Hongereni sana watani kwa kuvunja mwiko wa miaka 25

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Hongereni sana watani kwa kuvunja mwiko wa miaka 25 na kutinga makundi ya Klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998. Ni jambo kubwa sana kwa wana Uto wote. Mnastahili pongezi. Japo mmeingia kwa kuwatoa wakimbizi lakini si mbaya.

Sisi tumezoea kuingia makundi kwa miaka mingi. Ni vitu vya kawaida kwetu. Lakini kwenu huu ni muujiza. Kidogo mlikua mnaliwezea lile kombe la "Loser" lakini huku kwenye klabu bingwa mlikuwa mnatepeta mapema sana. Mmekua "sokomoko" kwa miaka 25. Hatimaye leo mmevunja mwiko. Japo sijui ni upi maana mnapenda kusema "mbele mwiko nyuma mwiko" lakini nachojua mwiko mmoja umevunjika leo baada ya miaka 25. Hongereni sana.

Mara ya mwisho kufika makundi klabu bingwa ni 1998 wakati Mayele akiwa na miaka minne, Feitoto alikua mimba, na Whozu alikuwa na mwaka mmoja lakini leo anaitwa Chibaba . Makundi pekee mliyokua mnaingia mara kwa mara ni ya Whatsapp. Kwahiyo hongereni sana kwa kuvunja mwiko.

Ilikua inatia simanzi sana wakati Simba tukienda group stage, nyie mnarudi kuosha vyombo na Njombe Mji au Itilima FC. Lakini mwaka huu ni furaha kwamba kaka zenu tumepata watu wa kutusindikiza kwenye makundi ya klabu bingwa. Raha mliyoipata leo, sisi tumeipata mfululizo kwa miaka mingi.

Sehemu kubwa ya mashabiki wa Uto, hasa wenye umri chini ya miaka 25 hawajawahi kuishuhudia klabu yao ikicheza makundi klabu bingwa. Na walikua na hatari ya kuzeeka bila kuiona timu yao ikitinga hatua ya makundi. Kwahiyo leo wana haki ya kufurahi, kujibaraguza na hata kuogea maji ya bahari kwa kutoa mkosi.

Mwisho niwashauri vijana mnaotaka kuoa changamkieni mabinti ambao ni mashabiki wa Uto. Kama ameweza kuivumilia timu yake kwa miaka 25, hashindwi kukuvumilia wewe na chumba chako kimoja kwa miaka mitano mpaka utakapojenga kwako. Kuanzia kesho kama unatafuta mke "piga sound" binti yeyote aliyevaa kitop cha kijani na shimizi ya njano. Mtanishukuru baadae
Credit: Malisa GJ FB
FB_IMG_1696137362193.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom