Hongera JK kwa kututoa katika Umaskini duniani! ila bado ....

Mkuu bado unatumia makosa yaleyale ya kulinganisha yale ya mwaka 1980 kwa mtazamo wa leo wakati hujui thamani ya Tshs mwaka 1980. Labda niweke hilo pato (highlighted) na tulifanye kwa mwezi..Mwaka 1980 hakuna kiongozi wala mtu aliyekuwa akipata mshahara wa Tsh 3,088 hakuna labda rais na mawaziri sina hakika, ni nyingi sana.. lakini leo hizo 662,856 ni mshahara wa kati kabisa kwa wafanyakazi (graduates) na maisha bado yatawashinda. Kwa hiyo, mwananchi wa mwaka 1980 aliyepata mshahara wa Tsh 700 robo ya pato la Tsh3,088 aliweza kuendesha maisha yake hadi akajenga nyumba na kadhalika wakati leo hii tunashindwa kuendesha maisha hadi tupewe 662,856 bado huoni kwamba hali ya maisha ya leo hailingani na pato?..

Mkuu,

Na nyie mnatumia makosa yale yale ya kulinganisha cost of living ya mwaka 1980 na cost of living ya mwaka 2011. Gharama ya ujenzi nyumba miaka ya 1980 ilikuwa haizidi Tshs 100,000 kama sikosei au zaidi. Leo hii bila ya milioni 10 hujajenga nyumba hata ya mbavu mbili. Tunarudi pale pale mazingira tofauti. Ila labda nikuulize inflation nayo inawakilisha gharama halisi za maisha Tanzania? Inflation ni 14% mie nimenunua mkate jana sehemu nimekuta ni Shs 2800 mkate huo mwaka jana ulikuwa Shs 1000 an increase of almost 100% je kuna uwiano hapo? Utaona any economic metric inatumia benchmark fulani kuwakilisha taswira ya sehemu husika. There is no such a thing as an actual economic metric in economics. Zote zina assumption fulani ambazo they have certain weakness. However, GDP has remain a strong indicator of economic performance na ndio maana hadi kesho financial markets in US, UK, Hong Kong, Australia are using it an important indicator of country economic performance and country well being.

Tukirudi katika kumpongeza JK hebu tufanye comparison of Tanzania GDP per capital income against other nations in East Africa. In 1980 our GDP took us to the bottom of income table tukijulikana kama moja nchi maskini kabisa duniani behind the likes of Msumbiji. 2010 We are 50th poorest nation isn't that an achievement? We are just few yards behind Kenya je sio mafanikio? Wewe ukiwa wa mwisho darasani na ikatokea ukawa wa 20 darasani hutafurahi na kushukuru? Tulikuwa mkiani kiuchumi leo tuko nafasi ya 50 kwa umaskini na tunaelekea kupanda mnasema sawa sawa kweli watanzania hatuna shukrani? I beg to differ wakuu. This is a success.

in relatives to other nations tukicompare our income miaka 1980 tulikuwa nchi za mkiani kwa utajiri
 
Kamanda Mkandara,

Mkuu wangu GDP per capital metric has got its own weakness but it remain to be strong economic indicator for economic changes and performance. Kuna mchina mmoja alikuja na model moja complicated nadhani imetupiliwa mbali kwani GDP is robust since it also takes into account the utility of consumers. Huwezi kuwa unanunua mkate kama huupendi na hivyo unavyonunua mkate inamaana umeridhika nao.

Tukirejea katika hoja yako unarudi nilichokisema mkuu kuwa distribution of income but ni kikwazo nchini kwetu. Watu wachache ndio wanamiliki uchumi wa nchi yetu. Pia wazungu wanatuibia na kuchukua baadhi ya mapato yetu la msingi ni kuziba mianya hiyo. Nashukuru umelitolea mfano Barrick kama umenisoma nyuma Barrick imekuwa listed canada na london. Kwanini wasiishinikize Barrick walist kampuni yao DSE ya Tanzania? Wakilist serikali itaweza kuwakata kodi, mishahara ya wafanyakazi wao itakatwa kodi, na pia tutapata mrahaba wanaotudanganya nao wa asilimia 3.

