi.
 
muhimbili hii au nyengine.. mi nililipia hiyo private kwa matibabu ya kinywa na meno mbona nilijuta na kuapa sitorudi tena
 
Hii ndio serikali tuliyokuwa tunaitaka, ukiita inaitika bila kujali imeitwa Na nani.

Nimpongeze The Boss kwa kuibua mjadala, pia pongezi zaidi ziende Mhimbili kwa Ofisa uhusiano kwa kulichukulia kwa uzito swala hili.!
 
Nyumbu kwenye operation ya kwanza ya kata funua yamefeli.. Sasa tafuteni uongo mwingine
 
Wanabodi,
Declaration of Iterest.
Mimi ni mhanga wa ajali mbaya ya pikipiki na kutibiwa Muhimbili, ila nilitibiwa private na kuhudumiwa kama mfalme hivyo ushuhuda wangu huu uko based kwenye Private na sio Public.

Jee wajua kuwa huduma zinazotolewa na hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni huduma the best zenye gharama ndogo kuliko hospitali nyingine zozote? .

Uthibitisho kuhusu gharama za Muhimbili kuwa ni the best na cheapest, umetolewa leo na Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bw. Aminiel Algaisha kufuatia hoja zilizoibuliwa humu Jf katika bandiko hili la Mkuu The Boss likihoji
https://www.jamiiforums.com/threads/yanayotokea-muhimbili-ni-kweli.

Bandiko hili lilimuibua Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bw.Aminiel Algaesha

Kitendo cha mwana Jf The Boss kuibua hoja yenye concerns kwa jamii, ni cha kupongezwa ila pía Kitendo cha Afisa Uhusiano wa Muhimbili kujibu ni cha kuungwa mkono na kupongezwa kwa sababu uongo ukisemwa na kuachwa bila kukanushwa kunapelekea watu kuuamini huo uongo, hivyo PRO wa Muhimbili amefanya vyema kujibu, ila asiishie kujibu tuu bali sasa ajiunge JF ili kukitokea uongo mwingine wowote, unajibiwa pale pale ila pia kwa vile JF inawanachama wengi, then sio vibaya Muhimbili ikiitumia JF katika uelimishaji masuala mbalimbali ambayo ni muhimu kwa umma.

Hizo ndio gharama za kutibiwa Muhimbili. Kama kuna yeyote aliyetibiwa hospitali nyingine yoyote yenye madaktari wa ubingwa kama wa Muhimbili na zenye vifaa kama vya Muhimbili, ajitokeze.

Ila pia kama kuna mtu alilipishwa viwango zaidi ya hivi vilivyoonyeshwa hapa na kupewa risiti, pia ajitokeze, ila kama umelipishwa zaidi na hukujali kuhusu risiti, naomba nikupe pole yako kwa sababu wale watumishi wa Muhimbili, nao pia ni binaadamu na sii malaika.

Nilipotibiwa Moi, Muhimbili miaka 8 iliyopita CT scan na MRI zilikuwa mbovu hivyo ikabidi nipelekwe Regency kwa vipimo hivyo, kila kimoja ni 500,000. Lakini leo MRI Muhimbili ni 210,000, CT Scan 150,000, Ultra Sound 25,000, X Ray 18,000, zunguka ukikuta popote huduma hizo ni nafuu kuliko Muhimbili, tujulishe tukimbilie hapo.

Baada ya Muhimbili nilikwenda Apollo India, nikilinganisha vifaa vya kule Apollo na vile vya Moi, kiukweli Moi wanavifaa bora kuliko Apollo. Kipimo cha pressure Moi ni cha umeme, Apollo nI kile cha kubonyeza. Vitanda Moi ni vya umeme, Apollo ni vile vya kunyonga, etc hivyo kiukweli tuna kila kitu ila basi tuu.

Tofauti pekee kati ya Muhimbili na Apollo ni customer care services, kule unahudumiwa kwa kunyenyekewa kama mfalme, jinsi manesi wanavyokuchangamkia na kukusmile, mgonjwa unajisikia nafuu na baadhi ya mgonjwa madogo madogo yanajiponea yenyewe.

Wenzetu kule wanafanya biashara ya tiba, huku tunatoa tuu huduma za tiba.

Hivyo hatua za Hospitali za umma kutoza gharama za kuchangia matibabu zina lengo jema la kuiwezesha Muhimbili kuboresha huduma zake. Yule nesi kule India anayekusmilea hadi kuchanganyikiwa, anakuwa alipata mlo asubuhi, anakula vizuri, anaishi mahali pazuri, ana usafiri wa uhakika na analipwa vizuri, kwa nini wasi smile hadi jino la mwisho?, vivyo hivyo huko kuchangia gharama kutawafanya wahudumu wa Muhimbili kusmile.

Kwa wenye uwezo tuchangie, penda chako, jenga chako.
Muhimbili ni yetu, tuipende, tuichagie kuiwezesha, tuijenge, tuitumie, itutumikie.

Paskali
Again i salute you sir your comparative analysis.
 
First track Muhimbili they are the best, huduma, kauli, kujali, upendo etc
 
Mkuu Pascal Mayalla nashukuru kwa kulifuatilia na kutuletea majibu
ingawaje bado naona huko Muhimbili kuna kitu hakiko sawa
inawezekana mfumo wa tarifa haupo sawa
sababu wananchi wanazungumza tofauti na taarifa rasmi
 
Ndio maana nimesema kwanza wahusika wote pía ni binadamu, lakini pili ambalo ni kubwa zaidi, namna ya kumthibitisha mtu kuwa hana uwezo kabisa hadi kustahili kutibiwa bure ni issue, nahisi kuna baadhi by the time uthibitisho unapatikana, mwili mgonjwa unakuwa umeishapelekwa kwenye kile kijichumba.

Paskali
 
Baada ya Muhimbili nilikwenda Apollo India, nikilinganisha vifaa vya kule Apollo na vile vya Moi, kiukweli Moi wanavifaa bora kuliko Apollo. Kipimo cha pressure Moi ni cha umeme, Apollo nI kile cha kubonyeza. Vitanda Moi ni vya umeme, Apollo ni vile vya kunyonga, etc hivyo kiukweli tuna kila kitu ila basi tuu.

Asante sana bwana Mayalla, ninataka kukufahamisha tu kuwa hivi vipimo vya pressure wamegundua kuwa back to basis ni bora zaidi, vile vipimo vya kubonyeza na kupump kwa mkono viko more accurate than electronic ones. Ni kweli Muhimbili wanajitahidi sana ingawa kwenye customer service kidogo bado, lakini wakipata mwongozo watafanikiwa katika hilo.
 
Back
Top Bottom