Hongera Regia, Mbunge kupitia viti maalum CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Karibu tena kuendeleza libeneke la malavidavi kwenye jukwaa la "Mahusiano na Mapendo". Lakini you'd better go undercover again with some stupid moniker like "gendersensitive", till the next elections in 2015!
 
all the best mjengoni

kwa vile umefika huko kwa nafasi za viti maalum za wanawake tunaomba uchukue msimamo unaonyesha kumthamini mwanamke, zaidi ya ule uliokuwa nao awali.
 
Hongera sana Mdogo wangu kwa kuteuliwa Mbunge wa viti maalumu kupitia chama chako CHADEMA. Mwenyezi Mungu akujalie kila jema.
 
Dada Regia, wakilisha kuingia kwako mjengoni iwe chachu ya maemdeleo ya chama chetu na taifa kwa ujumla. Mchango wako mjengoni usimame na kuishi milele hata pale utakapoamua kuachana na hiyo kazi.
kazi yako itufanye siku moja tufikirie kujenga mnara mkubwa wa kumbu kumbu kukuenzi katika moja ya majiji yetu hapa nchini. Natumaini pia utawakilisha vizuri mawazo na kiu ya Great Thinkers ambao wengi wetu tunahamu kuona taifa hili likipiga hatua kubwa katika kuunda sheria / sera zitakazofanya nchi zingine zizifuate na siyo taifa hili kufuata sera na sheria za nchi nyingine.
Hongera sana dada yetu, lakini nikukumbushe kutovaa mawani na kuacha kuchungulia jamvini mara ufikapo mjengoni. Daima mapambano yanaendelea huku nje ya mjengoni watu hatulali sababu ya huyu mdudu hatari, "UFISADI".
 
- Mheshmiwa Regia, heshima yako na ubarikiwe sana na Mungu wa Mbinguni. Kilombero ninaifahamu vizuri maana nimesoma hapo Kidatu Sugar Ins., Kilombero 1. Ni matumaini yangu kwamba utawasaidia sana wananchi wa jimbo hilo ili waweze kuona angalau mwanga wa maendeleo na utapigania vijana wa hapo jimboni kushiriki katika ajira ya kukata miwa ya kiwanda cha sukari hapo, badala ya kuendelea kutegemea watu kutoka nje ya jimbo, SALUTE!

- Ukikwama kimawazo popote katika njia za uwakilishi wa jimbo, tafadhali usisite kuja hapa Jamiiforums, kuchota mawazo.

Thanks na Ubarikiwe.


William.
 
Aisee huyu Dada mimi simfahamu lakini kwa jinsi mlivyompa hongera lazima atakuwa ni mtu wa kipekee sana yaani mpaka na mimi nimemwonea wivu. Lazima atakuwa na future nzuri huko aendako. Dada chukua hongera yangu WAKUMBUKE WADANGANYIKA WANAOIBIWA MALI ZA NCHI NA KURA. Ipo siku Mungu atauona udhalimu wao
 
Very many congratulations our dear Regia. You have shown the way and many more are coming. On the other side, I congratulate the CHADEMA leadership for being visionary enough to place the names of the courageous women who contested for parliamentary seats in constituents in the front line for nomination in case they fail to go through that way. I hope other women who failed to clinch the seats from voters are in the list as well.

Having said that, I recommend to the special seat ladies of CHADEMA to strategise their activities so that they earmark constituents to contest come the year 2015. There are names that came out in the list that was mentioned today which, in my opinion, should be given this chance for the last time. I don't need to mention the names but I personally feel that they have enjoyed that right long enough. I would be happy if, by 2015, we have new and vibrant young women from CHADEMA wing that are recruited into the parliamentary ranks for preparation of 2020 and 2025 elections.

Concise to the point, thanks Mween. Said it all.
Regia, Hongera kwenda Mjengoni. Ukifika huko watumie wazoefu wewe na wenzako wote kuendeleza kazi. Mtumieni Dr Slaa sana kwani upeo wake na umahiri wa kujenga na kutetea hoja ni sehemu ya njia iliyowafikisha huko.
Regia wewe ni Mpiganaji, bado tunaitaka Kilombero yetu hamisha mpambano kwa Pilato. Umetikisa Kilombero na Morogoro. Hukuhitaji kusubiri viti maalum uliingia msituni mwenyewe wakachakachua lakini riziki ni mdudu huja kwa kutambaa! tishi! mjengoni.
Regia na akina Myika, Kabwe, Owenya msisahau mlikotoka, mkawa busy na kuitupa JF, kumbukeni hapa ni kisimani.
JF member tunaanza ku recruit fo 2015 right now!

Natoa hoja, Regia apewe ''nishani'' ya JF itakayojulikana kama ''JF Dada wa Shoka''
 
Hongera dada yangu Regia,

Ile kazi nilyoibuku ya kukuendesha usisahau kunikabidhi.

Nina leseni class C tena Diplomatic.:smile-big::smile-big::smile-big::smile-big:
 
HONGERA.....!
wengi wakiingia mjengoni wanasahaulika......NOT SO TO YOU...wengi wakiingia mjengoni yale waliyoyasema wanayaacha...NOT SO TO YOU....! januari makamba amefafanua atafanikishaje maendeleo kwa kuwa mbunge.......NAPENDA HII STRATEGY...can you please nambie...utafanikishaje na kuchangia maendeleo maendeleo?....... kwa kuongea pekee au kwa kuchukua hatua thabiti na zinazoonekana kuleta maendeleo?
 
hongera dada ila ucheck health status yako kabala ya bunge na kisha ukajitunze sana hatupendi kukupoteza maana wakwaleee mh nawasilisha
 
hakuna kusubiri mwaka 2015, wezi wa kura ni vibaka ,dawa yao ni kwachoma kwa petroli kabla hawala krismasi, andaeni madumu ya petroli kabsaaa huko majimboni, choma wao wenyewe na nyumba zao,ila msichome familia zao. VIJANA AMKENI KUMEKUCHA
 
Hongera dada Regia................

USHAURI
1.Tumia muda mwingi kuisoma Katiba yetu.............na uielewe....kwani umekuwa dhaifu mno kwenye kuielewa katiba yetu
2.Soma sheria za Bunge na kanuni zake

All the best........

The Ogah

Ushauri huu ni kwa Wabunge wote "Especially Wapya"! Nimekuwa nikiwasikiliza wengi wakiongea "politics", but you wonder hata kama wanafahamu rangi ya "cover" la Katiba ya JMT!
 
Nilifuatilia tangu ukiongoza kwa kura 1212 na nilishangilia sana. Nilipigwa na butwaa niliposikia wamechakachua. Sipati maneno mazuri ya kukupongeza! NISEME TU HONGERA SANA. Nakuasa usiende bungeni kuwa kama wale viti maalum wa kupongeza tu, jifunze kujenga hoja na kuzisimamia. Kila nitakapokuwa na hoja ya kufaa nitakutumia kwenye email yako ya bunge maana kila mbunge hupewa email ya bunge. Usikose kutembelea JF - utapata mawazo mengi sana. Hongera tena- Hakika Mungu amekufuta machozi.
 
Huyu dada regia nilimuona katika kipindi cha mchakato majimboni kwa kweli dada anajitahidi hongera
 
Congrats12.jpg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom