Hizi simu zinawakera kama zinavyonikera mimi?

Bumpkin Billionare

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
1,332
621
Mara kadhaa nimekuwa nikipigiwa simu na namba 0901901901 ambayo ni automated call. Unapopokea simu hii unapatiwa maelezo ambayo huna haja wala shida nayo jambo ambalo kwangu mimi huwa naliona usumbufu tu. Cha kushukuru angalau kidogo namba hii ni tofauti na namba zingine za simu kwa hiyo sasa naweza kui-ignore.

Leo mchana huu nikiwa maeneo ya Ruvu Darajani nikiwa naendesha gari nimepigiwa simu na namba +255684000165, kwa kuwa nilikuwa kwenye barabara inayopitiwa na magari yanayoenda kasi niliamua kupaki gari pembeni niweze ku-attend hiyo call; KICHEFUCHEFU KITUPU!

"Hallow, mimi ni 'SIJUI KITUKO GANI MWAITEGE' nafurahi kwa kuwa najua wewe ni mpenzi wa nyimbo zangu. Ili kupata nyimbo zangu......" mpk hapa niliamua kukata kwani nilishasikia hasira.

Swali langu: Hivi kusajiliwa simu zetu na TCRA nia ilikuwa ni kutusupply haya makero au ni nini?

Imagine ndio umerudi job jioni umepumzika zako huku simu iko kwenye chaji, mtu anakunyanyua kwenda kuifuata kwa ajili ya tangazo lake la kipuuzi, huyu mama mimi nimemwambia nataka matege?

Kama ni biashara jamani, si ziwekwe kwenye mabango mwenye kutaka na ajisomee tusiotaka tupite kama hatujaziona. Huu ni usumbufu kwa kweli, unless kwa watu ambao kazi zao haziwachoshi mwili na akili. Mimi binafsi haya matangazo ya lazima YANANIKERA KUPITA KIASI.

Wengine ni TIGO. Hii mimesej mnayotujazia kwenye inbox zetu ni lazima au ni sehemu ya mikataba ya huduma? Oooh ukitaka raha tuma neno utamu kwenda 56601 huu sio upumbavu jamani?!!! Siku moja unatumiwa huu ****** mara 3 mpk 5, ni nini lakini?
 
Kwa kweli mie nilishafikiria kupeleka kampuni mahakamani kwa 'udhalilishaji'! Yaani ingebidi tujaze fomu na kuchagua kama tunataka matangazo na promotional stuff!
Wakati mwingine unakuwa mkutanoni, unajifaragua kutoka na kitochi chako unakuta ***** unarudi pozi limeisha! Inakera kwa kweli!
 
Mkuu uko kama mimi hawa wenye hii tabia ni tigo hasa hiyo namba ya kwanza hii ya pili ni air tell wanakera sana, yaani unapokea kwa heshima afu unakutana upumbavu kama huu, naomba TCRA wametunukuu namba zetu ili wawe wanatusumbua this is foolish enough. Miezi naomba waache hii tabia wanatukera.
 
Hata mimi Tigo wananichosha kabisa. Kutwa nzima ni meseji au simu kutoka kwenye automated system. This is chaos. TCRA wanajaza tu matumbo yao hakuna control yoyote wanayo-exercise hapa. They are simply foolish.
 
Dah, hakuna kitu inanikera kama hii. Mtu unapigiwa simu na unalazimika kuwaomba radhi ulio nao kwa wakati huo ili upokee simu halafu unakutana na huu ushenzi.. so annoying!!
 
Mimi hiyo ya Tigo mwanzoni nilidhani nimepata shavu la kazi napokea nakutana na sauti ya kike na kiume nilipatwa na hasira ile mbaya
 
kwa kweli wanasumbua la muhimu tusiishie kulalama naomba wanasheria watujuze jinsi tunavyaweza kuwaburuza mahakamani hawa mapimbi
 
JAMANI KWELI INAKERA SANA, SIE WENGINE HUKU NANJILINJI HAKUNA UMEME, TUNACHAJI KWA MWL MKUU WA S/M NANJILINJI, KUCHAJI SIMU SH. 500, SIMU ZENYEWE HAZIJAI CHAJI VIZURI, NIKIRUDI NYUMBANI NAPOKEA MSG ZAIDI YA 5 AMBAZO ZOOOTE SINA UMUHIMU NAZO, NAPATA CALLS ZA AKINA MWAITEGE, MWAIPAJA, n.k NAZO SIONI UMUHIMU WAKE, UKIZINGATIA HAO WATU HATA SIWAJUI ... NAOMBA TUSIMALIZIANE CHAJI...MNATUONGEZEA MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA.
 
MImi nachojiuliza, hivi katika huduma zao hakuna customer consent? Hatuna hiyari kweli ya kukataa mimeseji ya matege na maipaja mpk mtu ukerwe namna hii? Mimi napaki gari kusikiliza mambo ambayo siyahitaji. Naamini nchi nyingine ambazo watu wanathamini muda na privacy mtu anaweza kukufungulia mashtaka
 
Jamani hapa kwetu Tabata Chang'ombe ni siku ya nne(4) TiGO haipo hewani yaani full usumbufu, TCRA Inakuaje tunakosa huduma kwa siku nne mfululizo? Na kibaya zaidi ndo mawasiliano pekee ambayo yanayokuunganisha na wateja wako, ni ugomvi umetawala wateja wanaingia gharama hadi unapoishi na kukushangaa kisa cha kuwazimia simu ama mawasiliano hadi wapata gharama zingine ambazo unapaswa kuwarefund,

Hii ni Kero Idara husika zitusikie hii ni kero kwa wateja wa TiGO tunaoishi Tabata chang'ombe, kama mnara umeishiwa Mafuta kwanini wasiwe wawazi kwa hili? Kweli tunaudhika pamoja na minamba ya ajabu mnayotupigia simu, meseji nyingi za kutustua yasiyo na mantiki yeyote mnatuchosha. Uzeni minara kama gharama za uendeshaji zinawashinda!
 
Nina ombi moja tu! naomba muongozo wa kisheria dhidi ya madhalimu hawa ,maana nimechoshwa na niko tayari kuchukua hatua!
 
Mara kadhaa nimekuwa nikipigiwa simu na namba 0901901901 ambayo ni automated call. Unapopokea simu hii unapatiwa maelezo ambayo huna haja wala shida nayo jambo ambalo kwangu mimi huwa naliona usumbufu tu. Cha kushukuru angalau kidogo namba hii ni tofauti na namba zingine za simu kwa hiyo sasa naweza kui-ignore.

Leo mchana huu nikiwa maeneo ya Ruvu Darajani nikiwa naendesha gari nimepigiwa simu na namba +255684000165, kwa kuwa nilikuwa kwenye barabara inayopitiwa na magari yanayoenda kasi niliamua kupaki gari pembeni niweze ku-attend hiyo call; KICHEFUCHEFU KITUPU!

"Hallow, mimi ni 'SIJUI KITUKO GANI MWAITEGE' nafurahi kwa kuwa najua wewe ni mpenzi wa nyimbo zangu. Ili kupata nyimbo zangu......" mpk hapa niliamua kukata kwani nilishasikia hasira.

Swali langu: Hivi kusajiliwa simu zetu na TCRA nia ilikuwa ni kutusupply haya makero au ni nini?

Imagine ndio umerudi job jioni umepumzika zako huku simu iko kwenye chaji, mtu anakunyanyua kwenda kuifuata kwa ajili ya tangazo lake la kipuuzi, huyu mama mimi nimemwambia nataka matege?

Kama ni biashara jamani, si ziwekwe kwenye mabango mwenye kutaka na ajisomee tusiotaka tupite kama hatujaziona. Huu ni usumbufu kwa kweli, unless kwa watu ambao kazi zao haziwachoshi mwili na akili. Mimi binafsi haya matangazo ya lazima YANANIKERA KUPITA KIASI.

Wengine ni TIGO. Hii mimesej mnayotujazia kwenye inbox zetu ni lazima au ni sehemu ya mikataba ya huduma? Oooh ukitaka raha tuma neno utamu kwenda 56601 huu sio upumbavu jamani?!!! Siku moja unatumiwa huu ****** mara 3 mpk 5, ni nini lakini?

nahisi nakereka kuliko wewe maana mimeseji yao inatibua ulcer zangu!
 
Back
Top Bottom