Ni mipango tu mkuu. Hebu niambie sarakasi ya makampuni ya mahoteli makubwa kwani serikali yetu inashindwa nini kuwadhibiti? Kila siku wanabadilisha majina kuendelea kukwepa kodi. Serikali inashindwa kuzuia mianya hiyo. Watu wanapangisha watu nyumba hawalipi kodi serikalini je unalizungumzaje? Ni mipango tu mkuu but for this hata wewe you have to acknowledge him kuwa ni mafanikio yake.
Nashukuru sana wakati tukiendelea kumpongeza Kikwete umefika mahala nawe umekubali matumizi mabaya ya mahesabu kwa maendeleo yetu. Kusema kweli mimi ningependa sana hawa wachumi na mataifa makubwa wakubali kutuhusisha nasi ktk umilikaji wa mauzo yao, na wala sii soko la Barrick liwe DSE libaki huko huko Marekani na Canada lakini Tanzania kwa dhahabu yetu tuwe na share ndani ya investment ya Barrick huko sokoni, kwa sababu sisi ndio wenye mali.

Hivyo mataifa yote yenye dhahabu na Barrick ndio tuwe na share kubwa iwe asilimia 51 au 49 halafu zilizobakia ndio ziuzwe kwa wacheza kamari lakini sii kuunda shirika kama Barrick na matajiri wake ambao hawana Uraia ama uhamiaji nchini isipokuwa Ukoloni mamboleo kuja wekeza kwetu kama wageni lakini wewe ukienda kwao hawakuruhusu hata kufanya biashara ya genge la nyanya bila kuwa mhamiaji au raia. Na kinachouma zaidi hawatumii fedha yao wala mitambo yao isipokuwa wanakopesha fedha na ku sub contract kazi kwa mashirika yenye uwezo wa kuchimba na kadhalika wao matajiri wanakunywa juice kwa mrija wakipiga mahesabu tu ya faida.

Haki iko wapi halafu wanapouza wao mali zetu wakigawana wao equity wanatutangaza ktk magazeti jinsi uchumi wetu unavyokua kama mbiu ya kuwaambiana wao - Jamani eeeh Ulaji uko Tanzania, nenda kaweke laki kesho zitazaa millioni wakituacha sisi na makapi kama sii mapanki.
 
Ndio waanze naungana na wewe kwa hili ila vile vile tusiache kumpongeza every step of the way hata mtoto wako uliyemzaa akigeuka kitandani anapokuwa mchanga wa miezi nane -12 unampigia makofi, akianza kutembea unampigia makofi, akianza shule pia unamnunulia nguo mpya, akifaulu unamchukulia zawadi kumpa, hadi anakuwa raia mwema. Rome was not build in one day. This is success still tulikuwa the third or second poorest country in the world sasa tuko 50 kitu. Wakaze buti tutafika safari.

Wewe jidanganye utafika ccm waendelee kupokezana urais kwa kura za wizi na kujipendelea anachojua kinamfaa basi ila tz kuendelea ni ndoto za abunuasi
 
Nashukuru sana wakati tukiendelea kumpongeza Kikwete umefika mahala nawe umekubali matumizi mabaya ya mahesabu kwa maendeleo yetu. Kusema kweli mimi ningependa sana hawa wachumi na matifa makubwa wakubali wala sii soko la Barrick liwe DSE libaki huko huko Marekani na Canada lakini Tanzania kwa dhahabu yetu tuwe na share ndani ya investment hiyo kwa sababu sisi ndio wenye mali. Hivyo mataifa yote yenye dhababu na kuiunda Barrick ndio wapewe shares iwe asilimia 51 au 49 halafu zilizobakia ndio ziuzwe kwa wacheza kamari lakini sii kuunda shirika kama Barrick na matajiri wake ambao hawana Uraia ama uhamiaji nchini isipokuwa Ukoloni mamboleo kuja wekeza kwetu kama wageni lakini wewe ukienda kwao hawakuruhusu hata kufanya biashara ya genge la nyanya bila kuwa mhamiaji au raia... haki iko wapi halafu wanapouza wao mali zetu wakigawana wao equity wanatutangaza ktk magazeti jinsi uchumi wetu unavyokuwa kama mbiu ya kuwaambia wao jamani eeeh Ulaji uko Tanzania, nenda kaweke laki kesho zitazaa millioni wakituacha sisi na makapi kama sii mapanki.

Hilo mkuu halitatokea kwani ufahamu wawekezaji wakija Tanzania hawaji mikono mitupu wanakuja na $Billions of them kuja kuinvest nchini kwetu. Sasa unapotaka 50-50 gawio sijui inakuwaje labda iwe makubaliano kama walivyofanya wenzetu waarabu kuwa mnashare cost of exploration (ambazo mara nyingi ni sunk costs), cost of uchimbaji, usafishaji, ungarishaji na uuzaji. Kama vyote hivyo haushiriki itakuwa vp mshare 50-50 costs mkuu haingilii akilini hata wewe ukianzisha biashara ni ngumu sana kukubali 50-50 wakati kazi yote unaifanya wewe. Dawa ni kutumia sheria zilizopo kuwabana Barrick na wengineo nchini kuwawanasimamiwa nchini ili hata kama tunapata 3% mrahaba basi kodi za serikali zinasaidia pia kunyanyua pato la nchi otherwise mshare cost. Hakuna free lunch mkuu.
 
Data nzuri sana bwana kwenye vitabu ila reality hiko je?Nafananisha na mwanafunzi ambaye mitihani ya shule anafauru na kuongoza bt ya kitaifa like necta anapata zero hahah
 
Star tv juzi j2 nilikua naangalia kipindi fulani asubuhi ambapo mzee mmoja alielezea ukuaji wa rushwa nchini tangu jk aingie madarakani hadi leo
mwaka 2005 corruption parception index (CPI) wakati ndo anaingia madarakani ilikua ni 2.3 na sasa mwaka 2011 imefika 3.5 akasema sasa anasubiria ifike 4.0 tuanze kupigana kama somalia je kweli huyu mtu (JK) anahitaji kupongezwa?
 
GDP ya tz kwa asilimia karibia 40 inachangiwa na sekta ya madini na utalii ambazo hata JK mwenyewe analalamika hazimsaidii mtz wakawaida...sekta ya kilimo inayoajiri watu wengi inazidi kuporomoka...ajira nyingi tz ni wachuuzi..ngo..
 
Hoja yako ingekuwa na maana km data hizo hapo juu zingekuwa zimetolewa kwa Tshs ila zimetolewa kwa dola. Kwa hiyo si hoja tena. Na si kila kitu kupinga vitu vingine kubalini tu na kumbukeni hata New York haikujengwa kwa siku moja, well done JK

mrudi darasani uchambuzi huu wa kutazamia madaftari vyuoni
 
So unatuambia JK tusimpongeze katika hili? Nafikiri utakuwa mkosaji wa shukrani. Hebu chungulia tena hizo data kipindi cha mwinyi GDP per capital ilikuwa baina 400-600 (sehemu ambayo Zimbabwe, Congo wapo sasa hivi). Mkapa GDP per capital income ilikuwa baina ya (600-1000) which is commendable. JK from 2005-2011 ni baina ya (1000-1400 ) je haikutoshi kumpongeza kwani yuko sawa sawa na mkapa kwa ukuaji wa uchumi kwa kipindi cha miaka 4. Tuwe watu shukrani wakuu sio kubeza kila kitu kwangu mie haya ni mafanikio mwanauchumi yeyote ayasifu.
Yawezekana kimtazamo wa figures per capital income imekuwa sanatoka USD 800 20 years back to 1400 now. Sasa chukua changamoto hizi mbili ziweke kwenye takwimu zako kisha utoe hizi pongezi, moja what was the exchange rate of USD vs Tshs in 1980, and what is the current exchange rate? The purchasing power of Tshs in 1980 vs Purchasing power of Tshs in 2010. What was the inflation rate in 1980, what was in 2010? Yaani kula ya kila siku ya common mwananchi ilimgharimu kiasi gani 1980 na ilimgharimu kiasi gani 2010? Ukifanyia kazi takwimu hizo na ukapata positive answers bravo.
 
Sijasomea uchumi lakini nimesoma somo moja linaitwa development studies (DS) na hapa sijatoka kapa, nilichojifunza hapa kuna aina nyingi za development mfano economic development, social development, human development, culture development. Sasa huyu ndugu yangu kakurupuka na stastistics zake economic development na kuja kuzimwaga hapa akidhani wanaosoma wote hapa ni manunda kama yeye, anafikiri watu wanalalamikia hiyo economic development unayoleta hapa, zaidi hapa watu wanapigika na social development na human development yaani kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii. Mi si mtaalamu sana wa masula ya uchumi ila kwa wale wanaojua masuala ya uchumi wanaweza wakatusaidia kudadavulia huyu nunda mkulupukaji
 
Mkuu wangu, tunapozungumzia swala la GDP na makuzi ya uchumi sii swala la watu wachache kumiliki uchumi wa nchi yetu. Hapana! hii kitu nyingine kabisa.

Kuna tofauti kama mauzo yetu yanafanywa na mashirika ya watu binafsi wenye accounts zao nchini yaani kina Bakhresa. mauzo yao tunaweza kuyaweka ktk hesabu zetu lakini sii mauzo ya kina Barrick ambao pato zima la mauzo linakwenda Canada na kufanya mzunguko huko.

Nakuomba unielewe ktk hili, yaani ipo tofauti kubwa sana kama mzee wako ana duka na mnauza yake mkahesabu kama mauzo na pato la Familia, tofauti na Mhindi aliyepangisha ktk nyumba yenu na mkaanza kuhesabu mauzo yake kama ndio pato lenu kwa sababu tu anauzia nyumbani kwenu. GDP tunayoitumia sisi ni mauzo ya mhindi ambaye sisi hatuoni shilingi yake zaidi ya kodi ya nyumba.

Na unachozungumzia wewe ni mauzo ya duka la baba lakini baba hatugawii pato sawa lakini fedha zinaingia ktk account yake. Kimahesabu hata kama kazuia zote bado ni baba yetu hizo fedha zitatumika ndani ya familia hivyo ni zetu - hili halifanyiki ktk kuipima GDP yetu..

Na wanachokifanya Ulaya au Marekani, akija Mhindi kutaka kuuza duka kwanza anaozeshwa mke/mume ndani ya familia (uraia) halafu ndio unapewa kuuza duka hizo fedha zinakuwa za familia hata kama ni za mhindi lakini hazirudi India.
Mkuu, nakupongeza kwa kulichambua swala hili kwa lugha na mifano ya kawaida kiasi kwamba hata sisi tusio na elimu ya uchumi wa vitabuni tunaweza kuelewa nini kinatokea kwenye uchumi wetu ambao wasomi wetu wa uchumi wa vitabuni wanatulazimisha tumpongeze JK wao bila ufafanuzi wa kina. Tatizo la wasomi wetu wanaishia kukariri nadharia za uchumi bila kuhusisha na uhalisia wa uchumi wa nchi. Nawashauri wasomi wetu waachane na kukariri nadharia, wasome, watafakari na walinganishe na hali halisi ya uchumi wetu, vinginevyo elimu yao ya uchumi haina manufaa kwa watanzania wenzao. Inakuwa mtoto si liziki
 
Hilo mkuu halitatokea kwani ufahamu wawekezaji wakija Tanzania hawaji mikono mitupu wanakuja na $Billions of them kuja kuinvest nchini kwetu. Sasa unapotaka 50-50 gawio sijui inakuwaje labda iwe makubaliano kama walivyofanya wenzetu waarabu kuwa mnashare cost of exploration (ambazo mara nyingi ni sunk costs), cost of uchimbaji, usafishaji, ungarishaji na uuzaji. Kama vyote hivyo haushiriki itakuwa vp mshare 50-50 costs mkuu haingilii akilini hata wewe ukianzisha biashara ni ngumu sana kukubali 50-50 wakati kazi yote unaifanya wewe. Dawa ni kutumia sheria zilizopo kuwabana Barrick na wengineo nchini kuwawanasimamiwa nchini ili hata kama tunapata 3% mrahaba basi kodi za serikali zinasaidia pia kunyanyua pato la nchi otherwise mshare cost. Hakuna free lunch mkuu.
Najua sana kwamba haliwezekani lakini tuzungumzie ukweli na sii hisia. Ya kutowezekana ni wazungu wanataka sisi tufikirie hivyo lakini chenye thamani ni dhababu yetu sio fedha yao. dhahabu haiko kila nchi paper money ni udanganyifu mwingine tu.

Hawa wawekezaji wanapokuja nchini na Billioni ni mkopo wanaopewa kwa sababu sisi tumewahakikishia bank kuwepo kwa mali hiyo (exploration). Hivyo pasipo kuwepo dhahabu Tanzania hawa wawekezaji hawawezi kupata hayo mabillioni waliyoyapata tena basi dhamana yake inakuwa mali yetu kutokana na mkataba ambao wanahakikisha lazima mali yetu iwe dhamana na sii insurance company ama accounts zao isipokuwa mali yetu ktk mkataba.. Kwa hivyo sababu ya mkopo ni sisi na dhahabu yetu kwa nini tusiwe na ushirika na hiyo mali?

Mkuu wangu kama mimi leo naanzisha biashara kwa kumwaga hela za ukulima ktk shamba lako kwa nini nisikubali ubia ikiwa nategemea mazao yatakayotokana yatakuwa mara mbili ya uwekezaji wangu licha ya hivyo kazi zote za ukulima unazifanya wewe. Mbona wapo watu wengi tu wamewekeza nyumbani na kuwapa share washirika wao na biashara inakwenda.

Tazama nyumba za Kariakoo mbona watu wanajenga kwa share za asilimia 70 kwa 30 kati ya mwekezaji na mwenye nyumba (kiwanja) au zaidi mradi makubaliano, lakini huwezi kuta mtu anachukua nyumba nzima akaijenga hotel kisha wewe ukalipwa kodi ulokuwa ukipangisha ya nyumba ya vyumba sita...Tunachokifanya Tanzania ni sawa na kumkodisha mtu nyumba ya vyumba sita akaibomoa na kujenga Hotel kisha wewe ukaendelea kukusanya kodi yako ya mwezi kwa makubaliano ya kupangisha miaka 99 halafu anaweza kusublet nyumba yako kwa mtu mwingine.. Hii kweli inaingia akilini?
 
uchumi haupimwi kwa GDP pekee kuna mambo ya kuangalia na kuzingatia,kuna vpmo vingne,na sio kipimo hicho cha GDP.
Kuna kipindi GDP ya msumbiji ikuwa inakuwa kwa kasi ya15% per year,lakin wananchi wake ni masikin wa kutupwa.
Kwa wanauchumi watanisaidia kwa hili.
 
GDP &Per capita income is not a good measure of economic development..so those statistical data have nothing to do with the living condition of poor Tanzanians..
Definitey yes, we cannot judge our life standard by looking on the per capita income figures, which are just average estimates. How if the total GDP is possessed by a few people in the country (which is true for our country)? Those commending Kikwete for the rose of per capita income in the country MUST remember that, the figure is the result of total GDP divided by total population in the country. Even those poor people in the country are included in the calculation. Hence, we must talk more of economic development rather than relying on the economic growth trend as the late does not give us the actual trend of how a cake is divided/distributed among the population.

Yes, under Kikwete regime, I agree that the gap between the poor and rich has widened hugely to the extend that, the poorers' wealth has moved in the hands of the already rich population. How can someone commend to a leader who causes such huge discrepancy in our society? No way! Unless we get to the right direction on how to measure our economic progress, many of the Tanzanians will remain poorer as time goes on.
 
Najua sana kwamba haliwezekani lakini tuzungumzie ukweli na sii hisia. Ya kutowezekana ni wazungu wanataka sisi tufikirie hivyo lakini chenye thamani ni dhababu yetu sio fedha yao. dhahabu haiko kila nchi paper money ni udanganyifu mwingine tu.

