Hiyo ndio ilikuwa Mbuguni (Kwa sasa Mererani) enzi hizo

godson Lomayani

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
538
711
Nakumbuka miaka ya 1989-93, nilizamia Mbuguni kwa sasa Mererani kwenda kusaka Tanzanite nilishawishika kwenda huko baada ya kuona rafiki zangu niliosoma nao wanaporudi mtaani wakifanya kufuru ya matumizi ya fedha baada ya kuuza Tanzanite.

Kwa kweli kipindi kile mtu aliyetoka Mererani kuja Arusha mjini ndio alikuwa akionekana mfalme na kina dada wa Arusha, haikujalisha jinsi alivyokuwa akionekana kuchafuka nguo na sura kuwa nyeusi kwa lile vumbi la kwenye mashimo lenye ulanga.

Ukisikia pikipiki HONDA CC 250 zikiendeshwa kwa fujo unajua ni jamaa wameingia mjini toka Mbuguni. Kuna duka moja pale Arusha liko mkabala na jumba la sinema Metropole linauza pamba kali kwa bei ghali linaitwa London Bazaar jamaa walikuwa wakitoka machimboni ndio walikuwa wanakwenda kufanya shopping hapo.

Jeuri ya pesa mtu ananunua nguo za mamilioni bila kutetereka na baadae anaingia viwanja kukamua. Basi baada ya kuona hali ile ilibidi nitoroke home na kwenda Mbuguni. Kwa kweli nilipofika tu niliona mazingira ya kule yamekaa kishari shari bangi zinavutwa hadharani ukimzingua mtu anaweza kukupiga panga yaani vurugu tupu.

Jamaa yangu alinipeleka eneo la machimbo linaloitwa Zaire nilizama shimoni na kuanza kusaka Tanzanite kazi ilikuwa nzito lakini nilikuwa najipa moyo iko siku nitapata kipande cha "jiwe" piga kazi kwa nguvu zote baada ya baruti kulipuliwa tukakuta mkanda ambao wataalamu wanakuambia ukichimba kwa kuufuata huo mkanda ndio dalili ya kupata madini tuliongeza juhudi na hatimaye tulikikuta chungu kilichokuwa na Tanzanite.

Rafiki yangu aliniambia hapa tayari tumeula, tukiwa katika harakati ghafla aliingia mshika kofia ambae ndio mbabe aliyeaminiwa na tajiri mwenye shimo kwamba madini yakipatikana yeye ndio atakuwa na jukumu la kuhakikisha hachukui mtu yeyote isipokuwa yeye tu na kuyawasilisha kwa bosi mwenye shimo.

Baada ya kuhakikisha mali iliyopatikana alichukua kipande kimoja cha Tanzanite chenye uzito wa gramu 5 na kumpa yule rafiki yangu na kumpa maagizo wakutane Arusha pale Ottu House sehemu iliyokuwa busy kwa uuzaji wa Tanzanite enzi hizo.

Yule mshika kofia alitangulia kuondoka siku ileile na mzigo kwenda Arusha kuukabidhi kwa 'Kifaru' au 'Digala' wakati anaondoka alimwambia yule rafiki yangu watawasiliana. Basi sisi tulibaki shimoni hadi kesho yake jioni tukaondoka Mbuguni kuelekea Arusha.

Rafiki yangu alinipakia kwenye pikipiki alikuwa anatembea kwa speed ya kutisha nakumbuka tulitumia muda mfupi sana kutoka Mbuguni hadi eneo la KIA ulipo uwanja wa ndege. Tukaikamata barabara ya lami kutoka airport kuja barabara kubwa ya Moshi-Arusha kwa kweli kama ni mwoga unaweza kuomba ushuke utafute usafiri mwingine.

Kwa sababu ule mwendo haukuwa wa kawaida, tulifika njia panda na kuchukua uelekeo wa Arusha shughuli ikawa ileile. Tulikuwa tunayapita magari kama yamesimama.Tuliingia mjini Arusha majira ya saa 2 usiku. Niliteremka Mianzini jamaa yangu akaniambia asubuhi saa moja anikute pale ili tuelekee Ottu House, akaenda nyumbani kwao Sakina.

Basi nikapita madukani nikafanya shopping ya mazagazaga kwa ajili ya wazee nilichukua Taxi na kuelekea home kitendo cha kubisha hodi alifungua mlango mdogo wangu wa kike aliponiona ni mimi akapiga kelele Kaka Gooodi! nikamwambia ndio mimi nilikuwa nimechafuka na vumbi jeusi la mashimoni lililokuwa na ulanga.

ITAENDELEA............

