Hongera Gelard Hando

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Hongera broda!! kwa kuwachana wanabodi wote walikuwapo rasmi kwenye bodi ya kuutangaza mlima kilimanjaro katika maajabu 7 ya dunia.

Kawachana mno, na kadai bodi ilikuwa inakaa kimyakimya. Wizara ya utalii kila uchao ni matatizo tu..., mara wameuza wanyama, mara kujenga hoteli mbugani, mara kunyang'anyana vitalu vya uwindaji...kila siku viroja tu. Mambo muhimu na kitu kidogo kama kuhamasisha upigaji kura kwa mlima kilimanjaro wameleta siasa. Vyombo vya habari vimejitahidi lakini maswali yanayotoka kwa raia inaonyesha kabisa wizara haikujiandaa kuutangaza.

Matokeo yake dakika ya mwisho wanaaichukua sauti ya Waziri Mkuu halafu wanaitoa eti kuhamasisha, mara kampuni za simu dakika mwisho ndo wanaachia msg free eti kuhamasisha. Whaaaaaaaat??

Wameshindwa kuwaangalia South Afrika ambao wameshinda table mountain ambayo ni sawa na kichuguu tu kwa mlima kilimanjaro, wao Tv zilienda mpaka kileleni kuutangaza, sie tumebaki na siasa tu kutuma msg mtu eti anachajiwa, radio, tv wala hazikupelekewa taarifa za kutosha,mambo mengi yameenda hovyohovyo. Table mountain ya South inapandwa kwa kamba tu wakati mlima wetu unapanda siku 6 na bado hujafika kileleni.

Poor waandaaji, Poor management, Poor Bodi....sasa wasouth wanazidi kujitangaza baada ya kitu kidogo tu kuhamasishana na mlima kichuguu chao kimeingia maajabu ya Dunia, sie tumebaki kuwindana na kuuana kwa kugombania vitalu vya uwindaji tu....Whaaaaaaaat????
34eytsh.jpg
33okvn5.jpg

Cheki chini kilimanjaro yetu inavyopendeza..!!

2cqz2fo.jpg
 
Hoja zake kuhusu Table Mountains hazikuwa na msingi. Kwa maoni yangu angeweza kuzungumzia udhaifu wa Wizara husika na Bodi ya Utalii bila kujenga hisia za kijinga na chuki kuhusu Table Mt.

Wakati mwingine huwa nakerwa na uwezo wa kuelewa na kuchambua "issues" wa Bw. Hando.
 
Mkuu tunavuna tulichopanda. Haya ndiyo matunda ya kukosa vision na team work kwenye mambo ya kujenga nchi. Subiri watatoa visingizio vingi tu. Mara watanzania hawana simu, hawako kwenye mtandao, mara Wasouth wana fedha etc.
 
Hoja zake kuhusu Table Mountains hazikuwa na msingi. Kwa maoni yangu angeweza kuzungumzia udhaifu wa Wizara husika na Bodi ya Utalii bila kujenga hisia za kijinga na chuki kuhusu Table Mt.

Wakati mwingine huwa nakerwa na uwezo wa kuelewa na kuchambua "issues" wa Bw. Hando.

Hoja aliyoisongesha hapa ni kwamba inakuaje table mountain inashinda wakati mlima wetu ni zaidi ya table?? sasa hapo tatizo sio table mountain(kichuguu) tatizo ni bodi ya uhamasishaji...ambayo Hando ndio alikuwa anaishambulia, hawakujiandaa vya kutosha pamoja na wizara husika.
Kwa mawazo yangu yako na yake zipo sawa tu in straight line..ina mashiko
 
hasira zote za nini mkuu? Hivi uko unatembea ghafla unamuona mwehu anatukana we mtu mzima na akiili yako unaanza kumfokea, si ni kupoteza muda tu. Ni afadhali tulivyokosa kabisa ili pengine watu watajifunza. Mie nilijua hiyo issue bado siku nne kura kufungwa tena nilishtuka kusikia hilo la Pinda kuwa mchakato ulianza tangu 2009.

Masaburi tupu yapo pale Maliasili, hata hivyo tusiwalaumu sana maana wakubwa wote waliopo pale Maliasili ni Luhanjo cohort, nani atathubutu kuwasema? Pinda mwenyewe anajua hata iweje ktk utendaji wake, hana ubavu wa kumsimamisha kazi mkurugenzi yeyote au KM ktk wizara za serikali coz hajawaweka yeye.
 
Kwani madini yetu gesi na samaki wetu baharini pamoja na uranium ni nani amevipigia kura? mijadala mingine ni upuuzi na uvivu wa kufikiri, Tanzania haiitaji hizo promo tuna kila kitu ila vinanufaisha wajanja tu.
 
