Hizi ndo athari za kupanda kwa bei ya umeme

Naunga mkono bei kupandishwa ili na wengjne nao wapate umeme, tulikuwa only 10% Now we need to go 30%. Sasa haiwezekani kufanya hivyo kwa ruzuku ya serikali.

Duh! Mko wengi kumbe? Hivi ni kupandisha umeme au serikali, wadaiwa wakuu wa umeme na wale wakubwa wengine kulipa madeni yao? Umeshajua Tanesco inadai watu na hawajalipa na umeme wanatumia?
 
Naunga mkono bei kupandishwa ili na wengjne nao wapate umeme, tulikuwa only 10% Now we need to go 30%. Sasa haiwezekani kufanya hivyo kwa ruzuku ya serikali.

Ukiwapa watu umeme ambao hawawezi kumudu gharama zake faida iko wapi?

Unaposema Serikali haina uwezo wa kutoa ruzuku wewe ni msemaji wa Serikali?! Acha unafiki!
 
Kidumu Chama cha mapinduzi na fikra za Ewura.
±±±±±±±
I left the label right a lot cats wonder how? Evry
tym I diss the label I get fine 100 thous just for
tellin y'all I get fined 100 thous uh them cats are ill five times half a mil.---You got luv it
 
Ukiwapa watu umeme ambao hawawezi kumudu gharama zake faida iko wapi?

Unaposema Serikali haina uwezo wa kutoa ruzuku wewe ni msemaji wa Serikali?! Acha unafiki!

Utakuwa unaishi miaka kama 20 nyuma; hela za serikali zinatokana na kodi zetu! Na zaidi zinatoka pia nje ya wale wenye umeme majumbani: Kutumia hizo hela ku-subsidize watumiaji umeme ni uhuni. Nashauri wanaoneemeka na umeme ndio wenyewe walipie huduma yao. Hapa Unafiki uko wapi?
 
Naunga mkono bei kupandishwa ili na wengjne nao wapate umeme, tulikuwa only 10% Now we need to go 30%. Sasa haiwezekani kufanya hivyo kwa ruzuku ya serikali.

Kupanda kwa bei ya umeme hakufanyi watanzania wengine wapate umeme, Umeme unapanda bei kwa faida ya Watanzania wachache sana na hii itaendelea kuumiza sana watanzania!!

Viongozi wao haiwasumbui kwa kuwa bado kuna wananchi wajinga kama wewe ambao hata wakichukuliwa wake/waume na kiongozi wa serikali bado watakwambia ni haki yake tu, vipofu!!

Nashukuru wenzangu hapo juu wamejaribu kukuelekeza lengo halisi la kupanda kwa bei ya umeme na si kweli kuwa ni ili isaidie maendeleo ya usambazaji nishati hii.

Unafahamu kwamba mtanzania Fisadi Nimrod Mkono anaidai Tanesco 18bilion!?
Uliza ilikuwajekuwaje mpaka anadai shirika kiasi kikubwa hicho cha pesa!!

Hizi ni mojawapo ya sababu kidoogo nimekumegea kwa nini umeme unapanda bei, usishabikie vitu muhimu kama vile timu za mpira!!
 
Sidhani kama ni busara kulipongeza hili, Hii ni hatari sana kwa ustawi wa maisha ya Watanzania Unapopongeza ni vema ukatafakari kwa kina kwani kuna mambo yaliyopita ambayo CCM wametuaminisha kuwa yatasaidia kupeleka umeme vijijini
1. Kikwete akiwa katika ziara zake kanda ya Ziwa alitamka kuwa Marekani (USA) imeisaidia Tanzania katika Mradi mkubwa wa umeme na ni nchi pekee Africa iliyopewa fedha nyingi katika Mradi huu wa Umeme. Kwa kauli hii kulikuwa na haja ya kuongeza gharama eti kusaidia kupeleka umeme vijijini?

2. Tunaponunua umeme kuna 3% REA ambayo tunaambiwa ni kwa ajili ya kusaidia kupeleka umeme Vijijini, Kato hili maana yake nini?

3. Nakumbuka Zanzibar walikuwa wanadaiwa na TANNESCO 50,000,000,000/= lakini cha kushangaza deni hili lilisamehewa na TANNESCO na mzigo huu ndio unatuangukia sisi kufidia.

4. TANNESCO wananunua umeme kutoka SONGAS na IPTL sisi kama wananchi hatujui wanauziwa kwa shillingi ngapi na wao wanaamua kula cha juu kutuuzia sisi, lakini cha msingi tungejiuliza hii Gesi inayozalisha umeme ule kule Songas ni ya kwetu lakini cha ajabu wageni wamemiliki mitambo hiyo kwa kutumia gesi yetu wanazalisha umeme na kutuuzia huu ni ujinga.

