Hizi ni hasira au? Watu wasio na ajira wajilipua kwa petroli huko Moroco

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Hii nayo ni kali kuliko, kweli dunia haishi vituko. Ukistaajabu ya TZ Utayaona ya Moroco. Wahitimu wasio na ajira wameanza kujilipua kwa petroli huko Moroco kwa sababu ya kukosa ajira. Wananafanya hivyo kuonyesha hasira kwa serikali yao. Hii si habari ya kuchekesha japo unaweza kucheka. Tusubiri Bongo tu sasa.. Nimeiona TBC taarifa ya habari.
 
Waarabu kweli hawanazo, wanahitaji ushauri nasaha. Wawili kati yao hali zao ni mbaya na wapo ICU!
 
Mwana mapinduzi hafaidi mapinduzi bali watafaidi wengine wanajitoa kwawjili ya wenzao
 
Kama huna chakuchangia kaa kimya..usinitie hasira watu hapa
We umechangia nini cha maana? Kama una hasira pasuka, we vipi wewe! Kwa hy unaunga hoja mkono watu kujilipua?KWA HASARA YA NANI? Badala ya kumlipua anayekukosesha ajira unajilipua wewe hlf ukifa ndo umesaidia nini?
 
Mwana mapinduzi hafaidi mapinduzi bali watafaidi wengine wanajitoa kwawjili ya wenzao

Hakika usemayo. Kujitoa muhanga kwa staili hii! Yaani mpaka sasa mwili unasisimka. Hawa kweli ndio wanamapinduzi wa kweli. Tukiwaita hamnazo tunakosea.
 
We umechangia nini cha maana? Kama una hasira pasuka, we vipi wewe! Kwa hy unaunga hoja mkono watu kujilipua?KWA HASARA YA NANI? Badala ya kumlipua anayekukosesha ajira unajilipua wewe hlf ukifa ndo umesaidia nini?

Hata mimi namshangaa huyu anayekucharukia! Eti usimtie hasira, basi ajilipue basi kama anaona ni vizuri!
 
inaonekana wamekaa sana kitaa bila ajira.hizi serikali za afrika usizitegemee kuwa zitakupa ajira,fanya mchakato wa kujiajiri
 
wakishajilipua ndo watapata ajira au?

kaka siku utakapokosa ajira ndiyo utajua maana ya kauli yako.
Swala la kujiua huja baada ya njia zote kushindikana na huwatokea watu wengi na si kwa ajira tu.
Kukosa ajira kwa msomi ni hali ngumu sana japo kuna njia za kujiajiri lakini jiulize serekali zetu zimewaandaa wasomi wake kujiajiri na je miundombinu ipo friendly kwa wasomi hawa wachanga wasio na mitaji wala mali za kuweka zamana za mikopo.
 
we umechangia nini cha maana? Kama una hasira pasuka, we vipi wewe! Kwa hy unaunga hoja mkono watu kujilipua?kwa hasara ya nani? Badala ya kumlipua anayekukosesha ajira unajilipua wewe hlf ukifa ndo umesaidia nini?

wewe hujui impact ya watu hawa kujiua?
Unajua mabadiliko yaliyotokea tunisia, misri, libya na sasa syria yametokea baada ya mtu mmoja wa tunisia kujiua?
Watu wengi wamepoteza maisha kwa ajili ya wengine hata wewe upo humu jf uliza watu wangapi wakepoteza maisha yao mpaka sasa wewe upo huru
mimi naunga mkono watu kujilipua hii itaamsha hizi serekali zetu zilizo usingizini
 
Ata Bongo mbona watu wanajiua kwa ugumu wa maisha sema kwa hapa kwetu wengi wao ni ambao hawajaenda shule.....but bliv or not ata BONGO itatokea tu coz haya matunda kidogo tunayoyapata kuna watu nyuma yake waliojitoa muhanga kwa namna moja au nyingine....mtu kasota shule miaka yote hiyo then akose ajira AKAIBE ndo umsifie kua anaakili? Msomi aliejitoa muhanga TUNISIA mchango wake siumeoneka kwa inchi nyingi za kiarabu zilizokua na madikteta? imagine apa kwetu watu kama watatu wajitoe muhanga kwa dizaini hiyp kupinga mapato KIDUCHU ya madini yetu na UFISADI weunafikiri hakitaeleweka? we unapinga tukuombee maisha marefu ili uje ushuhudie apa kwetu mbona NIGERIA wameanza na wao ni waarabu? kwa taarifa yako wanajeshi wengi wa MAREKANI they commit suicide themselves kuliko wanavyouliwa na TALIBANI hii inaonesha nini kama sio kupinga hizo vita au kuchoshwa na vita mpaka viongozi wao wanachanganyikiwa? Mbona YESU hakutukana lakini yaliyomkuta sinikwaajiri yetu? so husipuuze michango ya watu km huna historia by the way hivi unategemea kuishi milele ktk hii dunia yenye dhuluma?
 
Inataka moyo sana kufikia kuchukua hatua kama hii!
iran_man_fire_2.jpg
 
cr9 umesema kweli.,, anaweza kulisemea hili vyema ni yule mwenye elimu halafu anasota mtaani kwa kukosa ajira,,,,, so siwezi kuwaita hao waliojilipia hamnazo maana hata mimi ni victim wa kupata ajira. ila pia huko kujiajiri ni kugumu ile mbaya kutokana na urasimu iliopo katika nchi zetu za kiafrika. lakini zaidi vijana wengi wanashindwa kujiajiri kutoka na mfumo wa elimu yetu ambyo umejikita kwenye MEMORY test na si kitu uwezo wa kufikiri na kuvumbua vitu,,, na kwa mfumo huu wa elimu tusitegemee kuwapata akina steve jobs wa kiafrika,,,, wanafunzi wa vyuo vikuu kazi yao kubwa ni kukariri videsa na ndio maana sishangai wanapotoa advert ya kazi wanasema experience ya miaka kadhaa maana experience inamatter kuliko elimu waliyonayo wasomi wetu
 
Hii nayo ni kali kuliko, kweli dunia haishi vituko. Ukistaajabu ya TZ Utayaona ya Moroco. Wahitimu wasio na ajira wameanza kujilipua kwa petroli huko Moroco kwa sababu ya kukosa ajira. Wananafanya hivyo kuonyesha hasira kwa serikali yao. Hii si habari ya kuchekesha japo unaweza kucheka. Tusubiri Bongo tu sasa.. Nimeiona TBC taarifa ya habari.

hao si waarabu?
 
Back
Top Bottom