Hongera Eng. Hersi kwa kusajili top players

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,667
Yes lazima jamaa apewe kongole zake baada ya makosa mawili matatu pale mwanzoni kwa kuwaleta kina Yikpe, Sarpong, Urikhob, Juma balinya na kushindwa kutoa matokeo chanya mwamba alijipanga na kurudi na wachezaji wenye ubora Afrika.

Sio Ajabu leo timu zote za Afrika zinapiga hodi pale Yanga kutafuta sahihi za baadhi ya wachezaji hili hakika linahitaji pongezi.

Ukitoka mtandaoni ukirudi utasikia Al ahly wanamtaka Bangala mara Berkane wanamtaka Lomalisa, mara Kaizer chiefs wanamtaka Mayele, Mara Arsenal wanamtaka Bacca yani ni full utamu hili limeprove Yanga walikua bora sana.

Why not Simba au Azam, ukinitajia tetesi zozote za mchezaji wa Simba au Azam kutakiwa na timu yoyote hapa Tanzania au Afrika zaidi ya timu za Armenia tena hazijulikana hata jina ntakupa like mtoa taarifa.

Bado sijasikia habari za Diarra mdaka mishale ila ndio bado dirisha li mapema tunaweza kusikia hata kesho tetesi Man city au Burnely wanamtaka. My advice kwa injinia timu zikija na dau kubwa waachie vijana wakatafute malisho sehemu nyingine.

Soka letu bado kiuchumi halipo vizuri bado hatupo kwenye level za kupambana na timu kubwa zenye uchumu kubwa kwenye ishu ya kugombania wachezaji, bado tuna msuli mdogo.
 
Ukitoka mtandaoni ukirudi utasikia Al ahly wanamtaka Bangala mara Berkane wanamtaka Lomalisa, mara Kaizer chiefs wanamtaka Mayele, Mara Arsenal wanamtaka Bacca yani ni full utamu hili limeprove Yanga walikua bora sana.
Kama ni uchambuzi basi hapa umechambua dagaa apostle
 
Yanga hii itawatesa Makolo kwa miaka elfu 10 kama sajili zao ni za wachezaji aina ya Sawadogo.

Waache waendelee kufurahia uzuri kila mchezaji anayeondoka Yanga kuna mwingine mzuri zaidi kwa kifupi Yanga hakukua na Star labda Mayele kidogo.
 
Kutoka nbc premier league kwenda epl Moja kwa Moja ni sawa na kutoka primary kwenda chuo kikuu.... Kuna stages inatakiwa kupita, samatta alipitia hizo stages ila epl alichemsha

Afu wazawa wengi hawapendi kuchezea nje, washazoea huku bongo shobo nyingi mwendo wa kupewa bia za ofa, kuombwa selfies na kupewa nyapu za Bure
 
Hao wote pamoja na wewe pitieni notes za Shaban Nonda ndio mje hapa.

Unatutajia nonda sijui nondo kacheza Galatasaray hata uropa haina
Samata mtanzania kacheza simba kacheza mazembe mchezaji Bora Afrika kacheza Aston Villa timu yenye Uefa hata arsenyeto hana kacheza Uefa kawafunga Liverpunyeto inatosha bana
Taja chezaji la UTO lenye cv kama hyo Bangladesh bin pakistan
 
Wewe jamaa kama sio utoto basi kuna shida mahala
 
Back
Top Bottom