Hizi Mali za CCM hizi, msaada wa kisheria jaman.

Selous

JF-Expert Member
Jan 13, 2008
1,325
144
Sourc: Mwananchi.
MBUNGE wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema) amesema wiki hii itakuwa ya kihistoria wakati Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, litakapopitisha azimio la kurejesha mali za umma, zilizoporwa na CCM.
Alitaja mali hizo kuwa ni pamoja na kiwanja chenye hati namba 056038/94 chenye ofisi za CCM Moshi Mjini na eneo la hekari 2.7 lenye hati namba 15686 la Umoja wa Vijana wa Chama Chama Mapinduzi (UVCCM) mkoani Kilimanjaro.Ndesamburo aliwaambia waandishi wa habari jana mjini Moshi kuwa, wamefanya upekuzi wa kisheria katika ofisi ya msajili wa hati katika kanda ya kaskazini na kuthibitisha kuwa viwanja hivyo bado vipo kwa jina la halmashauri.

Mbunge huyo alisema Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo lenye madiwani 24 wa Chadema na watano wa CCM, litapitisha uamuzi huo Alhamisi wiki hii.Alisema maamuzi hayo ni magumu lakini yana maslahi ya umma.Ndesamburo alisema uamuzi wa halmashauri kuipa CCM mali hizo za umma, ulifanywa na madiwani wa chama hicho tawala, huku wakifahamu kuwa zilikuwa ni za wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao.

"Haiingii akilini watu wachache wanakaa na kuamua kuipa CCM mali zinazomilikiwa na wananchi wote,"alisisitiza Ndesamburo.Mbunge huyo alifafanua kuwa mali ya umma haiuzwi kupitia utaratibu wa madiwani kupiga kura na badala yake kwa kutangaza zabuni ili Watanzania wote washiriki katika kununua.

Ndesamburo alisema badala yake, madiwani wa CCM kwa kutumia wingi wao, waliamua kuwa wao ndio walalamikaji na mahakimu na hatimaye kujipatia mali hizo, jambo ambalo halikubaliki

Mbunge huyo alisema Watu wote wanaokaa au kutumia mali zilizopo katika viwanja hivyo, watalazimika kuingia mikataba upya na halmashauri na hata kama CCM watakubali kugeuka kuwa wapangaji hiyo ni ruksa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Bernadette Kinabo alipoulizwa, kuhusu azimio hilo, alisema hoja hiyo ni mfu na kwamba mali hizo zinamilikiwa kihalali na CCM."Hili jambo halina uhusiano na sheria ya manunuzi ya umma wala zabuni kwa sababu linahusu ardhi lilipelekwa kamati ya mipango miji na baadaye likapata baraka za madiwani wa wakati huo kwa hiyo ni halali kisheria,"alisema Kinabo.

Kinabo alisema kama suala ni sheria ya manunuzi ya umma au ya zabuni kukiukwa, inakuwaje madiwani hao wanalipeleka katika Baraza lao ambalo lina nguvu ya kisheria kama lile lililopitisha maamuzi hayo.

Viongozi wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa Manispaa ya Moshi, Godfrey Mwangamilo, wamekaririwa wakisema viwanja hivyo na mali zilizomo ndani yake ni za CCM na taasisi ya zake.

Hivi baraza la madiwani lina uwezo wa kumega eneo la shule ya Mapambano primary na kumpa Idi Azzan????? Bit confused.
 
Back
Top Bottom