Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 121,947
- 95,237
Utawala wa Kenya chini ya Rais William Ruto umepata pigo kubwa baada ya mahakama kuu nchini humo jana Ijumaa Juni 30 kutoa amri ya kusitisha utekelezaji wa sheria mpya ya Fedha ya mwaka 2023.
Katika maamuzi yao yaliyotolewa na Jaji Muguru Thande wa Kitengo cha Katiba na Haki za Binadamu Milimani,
Mahakama imemzuia Waziri wa Fedha Njuguna Ndung’u na Mwanasheria Mkuu Justin Muturi na Mamlaka ya Mapato Kenya KRA kutotoza, kuiimarisha au utekelezaji zaidi wa sheria hiyo anbayo ilitarajiwa kuanza rasmi Julai 1, 2023,
Ikisubiriwa usikilizaji wa kesi iliyowasilishwa na Seneta wa Busia, Okiya Omtatah.
Amri hizo zilitolewa baada ya Omtatah na wanaharakati wengine wanne kuwasilisha maombi ya uharaka wakiomba kusimamishwa kwa utekelezaji wa Sheria mpya ya Fedha 2023
Ambayo ilitiwa saini na Rais Ruto siku ya Jumatatu na kuelezea kuwa ilikuwa kinyume cha katiba.
Wakati wakiomba amri ya muda itolewe wanaharakati hao walimjulisha jaji kwamba sheria iliyopitishwa na utawala wa Kenya Kwanza inapelekea kuwalazimisha wakenya kulipa kodi bila ya mpangilio wala uhalali.
Walioshtaki wanadai kwamba kodi zilizowekwa katika Sheria ya Fedha 2023 ni batili na zinakiuka kipengele cha 23 cha katiba.
Hakika kama Tanzania tungekuwa na katiba iliyo na ubora angalau nusu ya wakenya tusingekuwa tunapitishiwa miswaada ya kutatanisha.