Zile Tsh.300 kwa kila meseji ni nani aliyekula? Ni bodi hiyo au wizara?
 
Kwanza sikuona umuhimu wa kuingia katika mchakato mzima na kupoteza pesa nyingi kwa ajili ya kugombania kitu ambacho wala hakina faida kwetu,mlima tunao na unajulikana duniani hivyo kuingia katika maajabu 7 au kutoingia hatukusaidii kwa lolote.

Ningeona umaana wa kufanya hivi kama tu tungekuwa tunautangaza mlima wetu na vivutio vyetu katika kujitangaza na kupata watalii na si kugombea mlima wetu uonekane wa ajabu.
 
angeliaza kwanza kwa kuuponda utawala wa serikari wanayoitete sana ndio siku zote angejua ni watanzania wengine wanasema siku zote, utawala uliokaa siku nyingi hauwezi kuwa na jipya zaidi ya kutawala kwa mazoiea tu
 
hapo lakini ndio wajue hawana ubavu wa kushinda kwenye ushindani wa kweli, labda tume ingekuwa uya majaji wetu uchwara
 
Kwa kweli ukifiika Mlima Kilimanjaro utasikitika! Nilipanda tarehe 7 Agosti, mwaka huu kwa 'day hike' nikakuta yafuatayo:

1. Maaskari (ranger) wamelewa.
2. Makarani hawana ushirikiano kwa wapandisha mlima.
3. Wafugaji wanakata majani ya mifugo
4. Watu na mashoka wanakata magogo kwa ajili ya kuni.

Haya pekee yanatosha kudhalilisha Mlima Kilimanjaro.

TANAPA na KINAPA hawafanyi juhudi yo yote ya kuhifadhi mlima huo. Inashangaza Waziri Mkuu anapotangaza kwenye vyombo vya habari
kuutangaza Mlima huo bila kukemea hayo.
 
Hao waandaaji wa hizo kura niwapuuzi. kama maajabu yanaamliwa kwa kura basi hayo sio maajbu labda waite jina jingine. Kwanza utachaguje kitu wakati options pinzani huzijui. Poleni mliopiga kura hamkujua mnachangia mitandao ee? huo ndo ubepari baba na huo undo ubunifu. Msiwe mnadandia vitu bila tafakari dunia ya wajanja hii. Na mgeshinda mgepatanini? poleni. Mmekumbana na babu wa loliondo wa kimataifa.
 
mlima kilimanjaro kwa asili una maajabu
hatuhitaji hawa wazandiki wa kigeni kuupaka sifa ya maajabu kwa kura za watu
uasili wake hautaisha milele na milele.
 
Hoja aliyoisongesha hapa ni kwamba inakuaje table mountain inashinda wakati mlima wetu ni zaidi ya table?? sasa hapo tatizo sio table mountain(kichuguu) tatizo ni bodi ya uhamasishaji...ambayo Hando ndio alikuwa anaishambulia, hawakujiandaa vya kutosha pamoja na wizara husika.
Kwa mawazo yangu yako na yake zipo sawa tu in straight line..ina mashiko
height haikua kigezo mkuu, si kila kirefu basi kiingie kwenyee maajabu, huo ni udhaifu wa kujenga hoja

we failed to show the world kwamba we have something special, and south african succeeded
 
mlima kilimanjaro kwa asili una maajabu
hatuhitaji hawa wazandiki wa kigeni kuupaka sifa ya maajabu kwa kura za watu
uasili wake hautaisha milele na milele.
good point mkuu

we usually do that hata kwa wake zetu kuwakataza hata kupaka mafuta kwani hawana haja ya kupendeza huko nje kwani sie waume zao tupo, i take a mickey out of your statement
 
Jamani mbona thread nyingine zinakuwa km za chei-chei shangazi ! Hando ni nani na kasema nn ?? Mwaga basi ndiyo tuone hongera zako zinafaa au ??

Hoja zake kuhusu Table Mountains hazikuwa na msingi. Kwa maoni yangu angeweza kuzungumzia udhaifu wa Wizara husika na Bodi ya Utalii bila kujenga hisia za kijinga na chuki kuhusu Table Mt.

Wakati mwingine huwa nakerwa na uwezo wa kuelewa na kuchambua "issues" wa Bw. Hando.
 
Jamani mbona thread nyingine zinakuwa km za chei-chei shangazi ! Hando ni nani na kasema nn ?? Mwaga basi ndiyo tuone hongera zako zinafaa au ??

Samahani Mkuu, ulipaswa kusoma post ya kwanza ambayo inajieleza vizuri tu.
 
Back
Top Bottom