Hongera CCM mpya na Halisi kwa Ushindi Mzito; ni salaam tosha kwa Chadema na Mafisadi

CCM Mpya, CCM ya zamani, CCM ya mafisadi???? CDM??? mbona unajichanganya? CCM imeoza, ccm imezeeka beyond repair hata mngeipa majina mazuri kiasi gani.............

Huo ndio ukweli.CCM imeoza kabisa
 
CHADEMA imeweza kutetea kata zake mbili, na kuongeza zingine tano. hapo utajua nani kapoteza. unakurupuka wakati umevaa bikini bana...............
 
Acheni kujidanganya, kwa taarifa yenu hamuwezi EL. Kesha wagaragaza kwenye chaguzi zenu za jumuiya na sasa ameishika NEC mkononi mwake.

Kilichosalia ni kushughulikia vitatizo vidogo vidogo kama vyenu, ambavyo hata haitaji kuumiza kichwa kuvifikiri. Mbwa ukishamng'oa meno yote na kumkata kucha zote hatakubabaisha tena wala hutashtuka hata akikuvamia.

Maana atakapoamua kukung'ata badala yake atajikuta amekupiga busu tu. Nyie bwekeni tu lakini hamna mnaloweza kulifanya ndani ya CCM. Mwisho wa siku mtafyata mikia na kuanza kulamba miguu ya mafisadi. Nawaambia hamuwawezi, acheni ndota za alinacha.
 
Mleta mada, mbona kimahesabu ccm haijashinda kwa asilimia 95 kama unavyotaka tuamini.
Viti vilivyopigombewa ni 29. ccm imepata 23 kihesabu ni 23/29 X100= 79.3 (79.3%); hii ndiyo asilimia ya viti vyote.
Kama ccm ilikuwa inatetea viti 26 na imepata viti 23 kimahesabu imepoteza viti 3 kiasilimia itakuwa imepoteza 3/26 X100=11.53 (11.53%). Hivyo usituletee hesabu za kufikirika, na hili ni pigo kwa ccm kwani, unaponyang'anywa kiti hata kimoja jaribu kujiuliza kulikoni! Kuliko kubaki ukijisifia, wakati umepoteza, au ccm haikuvitaka hivyo viti ilivyokuwa inavikalia;na sasa imenyang'anywa??

Unahangaika naye, hata hesabu haijui...achana nae mkuu.
 
Kura moja (1) ya ndiyo kwa upinzani ina thamani kubwa kuliko kura 99 za ndiyo kwa magamba.
 
Ushindi Mzito wa zaidi ya 95% asilimia katika chaguzi ndogo ni ishara tosha kuwa CCM Halisi imedhamiria kukijenga chama katika ngazi ya matawi na mashina na hivi karibuni mapinduzi makubwa yatafanyika katika ngazi ya Taifa.

Hongereni wana CCM wote na Wananchi wote wapenda amani na maendeleo kwa kuifanya CCM mpya kuendelea kuwa Chaguo lenu la kwanza katika kuongoza dola na kuleta maendeleo.

CCM Halisi haijutii kupoteza au kushindwa katika kata za Udiwani za Daraja Mbili Arusha, Rombo,Mtibwa kwani Mafisadi wanaopigwa vita na CCM Halisi walisimamisha watu wao kwa malengo yao binafsi ikiwa ni pamoja na kukihujumu chama kwa mfumo wa kisayansi na kukipa maujiko chama pinzani cha chadema kwani wao lao ni moja. kwa maana hiyo tunapenda kuwapa pole wananchi wote wakata hizo kwa kuingizwa katika mitego ambayo hawakuigundua mapema.

CCM mpya na halisi itafika katika kata hizo na kufumua uongozi kuanzia ngazi ya shina na tawi na kutoa elimu ya siasa na maendeleo kwa wananchi hao.

hakuna ushindi kwa CCM hata kwa sekunde.Vitisho wanavyotumia ndiyo vinawapelekea watu wasijitokeze kupiga kura.
Tunashukuru hata mnayafanya haya mapema.Tutazidi kuwajengea wananchi ujasiri,na mwisho wenu ni sasa.

Kumbukeni ujasiri unajengwa kwa hatua.Eauwaji wakubwa ninyi wanaCCM na wote mnaoishabikia,hakuna kitu chema ilichowafanyia,labda kwa mtu ambae hajui dunia inavyokimbia leo.

CCM mnataka kutupumbaza mpaka lini?
Mr Emmy pole sana,msimba utakao lia hakuna atakaekubembeleza.
 
Ushindi Mzito wa zaidi ya 95% asilimia katika chaguzi ndogo ni ishara tosha kuwa CCM Halisi imedhamiria kukijenga chama katika ngazi ya matawi na mashina na hivi karibuni mapinduzi makubwa yatafanyika katika ngazi ya Taifa.

Hongereni wana CCM wote na Wananchi wote wapenda amani na maendeleo kwa kuifanya CCM mpya kuendelea kuwa Chaguo lenu la kwanza katika kuongoza dola na kuleta maendeleo.

CCM Halisi haijutii kupoteza au kushindwa katika kata za Udiwani za Daraja Mbili Arusha, Rombo,Mtibwa kwani Mafisadi wanaopigwa vita na CCM Halisi walisimamisha watu wao kwa malengo yao binafsi ikiwa ni pamoja na kukihujumu chama kwa mfumo wa kisayansi na kukipa maujiko chama pinzani cha chadema kwani wao lao ni moja. kwa maana hiyo tunapenda kuwapa pole wananchi wote wakata hizo kwa kuingizwa katika mitego ambayo hawakuigundua mapema.

CCM mpya na halisi itafika katika kata hizo na kufumua uongozi kuanzia ngazi ya shina na tawi na kutoa elimu ya siasa na maendeleo kwa wananchi hao.

Hivi wewe, Mbona hueleweki, juzi tu ulikuwa unalia lia baada ya uchaguzi UVCCM,leo tena unaibukia huku, Walah utaliwa mapema sana weye, maaana una kihere here hicho
 
mr emmy alijaribu kuingiza kamtaji kake ka m2 ili ahonge kupata uongozi ccm vikaliwa na kambi ya lowasa ikalamba kiti kwa hiyo ana hasira sana.
mi namshauri arudi saccos akakope aendelee kukuza kamtaji kake ila siku nyingine ajue ccm ni zimwi ambalo halimjui mtu.
 
Back
Top Bottom