Hizi ni sehemu ya sababu za CCM kuendelea kukataliwa na Watanzania

Mkenazi

Senior Member
Apr 11, 2011
124
43
Sioni jambo jipya linaloweza kufanikishwa na CCM ikiwa mambo waliyopanga wenyewe yamewashida kama nilivyoweza kukumbuka machache hapa chini:

  1. Chama cha Mapinduzi kilishindwa kutekeleza programu yake ya miaka 15 (1987 2002). Pamoja na mambo mengine kulikuwa na kipengele kinasema "IFIKAPO 2002 kila wilaya itakuwa na matrekta 25" Mpaka leo hakuna kitu kama hicho badala yake miaka 24 baadae bado mnaongelea kununua Power tiller tena kwa UFISADI
  2. Chama cha mapinduzi kilianzisha mradi wake wa SUKITA pale bonde la Tabata kikashindwa, SUWATA kikashindwa ; leo CCM wanazunguka wanatuimbia wimbo wa EL, RA na AC yaani wanatafuta huruma za wananchi wa Tanzania kupitia mazao ya mfumo wao. Tumekwisha wagundua.
  3. Nchi nzuri Tanzania kwa sababu ya utawala wa CCM haina hata shirika la ndege lenye ndege za uhakika. Tunazidiwa na Rwanda. Hawa wawekezaji waliojaa nchini wangekuwa wanapanda ndege zetu shirika lingekuwa kubwa sana.
  4. UMEME – Eti mpaka leo hatuna umeme wa kutoshereza mjini. Mawazo ya CCM ni kukodisha tu hii ni milango ya UFISADI. Iko wapi mipango ya MCHCHUMA, KIWIRA na LIGANGA coal projects ? toka miaka hiyo mpo tu halafu mnasema mnataka ridhaa ya wanachi muendelee kuwatesa.
  5. VIWANDA, enzi hizo za Mwalimu Tanga, Morogoro, Dar Arusha n.k kulijaa viwanda vya kila namna na kutoa ajira leo viko wapi ? bado mnataka muendelee kutawala – Nasema imeishatosha pumzikeni muone wenye akili watakavyofanya kazi.
  6. CCM ni nini hasa ilichokianzisha kikafika mwisho kwa mafanikio ? Ilianzisha RUBADA – Rufiji Basin Development Authority miaka ya 1975 – Hilo bonde limeendelezwa ? ikaja KOTACO – Korea Tanzania Agricultural Company kwenye mabonde ya chitah je mlifanikiwa ?, haya kuna kilmo cha kufa na kupona miaka ya 1974, kilimo ni uti wa mgongo, Kilimo kwanza, MKUKUTA, Mkurabita n.k.
  7. Oh CCM – mmewadhoofisha wana wa Tanzania kwa kuwajengea mawazo hasi kwa kila eneo mf. Kauli ya viongozi wote wa CCM ni kusema tanzania ni masikini – hii ni mbaya sana. Nchi isiyotaka kutumia wataalamu wake Waandisi, wakandarasi n.k hii yote ni sababu ya UFISADI. – CCM inachojua ni kuchakachua tu hata taarifa za utafiti inachakachua ili ionekane imefanya vizuri.
  8. ELIMU – Shule za Yebo yebo – hakuna maabara halafu mnasisitiza masomo ya sayansi au kwa kuwa viongozi wengi na watoto wenu mnasomea siasa ?. Hakuna mkakati wa Kitaifa wa kuifanya sayansi ijenge uchumi wa nchi. Ikiwa mhandisi wa kitanzania ndiye supervisor kwenye makampuni ya wakoloni tutegemee nini ? - UFISADI kila sehemu.
  9. CCM, CCM, CCM pamoja na wabunge wako kitendo cha kuipenda ccm ya watu milioni tano kuliko watu milioni 40 wasiokuwa CCM na ambao ni wapiga kura wenu mnatenda kosa kubwa sana na ndio maana hamtapewa ridhaa tena ya kuongoza nchi hii. Wabunge wa CCM wanashangilia kil akitu hata kama ndani yake kina ajenda ya kuwachinja ndugu zao. Wabunge wa CCM walishangilia mswada wa uundaji wa tume ya Katiba mpya ulioondolewa bungeni, lakini pia wangeupitisaha serikali ingelazimisha uende bungeni. Huu ni wendawazimu ambao ni magamba kuliko hata haya y aya juzi kwani matokeo ya katiba dhaifu ni ufisadi uliokithiri.
  10. CCM kimekuwa ni chama cha kijeshi kama ifutavyo
  • Rais – ni mwnajeshi
  • Wakuu wa mikoa wengi wanajeshi wasitaafu
  • Wakuu wa wilaya – Wanajeshi
  • Makamba, Kapteni Mkuchika, Nape mtoto wa mwanajeshi, January Makamba – baba yake mwanajeshi, Kinana
  1. SHIME Watanzania tunayo kazi moja tu nayo ni kumwondoa nduli CCM kwani NIA tunayo, Sababu tunazo na uwezo tunao.
Naomba kuwasilisha na nyie muongeze sababu za kwa nini CCM haiwezi kuendelea kutawala zaidi.
 
