Hivi vituo vya Redio ni njaa kali au?

notyfeky

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
673
663
Hivi hii imejaaje wakuu? Kila redio stesheni ukifungulia ni michezo ya kubahatisha, mara cheza pesa, sijui mshiko chap n.k Sasa kuna tofauti gani na betting?

Halafu vijana wakibeti mnasema wanapoteza muda, hii cheza buku ushinde laki si ndo kamari kabisa?

Tena bora niweke treni langu mkeka nashuhudia ukichanika laivu laivu kwa wajinga kama PSG, Chelsea na Mamelodi Sundowns kuliko unishawishi nitume pesa yangu eti ntashinda Laki wakati hata vigezo vya kushinda ni unknown, mnachezeshaje huko hatujui, labda kama pesa yangu haina kazi.

Nikiwa na buku naweka mikeka yangu kumi ya miamia, hata ikichana yote fresh tuu, pesa yangu imeenda kihalali kabisa, yaani sina mashaka na hilo.

Ngoja nicheke hapa: Kuna vizee vinapondea betting halafu vinacheza hii michezo ya kubahatisha redioni, huwa nawacheki nacheka kimoyomoyo.

Hivi wadau biashara ya redio nayo ni kama magazeti nowdays, eti eeeh? Maana hadi redio yetu ya nchi kuanzia Am mpaka kule fm ni kamari mwanzo mwisho.

Wanangu wa betpawa tupieni matreni hapahapa tusonge nayo.

Ni mwendo wa kamari mwanzo mwisho.
 
Radio ni biashara, na inategemea 95% matangazo hivyo kwao kuwa na hayo matangazo mengi ambayo ni halali kwao ni mafanikio. kama ilivyo radio ya kanda ya ziwa karibu zote zina matangazo mengi sana ya masuala ya amlezi na uzazi pamoja na kumasisha wanaume wa huko kutahiriwa.
 
Siyo matangazo mkuu, mada ni kuchezesha kamari
 
kwani hizo kamari si ndio matangazo yenyewe? ujue hizo kamari ama hayo makampuni ya kamari sio yao wanaingia ubia na watu wanachofanya ni ya kuyabadili majina tu ili kila radio ifanye kivyake kisha wanapewa kamisheni,Ukisikia chota mihela, mchezo supa, shika ndinga, n.k ni kampuni moja ila kwenye kila media wamejiweka kwa majina tofauti
 
Imefika kila hatua kila radio station ina kamari yake na inapewa promo 24/7

Pia zimeibuka radio na tv nyingi zinazorusha live matangazo ya kwenye makanisa ya waroho watu wanapunwa sadaka kwa njia ya Mpesa na Tigopesa.
 
Ni njia ya kuongeza kipato kumbukeni wan awafanyakazi wa kulipa na wanahitaji faida toka kwenye vituo. Kama hutaki kusikia mambo hayo sikiliza bbc au dw online hutasumbuka kuhusu habari
 
Vyanzo vya mapato hakuna , ubunifu hakuna , content za kuvutia watu hakuna unadhani wataacha kuwa chawa wa Betting ili waendelee kuishi? hawana namna vinginevyo ni kufa tu.
 
Ina maan hadi TBC FM nao wana njaa? Jana wakati nasachi redio ya kusikiliza baada ya kuweka pembeni smartphone nikababatiza TBC FM wanataka kutoa zawadi ya elfu 50 kwa mshindi, ikabidi niwasikilize kwa dakika kadhaa ili nithibitishe kuwa hadi vyombo vya habari vya serikali navyo vinatafuta hela kwa udi na uvumba.
 
Ni hatari mkuu
 
Vyanzo vya mapato hakuna , ubunifu hakuna , content za kuvutia watu hakuna unadhani wataacha kuwa chawa wa Betting ili waendelee kuishi? hawana namna vinginevyo ni kufa tu.
Kabisa mkuu, aibu sana
 
Ni njia ya kuongeza kipato kumbukeni wan awafanyakazi wa kulipa na wanahitaji faida toka kwenye vituo. Kama hutaki kusikia mambo hayo sikiliza bbc au dw online hutasumbuka kuhusu habari
Sawa ndugu mtangazaji
 
kwani hizo kamari si ndio matangazo yenyewe? ujue hizo kamari ama hayo makampuni ya kamari sio yao wanaingia ubia na watu wanachofanya ni ya kuyabadili majina tu ili kila radio ifanye kivyake kisha wanapewa kamisheni,Ukisikia chota mihela, mchezo supa, shika ndinga, n.k ni kampuni moja ila kwenye kila media wamejiweka kwa majina tofauti
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom