Hoja ya Mnyika kuhusu Katiba Mpya iungwe Mkono

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,741
218,330
Kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba Katiba Mpya inapatikana kabla ya Uchaguzi wowote ule , hata kama kutakuwa na gharama nyemelezi .

Ujumbe wake huu hapa

Screenshot_2023-08-22-16-13-57-1.jpg
 
Kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba Katiba Mpya inapatikana kabla ya Uchaguzi wowote ule , hata kama kutakuwa na gharama nyemelezi .

Ujumbe wake huu hapa

View attachment 2725250
Naunga mkono HOJA 🙏🙏

Nimekuwa nikisema kitambo sasa humu kuwa, Kuna hatihati uchaguzi kuyeyuka.

Ni kheri kusogeza mbele uchaguzi tupate tume HURU na KATIBA mpya kuliko KURUDIA Yale ya 2020!!

Siasa ni sayansi, na sayansi ni HESABU!!
 
Naunga mkono HOJA

Hakika
 
Chadema inataka Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi
Hapa ndipo mvua itakapoanza kuwanyeshea kama hamtakuwa makini sana.

Mtaanza kuwa kama mnababaika na hamjui nini la kufanya. Leo hili, kesho lile.

Mliweka msimamo ulioeleweka huko siku za nyuma, kwamba hapatakuwepo na uchaguzi wowote bila Katiba Mpya, na Tume huru ya Uchaguzi.

Mlitakiwa kushikilia hapo hapo na kuliwekea uzito mahali popote kwenye mikutano yenu, ili wananchi wasiwe na mashaka yoyote juu ya msimamo wenu.

Mwenyekiti alipoanza kuyumba, chama kikaanza kuwa na mashaka na adhimio lile.
Tukawaeleza Samia swala la Katiba Mpya kisha lizima, nyinyi hamkuelewa!

Kitakachowasaidia sasa ni hili la Bandari, mkiliunganisha vizuri na hayo matakataka mengine wanayofanya CCM, hata chini ya Katiba hii iliyopo CCM hawatoboi.

Mtasema Katiba hii inamfanya Rais awe mungu. Huyu mungu hawezi kushindana na nguvu za wananchi wakishawaelewa na kuamua kuwaondoa CCM.

Kumbuka, ni CCM watakaoanza vurugu, hata uchaguzi ukifanyika chini ya hii Katiba iliyopo. Anayefanya vurugu ndiye atakayedhibitiwa.

Sasa nawaomba, acheni kuwachanganya akili wananchi. Ni lazima msimamo wenu uwe wazi kabisa, wananchi na dunia yote ijue hivyo.
 
Back
Top Bottom