Hoja ya Lissu ya kukataa marekebisho ya sheria yaungwa mkono na wabunge wa CCM

Tundu Lissu is an excellent lawyer. Hivi ccm hawana vikao vya ndani vya kufanya postmortem ya performance ya Wabunge wao? Ndoa ya mkeka Kati ya ccm na cuf ni bomb. Habibu Mnyaa, Mary Nagu na Werema wanatia Kinyaa! Yes waache za kuleta. For sure ccm iko in its deathbed and sooner or later my words shall become true. Hakuna Rais wala waziri Mkuu, spika aw Bunge ni uharo, Ag ni almost chizi, haya mambo wanakurupuka tu they don't have a work plan. Jana nilimwona Juha Kalulu(JK) akifungua FNB huku akilia watu wapewe mikopo nafuu. Watu wanakula kwa mgomo wa Madaktari Haka kajamaa kanazindua Bank! You only need a functional BOT watakaoweza kuweka na kusimamia interest rates. Wanacholia wakulima na wajasiriamali sio ukosefu bank Bali ni sera sawia za interest rates period na sio kuwa na utitiri wa Banks.
 
Kwa hiyo kinachokuuma ni Lisu kupongezwa hapa JF au? Tatizo ni kuwa nyie wanaccm hoja zenu huwa ni kuchangia kwa unafiki ndo maana sasa hivi watu hawaamini sana. Mimi nawapongeza wote Lisu na ndugulile.

Nani mwana CCM wewe? Futa kauli yako, wengine hatuna vyama. Nilichoandika hapo ndiyo sahihi wala si kuumwa kwa kupongezwa Lissu. Yeye alipomaliza hotuba yake naibu spika aliendelea na utaratibu wa watu kuchangia kama kawaida. Ndugulile alikuwa mchangiaji wa kwanza. Ndiye aliyetibua mambo. Wewe unaona raha mtu kupewa sifa ambayo hakustahili. Alichofanya Lissu ni kumkumbusha tu spika kuhusu vifungu vya kanuni. Muwe mnafuatilia mambo kwa makini na kuandika kwa uhalisia.
 
Hapo kwenye red: Kama Lissu hakutoa ufafanuzi muswada ungepita?

Palipo na ukweli wa wazi lazima uwekwe bila upendeleo. Sisi ambao hatuna vyama hutoa sifa kwa mbunge yeyote anayefanya vizuri bila kujali itikadi yake ya kisiasa. Sisi tuliokuwepo pale tulisha jua kuwa muswada unakwama kabla hata Lissu hajamkumbusha naibu spika vipengele vya kudumu vya kanuni za bunge. Hali ya hewa ilisha chafuka bungeni kwani kelele zilikuwa nyingi. Alichoandika mleta thread katika kichwa cha habari yake si sahihi, amewapotosha watu. Nao wanakuwa wakali kwa sababu thread inampa sifa mwana CDM mwenzao. Hawataki kuambiwa ukweli halisi ulivyokuwa. Kumbe hapa hata ukileta habari ya uongo inayompa sifa kiongozi wa CDM watu watatoa big up zao kwa nguvu hata akitokea mtu akawaambia "jamani hilo si la kweli" watamwita mnafiki huyo! Katumwa. Huu ni ushabiki uliopita kiwango cha ushabiki na kuwa ujinga. Ukweli halisi ulikuwa hivi: Si kweli kuwa hotuba ya Lissu ndiyo iliyokwamisha muswada wa sheria mbalimbali usijadiliwe kama mleta thread alivyopotosha. Baada ya hotuba ya Lisu, naibu spika aliendelea na ratiba kama kawaida kwa wachangiaji wa hoja kuanza kuchangia. Mchangiaji wa kwanza alikuwa Faustin Ndugulile, huyu ndiye aliyekuwa mwiba na kutibua mambo, mleta thread hakuliona hili. Baada ya utata wa hoja hiyo kuibuka na upande wa serikali kuomba kitolewe kipengele cha sheria ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu tu. Ili vipengele vingine viendelee kujadiliwa. Ndipo Lissu aliposimama na kumkumbusha spika kuwa kanuni za kudumu za bunge haziruhusu muswada kujadiliwa vipande vipande. Hapa utaona wazi kuwa, Lissu alikuwa anajazia uzito hoja ya Ndugulile na wala si hotuba yake kama mleta thread alivyowapotosha. Baada ya hapo ndipo naibu spika aliposema wazi. Kutokana na hoja ya Ndugulile kuungwa mkono na wabunge wengi. siyo hoja ya Lissu, wabunge wataulizwa ili waseme wanaafiki muswada huo uondolewe au la. Japo yeye mwenyewe kanuni zinamruhusu kutoa maamuzi..Shida yangu hapa siyo kupongezwa Lissu hapa JF. Nachotaka ni ukweli, watu wapongezwe kwa kile walichofanya bila kujali wanatoka chama gani. Hapa Lissu tunaweza kumpongeza kwa hotuba nzuri ya kambi rasmi ya upinzani bungeni na siyo kwa hoja ya kukwamisha muswada usijadiliwe. Huo ndiyo ukweli. Si sawa kukakamaza shingo kwa kumpa pongezi mtu asiyehusika.
 