Na baba yako aliyesomeshwa kwa jitihada za CCM akafanya hadi leo na wewe unajua ku CLICK mboja hujaiandika kama shortcoming hapo?
 
Na baba yako aliyesomeshwa kwa jitihada za CCM akafanya hadi leo na wewe unajua ku CLICK mboja hujaiandika kama shortcoming hapo?
Ni lini uliona CCM wanasomesha watu? Lini umeona CCM wametangaza scholarships? Acha kudanganya watu kuhusu elimu. Utoaji wa elimu ni moja ya majukumu ya lazima yanayopaswa kutekelezwa na serikali yoyote ile, iwe ya kifalme, kidikteta, au ya ki-CCM. Na kwa kuzingatia hili ndo maana unaona kila mahali duniani serikali zote zinasomesha watu wake pasipokuwauliza itikadi zao wala dini zao. Ulimbukeni wenu huu ndo maana umepelekea kuchukulia suala la elimu kama moja ya mambo ya kutilia msisitizo kwenye ilani ya CCM. Masuala ya maji, chakula, elimu. afya, na ulinzi siyo priorities but they are the must. Utaona serikali yenu ya CCM inasema eti mkituchagua tutawaletea huduma ya maji, afya na elimu, huu ni ujuha kwani CCM imekuwa madarakani kwa kipindi kirefu na haijayatekeleza mambo yote ya lazima huku ikiendelea kukusanya kodi za wananchi hao bila kuwapelekea huduma muhimu. Unafikiri mfumo wa kutoza kodi ulianzishwa kwa misingi ipi? Lengo la kodi ni kuiwezesha serikali kutoa huduma za pamoja ambazo mtu mmoja mmoja hawezi kuwa nazo kwa jitihada zake binafsi. Na kwa kuzingatia kuwa serikali huwa inatoza kodi kwa watu wote iwe washabiki wa CHADEMA, CUF, NCCR- Mageuzi nk, vivyo hivyo inapaswa kutoa huduma za msingi kwa watu wote. Acha mtizamo wa kijima kwani wanaodanganywa kwa sera kama yako ni wale ambao hawakufika darasani sawasawa.
 
<p>
Na baba yako aliyesomeshwa kwa jitihada za CCM akafanya hadi leo na wewe unajua ku CLICK mboja hujaiandika kama shortcoming hapo?
</p>
<p>&nbsp;</p>
mkubwa swala la elimu na huduma nygine ni haki kwa kila raia wa Tanzania na wala si hisani hatakidogo sasa kupewa haki yetu ya elimu hatulazimiki kumshukuru mtu yeyote,katafute vilaza wenzenu wenye Magamba
 
Sioni jambo jipya linaloweza kufanikishwa na CCM ikiwa mambo waliyopanga wenyewe yamewashida kama nilivyoweza kukumbuka machache hapa chini:

  1. Chama cha Mapinduzi kilishindwa kutekeleza programu yake ya miaka 15 (1987 2002). Pamoja na mambo mengine kulikuwa na kipengele kinasema "IFIKAPO 2002 kila wilaya itakuwa na matrekta 25" Mpaka leo hakuna kitu kama hicho badala yake miaka 24 baadae bado mnaongelea kununua Power tiller tena kwa UFISADI
  2. Chama cha mapinduzi kilianzisha mradi wake wa SUKITA pale bonde la Tabata kikashindwa, SUWATA kikashindwa ; leo CCM wanazunguka wanatuimbia wimbo wa EL, RA na AC yaani wanatafuta huruma za wananchi wa Tanzania kupitia mazao ya mfumo wao. Tumekwisha wagundua.
  3. Nchi nzuri Tanzania kwa sababu ya utawala wa CCM haina hata shirika la ndege lenye ndege za uhakika. Tunazidiwa na Rwanda. Hawa wawekezaji waliojaa nchini wangekuwa wanapanda ndege zetu shirika lingekuwa kubwa sana.
  4. UMEME &#8211; Eti mpaka leo hatuna umeme wa kutoshereza mjini. Mawazo ya CCM ni kukodisha tu hii ni milango ya UFISADI. Iko wapi mipango ya MCHCHUMA, KIWIRA na LIGANGA coal projects ? toka miaka hiyo mpo tu halafu mnasema mnataka ridhaa ya wanachi muendelee kuwatesa.
  5. VIWANDA, enzi hizo za Mwalimu Tanga, Morogoro, Dar Arusha n.k kulijaa viwanda vya kila namna na kutoa ajira leo viko wapi ? bado mnataka muendelee kutawala &#8211; Nasema imeishatosha pumzikeni muone wenye akili watakavyofanya kazi.
  6. CCM ni nini hasa ilichokianzisha kikafika mwisho kwa mafanikio ? Ilianzisha RUBADA &#8211; Rufiji Basin Development Authority miaka ya 1975 &#8211; Hilo bonde limeendelezwa ? ikaja KOTACO &#8211; Korea Tanzania Agricultural Company kwenye mabonde ya chitah je mlifanikiwa ?, haya kuna kilmo cha kufa na kupona miaka ya 1974, kilimo ni uti wa mgongo, Kilimo kwanza, MKUKUTA, Mkurabita n.k.
  7. Oh CCM &#8211; mmewadhoofisha wana wa Tanzania kwa kuwajengea mawazo hasi kwa kila eneo mf. Kauli ya viongozi wote wa CCM ni kusema tanzania ni masikini &#8211; hii ni mbaya sana. Nchi isiyotaka kutumia wataalamu wake Waandisi, wakandarasi n.k hii yote ni sababu ya UFISADI. &#8211; CCM inachojua ni kuchakachua tu hata taarifa za utafiti inachakachua ili ionekane imefanya vizuri.
  8. ELIMU &#8211; Shule za Yebo yebo &#8211; hakuna maabara halafu mnasisitiza masomo ya sayansi au kwa kuwa viongozi wengi na watoto wenu mnasomea siasa ?. Hakuna mkakati wa Kitaifa wa kuifanya sayansi ijenge uchumi wa nchi. Ikiwa mhandisi wa kitanzania ndiye supervisor kwenye makampuni ya wakoloni tutegemee nini ? - UFISADI kila sehemu.
  9. CCM, CCM, CCM pamoja na wabunge wako kitendo cha kuipenda ccm ya watu milioni tano kuliko watu milioni 40 wasiokuwa CCM na ambao ni wapiga kura wenu mnatenda kosa kubwa sana na ndio maana hamtapewa ridhaa tena ya kuongoza nchi hii. Wabunge wa CCM wanashangilia kil akitu hata kama ndani yake kina ajenda ya kuwachinja ndugu zao. Wabunge wa CCM walishangilia mswada wa uundaji wa tume ya Katiba mpya ulioondolewa bungeni, lakini pia wangeupitisaha serikali ingelazimisha uende bungeni. Huu ni wendawazimu ambao ni magamba kuliko hata haya y aya juzi kwani matokeo ya katiba dhaifu ni ufisadi uliokithiri.
  10. CCM kimekuwa ni chama cha kijeshi kama ifutavyo
  • Rais &#8211; ni mwnajeshi
  • Wakuu wa mikoa wengi wanajeshi wasitaafu
  • Wakuu wa wilaya &#8211; Wanajeshi
  • Makamba, Kapteni Mkuchika, Nape mtoto wa mwanajeshi, January Makamba &#8211; baba yake mwanajeshi, Kinana
  1. SHIME Watanzania tunayo kazi moja tu nayo ni kumwondoa nduli CCM kwani NIA tunayo, Sababu tunazo na uwezo tunao.
Naomba kuwasilisha na nyie muongeze sababu za kwa nini CCM haiwezi kuendelea kutawala zaidi.
Zinaweza zikawa sababu zinazowafanya wakataliwe na wananchi lakini at the same time ndiyo sababu zinazowafanya waendelee kuwa watawala.
 
sioni jambo jipya linaloweza kufanikishwa na ccm ikiwa mambo waliyopanga wenyewe yamewashida kama nilivyoweza kukumbuka machache hapa chini:

  1. chama cha mapinduzi kilishindwa kutekeleza programu yake ya miaka 15 (1987 2002). Pamoja na mambo mengine kulikuwa na kipengele kinasema "ifikapo 2002 kila wilaya itakuwa na matrekta 25" mpaka leo hakuna kitu kama hicho badala yake miaka 24 baadae bado mnaongelea kununua power tiller tena kwa ufisadi
  2. chama cha mapinduzi kilianzisha mradi wake wa sukita pale bonde la tabata kikashindwa, suwata kikashindwa ; leo ccm wanazunguka wanatuimbia wimbo wa el, ra na ac yaani wanatafuta huruma za wananchi wa tanzania kupitia mazao ya mfumo wao. Tumekwisha wagundua.
  3. nchi nzuri tanzania kwa sababu ya utawala wa ccm haina hata shirika la ndege lenye ndege za uhakika. Tunazidiwa na rwanda. Hawa wawekezaji waliojaa nchini wangekuwa wanapanda ndege zetu shirika lingekuwa kubwa sana.
  4. umeme &#8211; eti mpaka leo hatuna umeme wa kutoshereza mjini. Mawazo ya ccm ni kukodisha tu hii ni milango ya ufisadi. Iko wapi mipango ya mchchuma, kiwira na liganga coal projects ? Toka miaka hiyo mpo tu halafu mnasema mnataka ridhaa ya wanachi muendelee kuwatesa.
  5. viwanda, enzi hizo za mwalimu tanga, morogoro, dar arusha n.k kulijaa viwanda vya kila namna na kutoa ajira leo viko wapi ? Bado mnataka muendelee kutawala &#8211; nasema imeishatosha pumzikeni muone wenye akili watakavyofanya kazi.
  6. ccm ni nini hasa ilichokianzisha kikafika mwisho kwa mafanikio ? Ilianzisha rubada &#8211; rufiji basin development authority miaka ya 1975 &#8211; hilo bonde limeendelezwa ? Ikaja kotaco &#8211; korea tanzania agricultural company kwenye mabonde ya chitah je mlifanikiwa ?, haya kuna kilmo cha kufa na kupona miaka ya 1974, kilimo ni uti wa mgongo, kilimo kwanza, mkukuta, mkurabita n.k.
  7. oh ccm &#8211; mmewadhoofisha wana wa tanzania kwa kuwajengea mawazo hasi kwa kila eneo mf. Kauli ya viongozi wote wa ccm ni kusema tanzania ni masikini &#8211; hii ni mbaya sana. Nchi isiyotaka kutumia wataalamu wake waandisi, wakandarasi n.k hii yote ni sababu ya ufisadi. &#8211; ccm inachojua ni kuchakachua tu hata taarifa za utafiti inachakachua ili ionekane imefanya vizuri.
  8. elimu &#8211; shule za yebo yebo &#8211; hakuna maabara halafu mnasisitiza masomo ya sayansi au kwa kuwa viongozi wengi na watoto wenu mnasomea siasa ?. Hakuna mkakati wa kitaifa wa kuifanya sayansi ijenge uchumi wa nchi. Ikiwa mhandisi wa kitanzania ndiye supervisor kwenye makampuni ya wakoloni tutegemee nini ? - ufisadi kila sehemu.
  9. ccm, ccm, ccm pamoja na wabunge wako kitendo cha kuipenda ccm ya watu milioni tano kuliko watu milioni 40 wasiokuwa ccm na ambao ni wapiga kura wenu mnatenda kosa kubwa sana na ndio maana hamtapewa ridhaa tena ya kuongoza nchi hii. Wabunge wa ccm wanashangilia kil akitu hata kama ndani yake kina ajenda ya kuwachinja ndugu zao. Wabunge wa ccm walishangilia mswada wa uundaji wa tume ya katiba mpya ulioondolewa bungeni, lakini pia wangeupitisaha serikali ingelazimisha uende bungeni. Huu ni wendawazimu ambao ni magamba kuliko hata haya y aya juzi kwani matokeo ya katiba dhaifu ni ufisadi uliokithiri.
  10. ccm kimekuwa ni chama cha kijeshi kama ifutavyo
  • rais &#8211; ni mwnajeshi
  • wakuu wa mikoa wengi wanajeshi wasitaafu
  • wakuu wa wilaya &#8211; wanajeshi
  • makamba, kapteni mkuchika, nape mtoto wa mwanajeshi, january makamba &#8211; baba yake mwanajeshi, kinana
  1. shime watanzania tunayo kazi moja tu nayo ni kumwondoa nduli ccm kwani nia tunayo, sababu tunazo na uwezo tunao.
naomba kuwasilisha na nyie muongeze sababu za kwa nini ccm haiwezi kuendelea kutawala zaidi.

nakubaliana na hoja 100%. Shime tuungane pamoja kwani ukombizi wa mtanzania uko mikononi mwetu sote.
 
