Hoja ya kwamba hamna Mungu muumba ni hoja Dhwaaif

Mufti kuku The Infinity

JF-Expert Member
Sep 21, 2019
5,690
8,931
mbele yako akiwa na mwili wake unao jumuisha chembe (cells) takriban trilioni 37, na kila seli ina madaraja, viwanda, na mfumo tata wa kuweka misimbo ambao umefafanuliwa katika kanuni za urithi.

Na anakutazama kwa macho yake ambayo yana mfumo tofauti wa kupiga picha wa rangi, kwa usahihi wa ajabu wa takriban Megapixel 576, zenye utaratibu wakufikirika wa kuhifadhi picha zinazosonga na tuli, na hata kuzitafsiri kwa kutumia ubongo na kuzichanganua kwa muda usiozidi sekunde moja..!

Na kwa mwili wake wa wastani, ambao una simamiwa na misuli 640, akisahau moyo wake,ambao umekuwa ukifanya kazi kwa miongo kadhaa,mchana na usiku, katika usingizi na kuamka,bila kuacha au matengenezo ya nje..! Kisha amri hiyo inatolewa kutoka kwa akili yake, ambaye sehemu zake za kisayansi ziliandikwa, na bado kuna utata ndani yake..!

Kwa kusogeza ulimi ulioshikamana na taya na misuli kumi na saba..! Kukuuliza kwa akili isiyo ya kawaida: Uko wapi ushahidi wa kuwepo kwa Muumba......!

Asifiwe Mwenyezi Mungu Muumba wetu
 

Attachments

  • 1670494091328.jpg
    1670494091328.jpg
    31.9 KB · Views: 3
Sayansi ndio iliyoelezea habari za mfumo wa cells na mwili wa mtu kwa upana wake

Sayansi hiyo hiyo ambayo umetumia maneno yake kama reference kwasababu unaikubali kuwa ipo sahihi, kumbuka ndio sayansi hiyo hiyo iliyopinga habari za uwepo wa Mungu.

Ebu jaribu kufikiria kidogo, pamoja na vitu vyote hivyo vinavyozungumzia mfumo wa binadamu wa ndani mpaka nje ambavyo kwako vinaonekana ni very complex lakini bado sayansi hiyo hai-link swala hilo na habari za Mungu.

Pengine tungeitegemea kuiona Sayansi inakuwa ya kwanza kututangazia habari za Mungu kutokana na kile ilichoweza kukibaini kupitia tafiti zake zinazo shangaza, lakini haijawa hivyo.

Au kama Sayansi ilikuwa imejipanga tangu mwanzo kutokubali uwepo wa Mungu basi ingetuepushia mbali na hizi siri zilizopo ndani ya mwili wa binadamu ambazo watu wakianza kufikiria uchakataji wake wa kazi ulivyo wa ajabu wanaweza kufikia jibu la Mungu. Lakini kwanini ikaendelea kuweka vitu wazi?

Sasa hapo una machaguo mawili

  1. Ni eidha ukubali kuwa sayansi sio ya kweli (ambapo itakuwa ni pamoja na zile habari za cells ulizozichukua kama hoja za kweli)

  2. Au ukubali kuwa sayansi ni ya kweli kwasababu inatoa maelezo ya kweli na kwakua Sayansi hiyo hiyo imepinga uwepo wa Mungu basi jambo hilo lazima liwe kweli (kitu ambacho huwezi ukakubali)

Nikijiweka katika nafasi yako kiukweli naona upo umuhimu wa kuwa na machaguo mengi zaidi ya mawili

Kwa bahati mbaya ni kwamba unavyozidi kuongeza machaguo unazidi kulazimisha majibu yale unayoyataka wewe, majibu uayoyataka wewe ni pamoja na yale yasio sahihi.

Utachagua hizo option mbili ambapo kati yao kuna jibu sahihi au utavuruga mtririko wa hoja kwa kujiongezea options nyingine zaidi ili kuruhusu majibu yanayo kuridhisha? (yasio sahihi)

Uchaguzi ni wako
 
Back
Top Bottom