Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,351
- 6,479
Nimeona mara nyingi watanzania wanasafisha pua zao kwa kutumia vidole halafu wanataka kukupa mkono wakati wa kusaliamiana au (kwa wale wakristu kupeana amani kanisani), kushika milango vitu ambavyo ni rahisi kuambukiza magonjwa ya mafua. Vitambaa hivi aina ya leso vinauzwa kwa wingi barabarani na madukani kwa bei nafuu kabisa na wengi tunanunua lakini bado tunatumia vidole kusafisha pua zetu. Hivi tatizo hapa nini? Pia hatunawi mikono mara kwa mara hivyo kujikuta tunaambukizana magonjwa kama 'red eyes', minyoo. Je kifanyike nini ili watu wanawe mikono na kusafisha pua zao kwa leso badala ya vidole? Kama uamini angalia kuanzia sasa mpaka j3 utuambie umeona wangapi wanasafisha pua kwa vidole vyao.