duuu si lazima kupost jamni!
Hakuna mtu anayeitwa Mama wa nyumbani, bali ni wewe tu kama utapenda iwe hivyo. Baada ya kuoana unatakiwa kumwanzishia kitu asimamie na kujishughulisha, mfungulie hata Genge ili aone machungu na ugumu wa kutafuta pesa. Kosa ambalo watu wanafanya pale anapoa na kushika hatamu zote za utafutaji wa pesa katika familia, wakati mother house akibaki ktumia tu!!! Kwa maana hiyo hajui machungu ya utafutaji wa pesa, kwamba kuna siku unakosa na kuna siku unapata. Hata kama una ajira ya kudumu, kuna siku mshahara unachlewa, ukiupata unaishia tarehe 15. Ukweli ni kwamba kama mmoja wa familia ndiye mtafutaji mkuu, mwenzake anakuwa hajui ugumu wa kupata hiyo pesa- taa za umeme zinawaka mpaka saa 4 asubuhi, maji ya bomba kama yako ndani yakifunguliwa hayafungwi, chakula kitapikwa zaidi ya walaji ili wajirani waone kuwa tunazo.