Hongera Hazina kwa kazi nzuri

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Napenda kuwapongeza wahusika wote wanaohusika na hazina kwa kutoa mishahara ya watumishi mapema kabla ya tarehe stahili; wamefanya kazi nzuri sana mwezi huu ambao bado siku chache Watanzania wataungana na watu wengine duniani kusherehekea sikukuu za Krismas na Mwaka mpya. Hongera Mawaziri wahusika, makatibu wa Wizara, Wakurugenzi na wadau wengine pokeeni pongezi hizo na mwendelee hivyo na miezi ijayo.

Mfumo Kristo @ work
 
Mohamedi Mtoi,

..hata wakati huu ambapo Katibu Mkuu ni Alhaj Ramadhan Kijjah?

..vipi kuhusu wakati waziri wa fedha akiwa ni Prof.Kighoma Ali Malima, Jakaya Mrisho Kikwete, Zakhia Meghji, na Mustafa Mkulo??

..hao mawaziri wote Waislamu nao walikuwa wakiwakandamiza Waislamu wenzao??

Mfumo kristo. Nchi inaongozwa na Pengo hii JK ni political figure tu
 
Last edited by a moderator:
wanawahi kutoa mishahara kwenye xmass lakini hawafanyi hivyo kwenye sikuu za eid, .
Mkuu Mohamed Mtoi
Idd ngapi hufanyika mwishoni mwa mwezi? Ulitaka Idd ikiwa mfano tarehe 12.mwezi wa nne basi mshahara wa mwezi wa nne utoke tarehe 10 ya mwezi huo huo wa nne?
Hata hivyo wanafanya hivyo kwa xmass na sio pasaka kwa vile sikukuu hiyo ipo mwishoni mwa mwaka na shughuli+ matumizi mwishoni mwa mwaka ni mengi, kumbuka January mwanzoni wengi hupeleka watoto shule n.k
 
Last edited by a moderator:
Mohamedi Mtoi,

..hata wakati huu ambapo Katibu Mkuu ni Alhaj Ramadhan Kijjah?

..vipi kuhusu wakati waziri wa fedha akiwa ni Prof.Kighoma Ali Malima, Jakaya Mrisho Kikwete, Zakhia Meghji, na Mustafa Mkulo??

..hao mawaziri wote Waislamu nao walikuwa wakiwakandamiza Waislamu wenzao??
huu ni ushahidi wa ki digital hauna chenga wala nini.watu wenu hawawatakii mema dini yenu.
 
Mkuu JokaKuu
kwanza hongera kuja na haya majina ya walio wahi kuwa makatibu na mawaziri wa wizara ya fedha. Natamani nikugongee like 1000 hivi.

Hata hivyo bias niliyoisema si kumaanisha eti kwa kuwa hazina pana wakristo wengi! La hasha (mimi sio muumini wa udini) ni kwa kuwa wanawahi kutoa mishahara kwenye xmass lakini hawafanyi hivyo kwenye sikuu za eid, hapo haijalishi kuwa katibu au waziri ni muislamu ama laa. Nilicho kiangalia hapo ni double standard peke yake mkuu sio ka ulevi ka udini.

Hongera tena great thinker JokaKuu kwa comment yako ambayo inajibu vizuri hoja ya mtu ambae labda angeuliza akiwa na tingasi la udini kichwani.

Bado hujajibu, vipi ikitokea eid ni tar 10 ya mwanzo wa mwezi, Hazina wafanye nini??
 
Last edited by a moderator:
Hongera yako sijui ilimaanisha nini kwani ni mishahara bado haijatoka na haileweki ni lin itatoka, kwa sbb nasikia haina pesa. hivyo wansubiri makusanyo ndiyo walipe hiyo mishahara,
 
Tatizo hazina wako bias! Sikukuu za kiislamu huwa hawawahishi kutoa mishahara na hili nina ushahidi nalo imetokea hivyo mara kadhaa kwenye sikukuu ya eid.
Mkuu Mohamedi Mtoi hii tuhuma ni nzito sana,fafanua kidogo maana inalete chuki miongoni wa watanzania!Mimi huwa nakuheshimu sana kwa michango yako hapa JF,lakini leo umenishitua kidogo!
 
Mohamedi Mtoi,

..hata wakati huu ambapo Katibu Mkuu ni Alhaj Ramadhan Kijjah?

..vipi kuhusu wakati waziri wa fedha akiwa ni Prof.Kighoma Ali Malima, Jakaya Mrisho Kikwete, Zakhia Meghji, na Mustafa Mkulo??

..hao mawaziri wote Waislamu nao walikuwa wakiwakandamiza Waislamu wenzao??

Hilo ni ghubu la ushari, si uchungu wa dini si lolote!
 
Mbona akaunti zingine bado?nina uhakika wa kuwa mshahara utaingia baada ya x-mass .Huyu mleta mada alipima upepo wa wachangiaji tu.
 
Nashangaa mtu kutoa hongera kwa kitu cha kawaida. Ni kama kumwambia mtu "hongera kwa kutotoka nyumbani kwako uchi"!

Hii ndicho Watanzania walicholishwa na watawala kwa kudhani wajibu wa serikali na watendaji wake kwa umma ni hisani
 
Hongera yako sijui ilimaanisha nini kwani ni mishahara bado haijatoka na haileweki ni lin itatoka, kwa sbb nasikia haina pesa. hivyo wansubiri makusanyo ndiyo walipe hiyo mishahara,

Mie si mwanasiasa mkuu. Nilichosema ni ukweli 100%, uliza jamaa zako walioko katika halmashauri mbalimbali utaambiwa ukweli huu. Watu wamevuta karibu zinaisha hata kabla ya Xmass! Kama huko kwenu bado muulizeni mwajiri wenu.
 
Back
Top Bottom