Hivi uamuzi wa kuoa unakujaje jamani?

mchambuzixx

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
1,292
943
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 33, yaani katika maisha yangu yote toka nipo chuo hadi namaliza sikuwai kuwa na mawazo wala kufikiria kuoa, wakati nipo mwaka wa 4 chuoni nilimpa mimba mwanamke niliekuwa nae kwenye mahusiano, ni mimba ambayo haikuwa kwenye makubaliano na ilileta pukurushani sana, lakini nilichokuja kukigundua ni yule niliyezaa nae ni kama aliweka mtego flani wa mimba ili nimuoe.

Lakini hicho kitu hakikutokea kutokana na msimamo wangu maana niliona vijana wengi wanaingia kwenye hio mitego kisa kumpa mtu mimba huishia kuoa baadae inaleta shida ni kama mtoto ndie anaefanya ile ndoa iwepo tulifanikiwa kupata binti hadi sasa ana miaka 6 na yupo kwa mamake mahitaji yote yanapelekwa ikiwemo ada katika shule zetu zile za kisasa jamani apetite ya kuoa ilianza kunitoka kutokana na ndoa za marafiki zangu zilivyokua zinaenda shaghala bagala.

Kuna rafiki yangu mmoja tumemchangia hela nyingi aoee wameoana hata miaka miwili haijafika kumbe bint alikuwa na uhusiano na mzungu na kazaa mtoto wa kizungu pure ndoa ikafia hapo hapo, wenigne tukikaa kwenye vikao vyetu vya bia ndo wanakwambia kabisa kama hujaoa bora ujitulize dogo utaishi vizuri sana jamani sio siri maisha yangu ni mazuri sana hayana stress za wanawake kabisa ingawa umri unaenda sina mawazo hayo kabisa.

Hata nikiwa na mahusiano na mwanamke nitamwambia nina mtu na yeye anaiba basi usumbufu wa kuoana unapungua sema tuu mother ndio anasumbua kila akipiga simu tukipiga story za hapa na pale atagusia hilo swala la kuoa lakini halazimishi yeye anasema tuu mzee wako kaondoka hujaoa hutaki hata mimi nione harusi yako.

Maana kila siku sisi tunachangia watu tu, hivi mlioa au kuolewa hayo maamuzi yalikuja tuu au kuna maombi ndani yake? Maana wengine mawazo hayo hatuna kabisa yaani, mawazo yangu huwa ni kutafuta hela tu sasa sijui kwasababu nina haka katoto kangu kabinti kamoja kanakofanya hata nisifikirie.
 
maziwa na nyama unavipata hivi utakuwa na shida na ng'ombe wewe??

ushauri, ndoa ni karama toka kwa Mungu hivo jitahidi umuombe na atakupatia Mke mwema tena Mali yako peke ako na hautashare na mtu.
 
Sio watu wote walio kwenye ndoa wanakumbwa na misukosuko kama ya rafiki yako,kuna changamoto za kila siku kama katika maisha yetu and it makes life worth living,we need some spices hata ubongo usipoupa challenge unadorora na kuzembea.Na changamoto hizohizo zinapima imani zetu,upendo wetu,uvumilivu wetu na hatimae kujenga stronger bond.Muhimu kati ya yote uoe mtu sahihi ambae mnaendana,mnaelewana,mnapendana,mnaheshimiana n.k Haimaanishi kwa sababu mtu kajitupa baharini akazama kwasababu hajui kuoga basi watu wote wasioge.Ingia kwenye ndoa with ur head high up and be aware of what to expect and what not to expect.
 
Ukihitaji staha na heshima kwa jamii inayokuzunguka lazima uoe/uolewe. Swali ni je mke na mme atoka wapi????????????? "Mke/mme bora atoka kwa mungu" Kwani usimuulize mungu alipo mkeo ili akuonyeshe???????????? Usitumie matamanio yako ya mwili hutavuka salama.
 
Sio watu wote walio kwenye ndoa wanakumbwa na misukosuko kama ya rafiki yako,kuna changamoto za kila siku kama katika maisha yetu and it makes life worth living,we need some spices hata ubongo usipoupa challenge unadorora na kuzembea.Na changamoto hizohizo zinapima imani zetu,upendo wetu,uvumilivu wetu na hatimae kujenga stronger bond.Muhimu kati ya yote uoe mtu sahihi ambae mnaendana,mnaelewana,mnapendana,mnaheshimiana n.k Haimaanishi kwa sababu mtu kajitupa baharini akazama kwasababu hajui kuoga basi watu wote wasioge.Ingia kwenye ndoa with ur head high up and be aware of what to expect and what not to expect.