Lissu ana kila haki ya kuungwa mkono kwa sababu m/sheria wa serikali katoa hoja ikaungwa mkono na kamati ya sheria na utawala na baadae Lissu akaja akaeleza mapungufu ya hoja hiyo na mwisho akasema haungi mkono hoja.

Alipokuwa akichangia alienda kwenye msimamo uleule wa Lissu, na akatoa hoja ya kuahirisha mjadala, mgongano wa namna ya kuuahirisha mjadala aliyetoa msimamo na way forward ni Lissu hata pale cuf na serikali walipokuwa na msimamo wa aina moja.

Na kura zikapigwa, hoja ikaahirishwa mpaka mkutano wa mwezi aprili.

Je juhudi za Lissu hazionekani mpaka hapo?
 
Nani mwana CCM wewe? Futa kauli yako, wengine hatuna vyama. Nilichoandika hapo ndiyo sahihi wala si kuumwa kwa kupongezwa Lissu. Yeye alipomaliza hotuba yake naibu spika aliendelea na utaratibu wa watu kuchangia kama kawaida. Ndugulile alikuwa mchangiaji wa kwanza. Ndiye aliyetibua mambo. Wewe unaona raha mtu kupewa sifa ambayo hakustahili. Alichofanya Lissu ni kumkumbusha tu spika kuhusu vifungu vya kanuni. Muwe mnafuatilia mambo kwa makini na kuandika kwa uhalisia.

Heshimu kukinzana kwa maoni, usiyabinafsishe hayatatoa taswira yako sahihi. Kumbuka Beuaty is in teh eyes of the beholder. Tukubali kutofautiana tunapotazana na kusikia kitu. MIMI NAONA WOTE MKO SAWA kulingana na mitazamo yenu.
 
Asante lissu kwa kutujuza mapungufu hayo,ila waheshimiwa hasa wa ccm wekeni maslahi ya taifa mbele na sio ya chama,zamani mlikuwa hamsomi kabisa mlikuwa mnapitisha tu mambo ndio haya yametufikisha hapa tulipo.kuweni makini jamani kama wabunge wa chadema,ndio maana mnajikuta mnashindwa hata kusimamia ukweli kwa kuhofia hili limesemwa na chadema tukilikubali tutakuwa wasaliti ,jamani sie na nyie wote ni watanzania tuwe wazalendo kama hili mlilofanya jana mmetufurahisha sana watanzania.endeleeni na ushirikiano huo katika mustakabali wa nchi yetu msione aibu palipo na ukweli mkatae mjenge nchi yetu.mungu ibariki tanzania.
 
Heshimu kukinzana kwa maoni, usiyabinafsishe hayatatoa taswira yako sahihi. Kumbuka Beuaty is in teh eyes of the beholder. Tukubali kutofautiana tunapotazana na kusikia kitu. MIMI NAONA WOTE MKO SAWA kulingana na mitazamo yenu.

Sawa kabisa, mara nyingine CDM HOYEEE! na CCM pia HOYEEE!
 
Back
Top Bottom