Hawa wawekezaji wanapokuja nchini na Billioni ni mkpo wanaopewa kwa sababu sisi tumewahakikishian kuwepo kwa mali hiyo. Mali yetu hivyo pasipo kuwepo dhahabu Tanzania hawawezi kupata hayo mabillioni waliyoyapata tena basi dhamana yao inakuwa mali yetu kutokana na mkataba ambao wanahakikisha lazima mali yetu iwe dhamana na sii insurance ama accounts zao isipokuwa mkataba wetu na wao. Kwa hivyo sanbabu ni sisi na dhahabu yetu kwa nini tusiwe na ushirika na hiyo mali?

Mkuu wangu kama mimi leo naanzisha biashara kwa kumwaga hela za ukulima ktk shamba lako kwa nini nisikubali ubia ikiwa nategemea mazao yatakayotokana yatakuwa mara mbili ya uwekezaji wangu licha ya hivyo kazi zote za ukulima unazifanya wewe. Mbona wapo watu wengi tu wamewekeza nyumbani na kuwapa share washirika wao na biashara inakwenda. Tazama nyumba za Kariakoo mbona watu wanajenga kwa share za asilimia 70 kwa 30 au zaidi mradi makubaliano, lakini huwezi kuta mtu anachukua nyumba nzima akaijenga hotel kisha wewe ukalipwa kodi ulokuwa ukipangisha ya nyumba ya vyumba sita...Tunachokifanya Tanzania ni sawa na kumkodisha mtu nyumba ya vyumba sita akaibomoa na kujenga Hotel kisha wewe ukaendelea kukusanya kodi yako ya mwezi kwa makubaliano ya kupangisha miaka 99 halafu anaweza kusublet nyumba yako kwa mtu mwingine.. Hii kweli inaingia akilini?

Mkuu,

Unachokiomba na kukipendekeza naona kama ndoto vile kwanini. Mfano miradi ya uchimbaji dhahabu you need a huge capital let say around 600 Billion (assume). Bajeti ya Tanzania tu ni Trilioni 3 of which 30% of it comes from donors. Sasa nikuulize capital ya 600 Bilion utazitoa wapi? Tungelikuwa na maadili kusave serikalini tungeliweza kufanya unayoyapendekeza ila serikali za Tanzania matumizi kwenda mbele. Budget ya serikali inakuwa kila kukicha. Waarabu walikuwa wajanja walikuwa wanasave huku jamaa wanachukua mafuta kwa ubwete. Hadi walipohakikisha wameshakusanya mtaji wa kutosha wakaamua kuwa wanashare na wazungu (50-50 agreement). Sisi tunachokipata tunatumia hilo unaloliwakilisha halitawezekana labda serikali ya JK ikubali kufunga mkanda na wapinzani pia.

What next ?
 
Mkuu,

Na nyie mnatumia makosa yale yale ya kulinganisha cost of living ya mwaka 1980 na cost of living ya mwaka 2011. Gharama ya ujenzi nyumba miaka ya 1980 ilikuwa haizidi Tshs 100,000 kama sikosei au zaidi. Leo hii bila ya milioni 10 hujajenga nyumba hata ya mbavu mbili. Tunarudi pale pale mazingira tofauti. Ila labda nikuulize inflation nayo inawakilisha gharama halisi za maisha Tanzania? Inflation ni 14% mie nimenunua mkate jana sehemu nimekuta ni Shs 2800 mkate huo mwaka jana ulikuwa Shs 1000 an increase of almost 100% je kuna uwiano hapo? Utaona any economic metric inatumia benchmark fulani kuwakilisha taswira ya sehemu husika. There is no such a thing as an actual economic metric in economics. Zote zina assumption fulani ambazo they have certain weakness. However, GDP has remain a strong indicator of economic performance na ndio maana hadi kesho financial markets in US, UK, Hong Kong, Australia are using it an important indicator of country economic performance and country well being.

Tukirudi katika kumpongeza JK hebu tufanye comparison of Tanzania GDP per capital income against other nations in East Africa. In 1980 our GDP took us to the bottom of income table tukijulikana kama moja nchi maskini kabisa duniani behind the likes of Msumbiji. 2010 We are 50th poorest nation isn't that an achievement? We are just few yards behind Kenya je sio mafanikio? Wewe ukiwa wa mwisho darasani na ikatokea ukawa wa 20 darasani hutafurahi na kushukuru? Tulikuwa mkiani kiuchumi leo tuko nafasi ya 50 kwa umaskini na tunaelekea kupanda mnasema sawa sawa kweli watanzania hatuna shukrani? I beg to differ wakuu. This is a success.

in relatives to other nations tukicompare our income miaka 1980 tulikuwa nchi za mkiani kwa utajiri
Shukuran ktk huo mfano wa nyumba kujenga mwaka 1980 ilikuwa 100,000 leo hii ni millioni 10. Kwa hiyo mtu mwenye millioni 10 leo hawezi kuwa na maendeleo zaidi ya mwenye laki moja mwaka 1980 kwa sababu wote wangeweza kupata kitu kile kile.

Mahesabu ulotumia wewe ni kuonyesha jinsi tulivyotoka pato la 100,000 hadi millioni 10 kama makkuzi ya uchumi wakati fedha hizo hazimwongezei mwananchi kujenga nyumba na kibada cha kuku. Wewe ndiye unashindwa kutazama mazingira na tofauti zake kuhalalisha makuzi ya uchumi wetu. Acha mbali kwamba leo hii fedha hizo sii zetu mwaka 1980 tuliuza sisi mali yetu wenyewe hali mwaka 2010 asilimia kubwa ya mauzo sii mali yetu..
 
Shukuran ktk huo mfano wa nyumba kujenga mwaka 1980 ilikuwa 100,000 leo hii ni millioni 10. Kwa hiyo mtu mwenye millioni 10 leo hawezi kuwa na maendeleo zaidi ya mwenye laki moja mwaka 1980 kwa sababu wote wangeweza kupata kitu kile kile.
Mahesabu ulotumia wewe ni kuonyesha jinsi tulivyotoka pato la 100,000 hadi millioni 10 kama makkuzi ya uchumi wakati fedha hizo hazimwongezei mwananchi kujenga nyumba na kibada cha kuku..

Nikuulize Tanzania ilikuwa nafasi gani interms of GDP per capital in 1980 na sasa hivi iko nafasi gani in terms of GDP per capital mkuu. Relative measure? Je hayo sio mafanikio. Hivi nikuulize unazijua G7 au G20 countries zinapimwa kwa nini? Moja ya indicator zao ni GDP per capital sasa nikuulize kila mtu marekani anapata $47,000 kwa mwaka?
 
Nikuulize Tanzania ilikuwa nafasi gani interms of GDP per capital in 1980 na sasa hivi iko nafasi gani in terms of GDP per capital mkuu. Relative measure? Je hayo sio mafanikio. Hivi nikuulize unazijua G7 au G20 countries zinapimwa kwa nini? Moja ya indicator zao ni GDP per capital sasa nikuulize kila mtu marekani anapata $47,000 kwa mwaka?
Marekani kwa sasa ukiwa na mshahara wa $20,000 kwa mwaka na una familia ya watoto wawili unaishi kwenye kile wanaita poverty level.
Ukiwa na mshahara wa $11,000 na unaishi peke yako vivyo hivyo.
 
Ni kweli ameupunguza kwa maana ya calculation za mezani
Lakini kwa maana ya uhalisia wa maisha hakuna reflection yoyote zaidi ya hali kuwa mbaya kuliko kipindi unapotajwa umasikini ulikithiriri huko nyuma
Nchi hii kila kitu ni shaghalabaghala, hakuna takwimu zozote sahihi, zinapigiwa mahesabu takwimu za kubumba tu na kuja na matokeo kama hayo
But in real sense unatakiwa uje huku chini uone kama kuna reflection yoyote ya kupanda huo uchumi kwa kiasi kikubwa hivyo, FULL SANAA
 
Habari za kwenda kuwasimulia wale tunaowatembelea ulaya na marekani.yaani we acha tu
 
Back
Top Bottom