Hongereni kamati teule za bunge

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Watanzania – Hebu tuungane wote kuzipongeza kamati teule za bunge. Kila mmoja atakubaliana na mimi kuwa kweli wanatufanyia kazi nzuri ambazo sielewi bila hizi kamati tungekuwa wapi leo.

Hongereni kwa kazi nzuri

Nimefuatilia kamati teule mbili zilizowasilisha taarifa zake bungeni jana na leo (ya nishati na ile ya Sakata la Jairo). Nimemsikia Makamu wa kamati teule Martha Umbulla na– akitoa tu vijimambo walivyokutana navyo katika uchunguzi wa kamati teule wa kutisha mambo anasema gari linajazwa mafuta lita zaidi ya 200 kuzunguka Dodoma kwa siku. Wachangiaji wengine waliongea kwa uchungu kuhusu ufujaji wa ajabu uliojitokeza katika huu uchunguzi mdogo tena haukufanywa na wakaguzi waliobobea (CAG &Co)

Nafika mahali najiuliza hivi kweli nani katudanganya kuwa sisi Tanzania ni maskini?

Hivi Mh rais wetu anaweza kuyaeleza haya kwa wazee wa CCM wa Dar na akahalalisha tusivyo na pesa za madawati na dawa za hospitali?

Hivi kwa nini nchi wahisani wanafumbia macho haya na kuendelea kungangania kutusadia?

Wanaona wazi kuwa hatuna tatizo la pesa ila tunahitaji za kutanua?
Au nao wahisani wana agenda ya siri na Tanzania?

:director:
 
Tatizo la Watanzania kila kitu ni siasa .Jambo la ajira ya mtumishi lina sheria inayolilinda ,ndo maana kamati imeshindwa kutamka moja kwa moja kwamba hao watu wamefukuzwa kazi.Siyo kwamba Serikali haitaki kuchukua hatua ,inataka sana lakini kwa kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali hiyohiyo(angalia Mwongoziowa namna ya kumchukulia hatua mfanyakazi wa Serikali), ama sivyo itaingia nchi katika mgogoro na vyama vya Wafanyakazi.Kawia ufike.
 
Back
Top Bottom