Take my like
 
Kaka yangu acha uzinzi baada ya kuacha - piga goti mwambie Mungu nahitaji kuoa naomba unipe mke, maana naamini mke mwema anatoka kwako. AMENI, kaka utapata mke na uoe na utabarikiwa na mama yako atafurahi sana na kukubariki.
 
hata kama una 33yrs nahisi bado hujaiva kuwa na mke (wewe bado mtoto). ukikua wala hutakuja JF kuuliza inakuwaje. Yaani utajikuta bila kulazimishwa unaanza kuhaha kutafuta mchumba kama unavyotafuta hao wa siku moja moja.
 
Wakati wako haujafika bado naamini siku ipo,ama inakuja ambapo utakutana na binti mmoja ambaye hutotamani akupotee tena machoni...ni hapo sasa wimbo utabadilika kichwani!
 
Sio kila mtu anayekuja duniani amepangiwa WITO huo mtakatifu.

Na wewe si wa kwanza. Go ahead with ur life.
 
Nadhani hii thread yako inaashiria hitaji lako lililojificha la kuoa. Kama usingekuwa na hitaji nadhani usingejisumbua hata kuandika yote haya.
 
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 33, yaani katika maisha yangu yote toka nipo chuo hadi namaliza sikuwai kuwa na mawazo wala kufikiria kuoa, wakati nipo mwaka wa 4 chuoni nilimpa mimba mwanamke niliekuwa nae kwenye mahusiano, ni mimba ambayo haikuwa kwenye makubaliano na ilileta pukurushani sana, lakini nilichokuja kukigundua ni yule niliyezaa nae ni kama aliweka mtego flani wa mimba ili nimuoe.

Lakini hicho kitu hakikutokea kutokana na msimamo wangu maana niliona vijana wengi wanaingia kwenye hio mitego kisa kumpa mtu mimba huishia kuoa baadae inaleta shida ni kama mtoto ndie anaefanya ile ndoa iwepo tulifanikiwa kupata binti hadi sasa ana miaka 6 na yupo kwa mamake mahitaji yote yanapelekwa ikiwemo ada katika shule zetu zile za kisasa jamani apetite ya kuoa ilianza kunitoka kutokana na ndoa za marafiki zangu zilivyokua zinaenda shaghala bagala.

Kuna rafiki yangu mmoja tumemchangia hela nyingi aoee wameoana hata miaka miwili haijafika kumbe bint alikuwa na uhusiano na mzungu na kazaa mtoto wa kizungu pure ndoa ikafia hapo hapo, wenigne tukikaa kwenye vikao vyetu vya bia ndo wanakwambia kabisa kama hujaoa bora ujitulize dogo utaishi vizuri sana jamani sio siri maisha yangu ni mazuri sana hayana stress za wanawake kabisa ingawa umri unaenda sina mawazo hayo kabisa.

Hata nikiwa na mahusiano na mwanamke nitamwambia nina mtu na yeye anaiba basi usumbufu wa kuoana unapungua sema tuu mother ndio anasumbua kila akipiga simu tukipiga story za hapa na pale atagusia hilo swala la kuoa lakini halazimishi yeye anasema tuu mzee wako kaondoka hujaoa hutaki hata mimi nione harusi yako.

Maana kila siku sisi tunachangia watu tu, hivi mlioa au kuolewa hayo maamuzi yalikuja tuu au kuna maombi ndani yake? Maana wengine mawazo hayo hatuna kabisa yaani, mawazo yangu huwa ni kutafuta hela tu sasa sijui kwasababu nina haka katoto kangu kabinti kamoja kanakofanya hata nisifikirie.

Ukiwa muislamu ambaye umeamua kufuata dini yako. Mungu anakupa mke ambaye atakufanya ufumu na ndoa hiyo. Muogope mungu. Uzinzi haufai. Mrejee mungu then owa.
 
Miaka 33 Mwanamme unasema huna hamu sijui hujisiki,hiyo siku yakujisikia na nguvu pia zimekwisha wanakusaidiaje kumshughulikia mkeo,nadhani unatakiwa ukuwe ki mawazo ukiwa kama mwanamme,huna hamu ya kuitwa Dad au uwe na familia yako uitwe Dad someday? kama mwenyezi mungu amekujalia uwezo tafuta mke oa ili mzee wako nae afurahi kua mwanangu amekua A Real man,na akija anakuja kuwaona wajukuu zake anacheza nao na kufurahi,huyo mtoto alokua kwa mamake bado haina raha kama pale mkeo yuko ndani ya nyumba mnale Mimba pamoja na una wish lini ntamuona mtoto wangu au lini ntamshika mtoto wangu kwa mara ya kwanza ambae ana beba jina langu, wacha niishie hapa mkuu samahani kama ntakua nimekukera...
 
Ha ha hamkuu kama wazola kuoa huna bas acha uzinzi na uache kuharib watoto wa watu
 
Back
Top Bottom