HOJA BINAFSI: Maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yaahirishwe

mchemsho

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
3,212
867
Nadhani itasaidia. Kwa sasa hali ya uchumi hasa mdogo (micro-level) ambao ndio hasa unawagusa wananchi wa chini moja kwa moja imekuwa mbaya sana, huku mfumuko wa bei nao ukipaa kwa kasi ya ajabu, hii imesababisha kupanda kwa bei za bidhaa muhimu kama vile mafuta, sukari na vyakula vingi, kwa upande wa pili pato la mwananchi limebaki kuwa lile lile la zamani au linazidi kupungua hivyo kuwapa wananchi wakati mgumu, wengi hawana tena hata uhakika wa ile milo mitatu kwa siku. Kwa upande mwingine serikali imetenga na inaendelea kuteketeza mamilioni ya shillingi eti kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 5
ya uhuru, bila kuchukua hatua za dharura kuunusuru uchumi unaolekea icu. Binafsi naona kama serikali inajitegea bomu yenyewe linaloweza kulipuka mda wowote, sina uhakika mfumuko wa bei utakuwa umefikia asilimia ngapi. Hofu yangu ni kwamba sijui nini kitatokea hiyo 9 disemba kama wananchi wataamua siku hiyo kudai upya uhuru wao wa kweli kutoka kwa genge la watawala mafisadi. Tusubiri tuone, Naomba kuwa silisha.
 
walivyo wapuuzi hawwezi kukusikiliza kaka........we ona hayo masherehe kila wizara yametafuna kiasi gani??!!!nchii hii inashangaza kweli
 
Back
Top Bottom