Ili tupate chama safi kabisa kuongoza Tanzania Chadema iondoe picha hii kwanza TEC na Kanisa Katoliki kwa Ujumla wasijifanye washauri wa karibu wa Chadema na Kadinal Pengo asipende kudandia hoja za Chadema na Kutoa matamko! Pili Wachaga waiachie Chadema sasa kiondokane na sura ya ukabila yani kiondokane na Uchaga na kila mwana chama wake awe na haki sawa na heshima yake isitokane na Uchaga wake,tatu kama kuna deni analo dai Mzee Edwini Mtei kwa Kuanzisha Chadema alipwe ili chama kitoke kwenye Ukampuni Binafsi au Chama cha Ukoo na sasa kiwe Chama chenye sura ya Kitaifa! Na Mwisho Freeman Mbowe awape nafasi wanachama wengine washike nafasi ya kiti cha Mwenyekiti wa Taifa!
 
Na baba yako aliyesomeshwa kwa jitihada za CCM akafanya hadi leo na wewe unajua ku CLICK mboja hujaiandika kama shortcoming hapo?

inaonesha ni namna gani ulivokuwa mbumbumbu maana elimu, maji umeme na barabara ni vitu vya msingi yaani hata mtoto wa darasa la 4 anakushinda wewe zuzu kweli na nakuonea huruma wewe na familia yako
 
inaonesha ni namna gani ulivokuwa mbumbumbu maana elimu, maji umeme na barabara ni vitu vya msingi yaani hata mtoto wa darasa la 4 anakushinda wewe zuzu kweli na nakuonea huruma wewe na familia yako

Toa jibu sahihi acha longolongo! Baba yako hajasomeshwa na CCM?
 
Na baba yako aliyesomeshwa kwa jitihada za CCM akafanya hadi leo na wewe unajua ku CLICK mboja hujaiandika kama shortcoming hapo?

Duh yaani mpaka leo hii kuna watu wana mawazo ya siasa za 1995 (CCM imekusomesha, CCM imewasomesha) hii mbona iliisha julikana kuwa ni propaganda isiyoweza kushawishi hata mgonjwa wa akili?. CCM isomeshe watu ina hela za kutoka wapi?, watanzania wote wanaosoma either kwa mikopo au kipindi kile bure, ilikuwa ni pesa zao hizo, baba zao na mama zao wanalipa kodi za mazao yao kila siku. Na viwanja vya michezo CCM walivyojimilisha wajue kuwa whether wanaviuza au kuendelea kuviita uwanja wa micheza CCM.... navyo vitarudi kwa wananchi pindi wakichukua serikali yao.
 
Toa jibu sahihi acha longolongo! Baba yako hajasomeshwa na CCM?
Hii hoja jamaa umeing'ang'ania bure haina mashiko kwenye siasa. Baba yangu mimi hakusomeshwa na CCM, alisoma enzi za ukoloni ambapo CCM haikuwa inafikirika kama itakuja kutokea Tanganyika. Kama una akili japo ya kukuwezesha kujielewa mwenyewe nafikiri unaweza kunielewa hata mimi ninayetumia maneno rahisi kabisa. Kwa kuwa CCM haikuwepo enzi za ukoloni lakini watu walisomeshwa na hao wakoloni, huoni kuwa kazi ya kusomesha siyo sera ya CCM bali ni wajibu wa serikali yoyote inayokusanya kodi za wananchi? Kama jibu lako ni ndiyo, basi elewa kuwa watu husma kupitia kodi zao na siyo CCM. Serikali yoyote itakayoingia madarakani ni lazima isomeshe, siyo suala la mjadala wala propaganda za ki-magamba magamba hapa.
 
Tafuta gazeti la mwanahalisi wiki hii tar 20 april to 25 utaona Kikwete anavyo nuka ufisadi. Mambo yote yameanikwa hadharani na mafisadi yote list ya kwanza ili iliyo tolewa mwaka 2007 tar 15 september ipo na majina mapya yapo akiwemo Msekwa na magufuli.
 
Hata cdm ikishinda bado itakusanya kodi watu wasome tofauti iko wapi Kati ya CCM chadema na ukoloni. Tatizo la chadema ni uchaga na sera ya majimbo. Kwa mtaji wenu huo hamtakanyaga Magogoni, mtakuwa mnapaona kupitia linings .
 
Back
Top Bottom