Hofu ya kuongezewa mke mwenza, wepesi wa kutoa talaka na kuachana bila kugawana mali inachangia wanawake waislam kuwa na adabu kuzidi wakristo?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,081
Nimejaribu kutafakari hili jambo ila nimeona nikilileta humu naweza kupata michango ya ziada yenye afya,

Kwa maoni yangu nimeona ipo hivi, ningependa nisahishwe nilipokosea, kuongezewa nilipopunguza, n.k.

Kuoa mke moja vs ruhusa ya kuongeza -

kwetu wakristo unakuta mwanamke ukimuoa kiburi kinaanza kwasababu anajua nafasi ya mke ni ya peke yake huwezi kuongeza mke kihalali, anaanza kujiona wote mpo sawa.

Kwa waisalm mwanaume karuhusiwa kuongeza wake hadi wanne, nadhani hapa mke huwa ana hofu kwamba akiwa na kiburi ama mvivu anaongezewa mwenzake mke mwenza.

Utaratibu wa Talaka

Kwetu wakristo process ya talaka ni ndefu sana hadi muanze kwenda makanisani na hadi mahakamani, mambo ya ushauri huko kanisani yanakuwa mengi sana, yani hadi mje kupata kibali cha kuachana inaweza kuchukua mda mrefu.

Kwa waislam process ni rahisi ya kutoa talaka na pia wana chombo chao maalum cha Bakwata ambacho bado kinasimamia sheria za kiislam kwenye talaka, kuna aina kadhaa za talaka kulingana na uzito wa tatizo lililopo kwenye ndoa, Hapa mwanamke anaweza kupunguza kiburi maana anajua talaka katika ndoa yake ni peni na karatasi inatosha mda huo huo.

Kugawana Mali baada ya kuachana.

Kwakuwa uvunjaji wa ndoa za kikristo unasimamiwa kwa kiasi kikubwa na mahakama, mali huwa zinapigwa pasu kwa pasu, hii huwa inafanya wanawake wengi wa kikristo kupata pesa kirahisi na hata kuwapa tamaa ya kuomba muachane ili waondoke na mali.

Kwa ndoa za kiislamu mwanaume anaweza kuamua tu kumpa mkewe talaka ama kwenda Bakwata ambako sheria za dini yao zitafatwa na mwanaume atatoa chochote anachoweza. hii inampunguzia tamaa mwanamke kumuacha mme wake. huwa wapo wanaoenda mahakamani lakini hii haijazoeleka sana kwa waislam, kwao kwenda mahakamani ni kama kwenda kinyume na sheria zao za talaka.
 
Ukishaanza kusoma na kuuelewa uislamu kila kitu kinakuwa rahisi ... Uislamu ndo dini pekee ya Mwenyezi MUNGU hivyo mafundisho yake ni bora kwa ulimwengu wote.
Kila kitu kimewekwa bayana ... Hakuna sheria zilizotungwa na watu zikaingizwa kwenye dini ndiyo maana kila kitu kina enda na Logic na ku make sense kwa sababu ni kutoka kwa muumba wetu. Alhamdulilah for Islam.
 
sababu Ndoa ni Utapeli na washajua hilo
Ni kweli mkuu, kwa ndoa za kikristo zimekuwa ngumu sana, hata huko ulaya na marekani kwenye wakristo wengi malalamiko hayaishi ila ukienda uarabuni huko wala husikii hizo kelele.
 
Wakristu hata mwende mahakamani Ila kifo ndo kiwatenganishe, na hata mkitenganishwa na mahakamani akifariki mmoja utasikia tumtafuteni mke au mme wake wa ndoa aje kumzika mwenzie.
 
Back
Top Bottom