Hospitali ya Taifa Muhimbili hushikilia maiti hadi deni lote lilipwe. Maiti zitokazo ICU deni hufikia hata zaidi ya 5mil

Ukizaliwa nchi hii lazima ujutie, ninaamini ajali zitokeazo na mauti yanayotokea hapo Muhimbili ni meng ya kutengeneza kwa ajili ya miradi ya watu. Hizi habari waandishi wanashindwa kuweka wazi uozo kama huu. Hapo Muhimbili kwa mradi kama huo wa maiti kutolewa mpaka mil5 kifo utakikwepa vipi? Ni lazima ufe au uuliwe.
 
Ukizaliwa nchi hii lazima ujutie, ninaamini ajali zitokeazo na mauti yanayotokea hapo Muhimbili ni meng ya kutengeneza kwa ajili ya miradi ya watu.

Hizi habari waandishi wanashindwa kuweka wazi uozo kama huu. Hapo Muhimbili kwa mradi kama huo wa maiti kutolewa mpaka mil5 kifo utakikwepa vipi? Ni lazima ufe au uuliwe.
 
Pole na msiba!
Hoja yako ni nini haswa?
Je ni kukosekana kwa dawa ICU muhimbili?
Je gharama za ICU muhimbili ni kubwa?
Je familia ndio haina uwezo wakulipa?
Je huna imani na madaktari/wauguzi wanaohudumia ICU muhimbili?
Je unaomba msaada wa kifedha kwa jamii inayokuzunguka?

Ukiainisha hoja yako kwa uwazi ni rahisi kutatuliwa bila kuathiri majina au utendaji kazi wa watu wengine
Mkuu asante sana kwa maswali ya msingi....mtoa hoja yupo disorganised. Hii ni tabia mbaya sana..akijibu haya naamini atapata majibu muafaka...
 
Kwa nini unapendekeza hospitali za serikali peke yake ndio zitoe misamah
Serikali ina mbinu nyingi za kukusanya Pesa! Nchi ina rasilimali nyingi sana ambzo zinawezaa fidia hilo gap na chenji inabaki ya kutosha!
Wizara ya maliasili pekee ikisimamiwa vizuri inaweza endesha nusu ya bajeti ya serikali ya Tanzania, hapo bado madini mafuta na kilimo n.k
 
Badala ya kutafuta mandege kwanza angerudisha UTU na UWAJIBIKAJI. Vyenginevo vilio vya Watz haviwezi kumalizika hata uwaletee maendeleo unayoyaona kwa wenzetu

Nchi ilipofikia Rais asiwe anahubiri uzalendo wa ndege,madaraja,na barabara eti vitu ivo ndio vinamuumiza zaidi.
 
Mi nadhani si vema wala si utu kwa hilo kuendelea kufanyika.

kwa kuwa ni Pesa zetu walipa kodi ikitokea MTU kafariki deni lilipwe na kodi zetu wafiwa wasamehewe.
 
Ukisha ziita za Serikali inamaana wanaanchi wanazichangia kwa kodi zao ndio maana zipo hapo, hivyo basi mwananchi ana haki ya kutoa maoni yake au dukuduku lake kuhusiana na huduma husika, tofauti na za watu binafsi au Taasisi ambazo sio za serikali.
Kodi yako kwa mwaka ni shilingi ngapi?
Igawanye kwenye elimu,afya,barabara n.k halafu uniambie kama inatosha au la
 
Back
Top Bottom