Hongera Serikali kwa makato ya mishahara ya Waalimu

Kama ndo hivo na walaaaniwe wote mnaowakata masikini waalimu wa nchi hii!
Nyooooooooooopp
 
Huu ni upungufu wa akili kwa ye yote aliyependekeza wazo hili. Majukumu ya maendeleo ya nchi yanaihusu serikali iliyo madarakani na wananchi wote kwa pamoja. Vipi ujenzi wa maabara ubebeshwe walimu?? Nini kazi ya paye wanayokatwa walimu?? Au hii ni kodi mpya?? Mmezidi kuwaonea walimu. Hii ni too much.
 
Bandugu, mie binafsi kwenye mshahara wangu wa mwezi machi 10000+ haikuwepo, nikajiuliza hawa ni Cwt au ni watu gani?, hii ni halmashauri niliyohamia mwanzoni mwa February na kwa vyovyote vile mshahara wangu ulikuwa bado halmashauri niliyotoka, kama ni Cwt wamenifikia vipi?. ni shiida. Mbaya zaidi tuna chama ambacho kinaangalia maslahi yake zaidi matatizo ya wanachama wake kama hayo hayawahusu.
 
Mwigulu tangaza kusamehe motor vehicles license watu wamelaza leo miaka Kumi sasa wewe wambie yoyote mwenyewe kulaza motor vehicle alipe mwaka mmoja tu mingine samehe, utakusanya mabilioni mwigulu hii elfu Kumi ya wlimu una waonea, tu vyanzo vya hela mnavyo lakini mmkalia kuongeza kodi tu
 
Ni nchi gan unayozungumzia.?
Mbona hayo makato hayapo..? Au ni ya serikali ijayo.?
Ufafanuz pls
 
Nashangaa watu wengine anapondea ualim eti niwatu waliofel hizo ni fallacy kama we ulifaulu alaf unatoa argument za kijinga no research no right to speak msoropoke tu toa evidence kusuport argument yako
 
Habari wanajamii,

Nimefurahishwa sana na uamuzi wa serikali kuanzisha makato ya Tsh 10000 kwa kila mwezi kutoka kwenye mishahara ya Walimu kwa ajili ya ujenzi wa maabara mashuleni. Japokuwa binafsi bado nakiona kiwango hicho kuwa ni kidogo sana ukilinganisha na unyeti na mahitaji ya maabara ktk shule za sekondari nchini.

Ingekuwa vyema kama zoezi hili lingehusisha watumishi wote wa serikali na sekta binafsi.

Hapa namaanisha kuanzia rais wa nchi ambaye yeye angechangia asilimia 20 ya pato lake kwa mwezi huku mawaziri, wabunge ,makatibu wakuu,makamishina ,wakurugenzi,wakuu wa wilaya na mikoa wachangie asilimia 10 ya mishahara yao kwa mwezi.Maafisa wengine waandamizi wa serikali pamoja na madiwani wakatwe asilimia 5 ya pato lao.

Maafisa watendaji wa kata na vijiji pamoja na wananchi wa hali ya chini wachangie nguvu zao kwa kujitolea .Kutokana na mchakato huo makato ya mwaka mmoja yataweza kutosha kujenga maabara kwa shule zote nchini.Pia serikali ifikirie kujenga maabara kuanzia ngazi ya shule za awali ,msingi na sekondari haadir kidato cha sita.

Hapo tutaweza kuibua, kulea na kukuza vipaji katika tasnia ya Sayansi na Teknolojia .

Hebu tulitafakari hili...

Dah! Hii thread imeniuzunisha sana, kwa nini walimu??? Pili, hivi leo hii serikali ya ccm ikiamua kuceize account za Mh. CHENGE na fedha hizo kutumika ktk ujenzi wa maabara, tutajenga mahabara ngapi??? Hivi mwalimu wa primary ana nafasi yeyote ya kufanya ufisadi ktk shule anayofundisha...au labda aibe chaki...! Siungi mkono hoja, walimu Tanzania, we need to do something aisee!
 
Back
Top Bottom