*** Namalizia kwa kukuambia na kaa ufahamu hivyo ongezeko hili ni kwa ajili ya kupata fedha za kuwagawia CCM kwa ajili ya matumizi ya uchaguzi 2015 kwani lile dili la line za Simu lilipogonga mwamba ndio maana wamehamia huku. Hakuna cha Umeme vijijini wala nini yote hii ni wizi na unyanyasaji kwa raia.

Mkuu - kwa kuongezea , hayo ya juu, ni kuwa uchumi wa nchi utashuka zaidi maana itakuwa nafuu kuagiza bidhaa nje kuliko kuzalisha ndani hivyo hazina kidogo iliyopo itaishia ku import bidhaa hivyo Shilingi itashuka thamani tena; hatimaye bidhaa zitakwa juu
 
Umetoa hoja nzuri sana. Lakini hiyo principle itafanya kazi pala tayari umeme, nguzo, nyaya, mita na internal wiring zimefanyika kwa waTanzania wengi, Other than that it does not apply. Nawakumbusha tu kwamba TANESCO inataka ku-kopa iendeleze generation, distribution na supply ya umeme majumbani na viwandani lakini wakopaji wanasema hawezi kopesha shirika ambalo haliwezi kujenereti its own money, linategemea hisani
ya waziri wa fedha. Hivyo kupanda huku kwa tarifu kutalitoa kampuni kwenye matatizo,

Kwa nini tanesco hawawwzi kujerate their own money?
 
Wengine tunaongozwa na ku-think Big na critically; TANESCO lazima tuipe uwezo iweze kukopesheka ili tuitoe kwenye mzigo wa kubebwa na serikali... na tunaweza tu kufanya hivyo kwa kuipa momentum. Ambayo ni kulipia huduma zake ili serikali ikate kupeleka ruzuku ambayo inachezewa, then tuibane TANESCO kwa huduma ambayo ni fully paid without subsidy!!!!

Kuongeza gharama za kutoa huduma kamwe hakutaifanya TANESCO kuboresha huduma zake. Shirika chili linaendeshwa kwa gharama kubwa sana isivyostahili. Cost za mikataba yake ya "ki-Karl Peter" (IPTL, SONGAS, NK) ni kubwa mno, shirika liko overstuffed...matokeo yake operational cost ziko juu kulingana na mapato.

Ili TANESCO isonge mbele yanahitajika mabadiliko makubwa kimfumo, utendaji na ufanisi. Kamwe na haijawai tokea duniani kwa kampuni kuendelea kwa ku-finance operational cost period. Ni mara ngapi TANESCO wameongeza bei hivi karibuni? Je imeleta matokeo gani katika kuboresha huduma na upatikanaji wake?

Kwa mfumo wa kiutendaji wa sasa hata bei ya UMEME ikiongezwa ten-fold au ruzuku iongezwe ten-fold hakuna jipya litakalotokea Kwa maana kuongeza huduma au ubora wake.
 
Asiyeweza kununua Umeme ajifanyie mgao wa kutumia kwa wiki Mara mbili na asiyeweza kuna vibatari na chemli na mishumaa mingi
 
There is still a long way to go kwa watanzania kupata maisha stahiki na yalito bora kwa kuwa hatujui hata haki zetu za msingi. Unajua nishati ni driving factor ya uchumi, ukitemper na nishati unaathiri maisha ya mwananchi wa kawaida hata ambaye hatumii hiyo nishati direct. Kwa let's not support ujinga huu wa Tanesco na serikali, hili ni tatizo kwa uchumi wa Tanzania. I wonder why hata wabunge wall kimya katika hili.
 
shirika limekusanya hela nyingi 3% REA wala hatujui wamezifanyia nini vijiji vyenyewe hakuna umeme serikali na Tanesco kuna mchezo wanafanya
 
Utakuwa unaishi miaka kama 20 nyuma; hela za serikali zinatokana na kodi zetu! Na zaidi zinatoka pia nje ya wale wenye umeme majumbani: Kutumia hizo hela ku-subsidize watumiaji umeme ni uhuni. Nashauri wanaoneemeka na umeme ndio wenyewe walipie huduma yao. Hapa Unafiki uko wapi?
tumia busara tu kwenye utetezi wako na wala sio kejeli sijui kuwalipisha umeme wasotumia sijui ni uhuni sijui nini. Kwani hayo mashangingi mnayotumia wanapanda watz wote? mbona nyinyi mnaoyapanda msiyalipie gharama za uendeshaji toka mifukoni mwenu. Maana ingekuwa ni mapendekezo yetu mngetumia suzuki ama Rav4.
Wekeni mikataba ya kinyonyaji hadharani tujue inasemaje maana hapo ndio mnapotuumizia tumechoka kulipishwa hela tusizojua mikataba inasemaje.
 
Back
Top Bottom