Hivi unyanyasaji wa kijinsia makazini utaisha kweli?

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,700
1,415
Kuna dada mmoja anaefanya kazi ofisi ya jirani ambaye huna tunakutana wakati wa kula na tumezoeana nae na hula pamoja na kupiga stori za hapa na pale.Juzi kaja akiwa mnyonge sana nikamuuliza vipi mbona umepooza sana leo akasema we acha tu sisi watoto wakike tuna mitihani mikubwa sana humu makazini.Anasema bosi wake amekuwa akimsumbua kwa muda mrefu eti anamtaka kimapenzi,huyo bosi kaoa na ana watoto wakubwa tu.Mara hii ya mwisho bosi kasema asipopata majibu mazuri hali yake pale kazini itaharibika na akikubali ataongezewa mshahara na marupurupu mengine kibao.Mara hii ya mwisho alipoitwa ofisini alihisi suala hilo litazungumzwa kwa hiyo akajifanya anachezea simu bosi alipokuwa anaongea pumba zake akarekodi yale mazungumzo anasema apeleka wapi ili hatua zichukuliwe?
 
Amkatalie tuu then akitaka mtimua amwambie nimerecord mazungumzo yako ntayapeleka kunako husika atatia akili
 
hili suala ni gumu sana, na watu wengi wanaathirika na hilo.....hebu kwa wale wanaofahamu sheria kuhusu sexual harassment watueleze watu tuwe tunafanyaje.....
 
Amkatalie tuu then akitaka mtimua amwambie nimerecord mazungumzo yako ntayapeleka kunako husika atatia akili

Hii ni njia moja anayofikiria lakini anataka ajue options zote kabla hajaamua.

hili suala ni gumu sana, na watu wengi wanaathirika na hilo.....hebu kwa wale wanaofahamu sheria kuhusu sexual harassment watueleze watu tuwe tunafanyaje.....

Kaamua kuvunja ukimya unaosumbua kina dada wengi,tumsaidie mawazo.
 
Kweli anastahili kumfundisha adabu, mwanaume wa kileo analazimisha penzi?! ametoka sayari gani huyo mwehu?!
 
apeleke TAWLA wampe msaada wa kisheria, CMA wakasuluhishe au mahakamani afungue kesi ya jinai.
Kama vipi ampe live bila kuhariri... (that she has recorded their conversation and can use that as evidence against him b4 the crt of law)
 
ninaichukia rushwa ya ngono kuliko zote!! ni heri nisifanye kazi kuliko hiyo rushwa, mapenzi nyoyo zenu waote zikongane bana!!
 
Uporoto01 unajua hata mie nilikuwaga nafikiria kuwa watoto wa kike tuna bahati mbaya kuzaliwa watoto wa kike untili nilipokuja kurealize kuwa uvictim wa sexual harrassment tunautaka na kuukubali wenyewe. Kwa namna gani basi
1. Kama wewe ni mfanyakazi mwenye qualifications unajiamimi na unadeliver according to the job descriptions za kazi/post yako hakuna nasema tena HAKUNA bosi wala mlinzi atayekusumbua. Tena mwonyeshe kuwa unajua haki zako kisheria (hata kama huzijui zote take trouble ya kujua chache). Unapoanza kuonyehsa dalili ya kuwa wewe bila favor huwezi basi unajiweka kwenye victim position na hawa mabosi waroho huwa wanasubiri those chances.

2. Kama huna qualification ya kazi unayoifanya jitahidi u-do something to prove kuwa you have experience ambayo inakupa ufanisi wa kazi. KMwonyeshe kuwa uko tayari kuacha kazi kuliko kuudhalilisha utu wako kwa kumfurahisha yeye (But mhakikishie kuwa the moment you loose your job kwa sababu yake s/he is going down with you and worse enough him/her with the sameful act ever imargine- Hata kama hujawahi record mwambie you have evidence... believe me hata kama atakufukuza kwa kashfa kiasi gani moyoni atabakia akisema ..... daaaah mwanamke ana msimamo balaa and he is going to respect you for than

Lastly akumbuke Imani yake ya dini... aamini na kujua kuwa kama anaikimbia dhambi kiukweli basi ajue MUNGU ana mipango mikubwa kwake na she is going to be rewarded thrice!!
 
siachi kazi kwa mtu kuninyanyasa kijinsia aisee ataacha yeye au abaki na achunge heshima yake. Kinyume na hapo ...that spark must lead to an explosion.
 
mj1, kutokujua haki na wajibu wako na kutojiamini na chanzo cha matatizo kama hayo. Mtu unakuwa unsecured na mwisho wa siju unaona ulinzi pekee wa kibarua chako ni kujiachia.
 
siachi kazi kwa mtu kuninyanyasa kijinsia aisee ataacha yeye au abaki na achunge heshima yake. Kinyume na hapo ...that spark must lead to an explosion.

...HA HA HA, mbona kama ushaanza kurushia ngumi kivuli wewe?

Hujaona mbwa akijipeleka kwa chatu shingo upande na mkia kati ya miguu!?
Sexual Harrasment inaniudhi sana lakini for some reason kuna kina dada wanadhani ni haki yao 'kudhalilishwa,' ili kupata azma zao na hivyo kuwaweka pabaya wengi waliobakia.

Unaweza nyanyasika indirectly,
mfano; wewe na degree yako...unaongozwa na kabinti mwenye certificate tu.
Kwakuwa yeye ni chakula ya bosi kanakupelekesha na pa kushtakia huna, Unless nawe 'uingie ubia'
 
Mbu we acha tena kivuli chenyewe cha gizani.
Huo uoga wa mbwa hapa hautumiki aisee. Na usemacho ni sahihi baadhi yetu huwa tunaona ni sawa tu kudhalilishwa kwa kupewa upendeleo ambao hata hauna mantiki yoyote.
Sasa huo ubia unaingiaje na bosi wako? Mbu u will asking for trouble bora uvumilie kuendeshwa na kabinti ka bosi lol!
 
Hehehe bora upate boss uliemzidi elimu kuliko boss tineja!
 
Hii ni njia moja anayofikiria lakini anataka ajue options zote kabla hajaamua.

Kaamua kuvunja ukimya unaosumbua kina dada wengi,tumsaidie mawazo.

hivi (he) hawasumbuliwi?, kaka mmoja alinisimulia kisa chake cha kuacha kazi kuwa boss wake (she) alimtaka ki ngono, alipochelewa kumkubali shuruba zikaanza. Akaona atimke.
 
Back
Top Bottom