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka huku mtaani walikuwa wakija wanakuja na fujo kwelikweli.
Kuna Wanyaturu walizifuma wakawa wanatumia kwelikweli.
Walitanua sana wakanunua kiwanja na kujenga wakajenga.
Walipoanza kufulia wakauza nyumba zao wakarudi bush.
Nasikia maisha yaliwachapa wamebaki hawana kitu.
Sijui wakikumbuka zile bata walizokuwa wanakula wanajisikiaje na hali waliyonayo sasa.
Kuna tetesi mmoja wao alichanganyikiwa kabisa ila kwasasa alipona.
Hiyo ilikuwa miaka ya 2000 mwanzoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka miaka ya 1989-93,nilizamia mbuguni now MERERANI kwenda kusaka TANZANITE, nilishawishika kwenda huko baada ya kuona rafiki zangu niliosoma nao wanaporudi mtaani wakifanya kufuru ya matumizi ya fedha baada ya kuuza tanzanite,kwa kweli kipindi kile mtu aliyetoka Mererani kuja Arusha mjini ndio alikuwa akionekana mfalme na kina dada wa Arusha, haikujalisha jinsi alivyokuwa akionekana kuchafuka nguo na sura kuwa nyeusi kwa lile vumbi la kwenye mashimo lenye ulanga,ukisikia pikipiki HONDA CC 250 zikiendeshwa kwa fujo unajua ni jamaa wameingia mjini toka Mbuguni.Kuna duka moja pale Arusha liko opposite na jumba la sinema Metropole linauza pamba kali kwa bei ghali linaitwa LONDON BAZAAR jamaa walikuwa wakitoka machimboni ndio walikuwa wanakwenda kufanya shopping hapo,jeuri ya pesa mtu ananunua nguo za mamilioni bila kutetereka na baadae anaingia viwanja kukamua.Basi baada ya kuona hali ile ilibidi nitoroke home na kwenda Mbuguni,kwa kweli nilipofika tu niliona mazingira ya kule yamekaa kishari shari bangi zinavutwa hadharari ukimzingua mtu anaweza kukupiga panga yaani vurugu tupu,jamaa yangu alinipeleka eneo la machimbo linaloitwa ZAIRE,nilizama shimoni na kuanza kusaka tanzanite kazi ilikuwa nzito lakini nilikuwa najipa moyo iko siku nitapata kipande cha "jiwe" piga kazi kwa nguvu zote baada ya baruti kulipuliwa tukakuta mkanda ambao wataalamu wanakuambia ukichimba kwa kuufuata huo mkanda ndio dalili ya kupata madini tuliongeza juhudi na hatimaye tulikikuta chungu kilichokuwa na tanzanite,rafiki yangu aliniambia hapa tayari tumeula,tukiwa katika harakati ghafla aliingia mshika kofia ambae ndio mbabe aliyeaminiwa na tajiri mwenye shimo kwamba madini yakipatikana yeye ndio atakuwa na jukumu la kuhakikisha hachukui mtu yeyote isipokuwa yeye tu na kuyawasilisha kwa boss mwenye shimo.Baada ya kuhakikisha mali iliyopatikana alichukua kipande kimoja cha tanzanite chenye uzito wa gramu 5 na kumpa yule rafiki yangu na kumpa maagizo wakutane Arusha pale OTTU house sehemu iliyokuwa busy kwa uuzaji wa tanzanite enzi hizo.Yule mshika kofia alitangulia kuondoka siku ile ile na mzigo kwenda Arusha kuukabidhi kwa KIFARU au DIGALA wakati anaondoka alimwambia yule rafiki yangu watawasiliana.Basi sisi tulibaki shimoni hadi kesho yake jioni tukaondoka Mbuguni kuelekea Arusha,rafiki yangu alinipakia kwenye pikipiki alikuwa anatembea kwa speed ya kutisha nakumbuka tulitumia muda mfupi sana kutoka Mbuguni hadi eneo la KIA ulipo uwanja wa ndege,tukaikamata barabara ya lami kutoka airport kuja barabara kubwa ya Moshi-Arusha kwa kweli kama ni mwoga unaweza kuomba ushuke utafute usafiri mwingine,kwa sababu ule mwendo haukuwa wa kawaida,tulifika njia panda na kuchukua uelekeo wa Arusha shughuli ikawa ile ile,tulikuwa tunayapita magari kama yamesimama.Tuliingia mjini Arusha majira ya saa 2 usiku,niliteremka Mianzini jamaa yangu akaniambia asubuhi saa moja anikute pale ili tuelekee OTTU HOUSE, akaenda nyumbani kwao Sakina.Basi nikapita madukani nikafanya shopping ya mazagazaga kwa ajili ya wazee nilichukua Taxi,na kuelekea home kitendo cha kubisha hodi alifungua mlango mdogo wangu wa kike aliponiona ni mimi akapiga kelele Kaka Gooodi! nikamwambia ndio mimi nilikuwa nimechafuka na vumbi jeusi la mashimoni lililokuwa na ulanga.ITAENDELEA..

Sent using Jamii Forums mobile app

Unapenda kubembelezwaa eeh?

Haka katabia ka itaendelea sijui mmekatoa wap n kakishamba
 
Kumbe LONDON BAZAAR bado ipo.Mwaka 1978 nikiwa std7 Uhuru primary mwalimu wangu wa darasa alinituma hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka huku mtaani walikuwa wakija wanakuja na fujo kwelikweli.
Kuna Wanyaturu walizifuma wakawa wanatumia kwelikweli.
Walitanua sana wakanunua kiwanja na kujenga wakajenga.
Walipoanza kufulia wakauza nyumba zao wakarudi bush.
Nasikia maisha yaliwachapa wamebaki hawana kitu.
Sijui wakikumbuka zile bata walizokuwa wanakula wanajisikiaje na hali waliyonayo sasa.
Kuna tetesi mmoja wao alichanganyikiwa kabisa ila kwasasa alipona.
Hiyo ilikuwa miaka ya 2000 mwanzoni

Sent using Jamii Forums mobile app

Haha ni aibu watu wajue una pesa nyingi hlf baadae ufilisike feitty
 
Na wanawake waliowaoa waliwaacha.
Wamebaki na kumbukumbu kwakuwa walizaa nao.
Kufulia kubaya hata kama watu hawajali ila nafsi ya mtu huwa inakuwa inajistukia.
Pesa tamu
Sasa uishike halafu ije ipotee huo msoto wake sio mchezo.
Afadhali usote wee halafu ndio uzishike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi za akina Askofu, Sunda, Papa King na wengine. Ila yale madini yalileta impact kwa wananchi wa kawaida sana japo walitumia pesa vibaya. Pengine yalikuwa na impact kuliko madini mengine yote kwasababu yalishikiliwa na wazalendo na sio makampuni ya nje.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom