khayanda
JF-Expert Member
- Nov 6, 2007
- 247
- 25
Tanzania ni nchi nzuri ambayo viongozi wake wamekazania kuiharibu kwa makusudi. Tufunge na kuomba hawa watu wanotuharibia nchi yetu watahayari na kutuachia nchi yetu bila kutuachia matatizo makubwa ambayo yanaendelea kujijenga kila siku. Hawa watu hawana huruma na hawana aibu wala soni kama mfalme majuju. Tutafanyaje jamaniii?
Nchi yoyote ambayo viongozi wenye dhamana ya kuhakikisha sheria zilizopo zinafanya kazi, wanakuwa wa kwanza kuzivunja, basi hakuna sheria itakayofanya kazi. Tunayoyaona kama ugawaji wa viwanja holela, wizi katika mabenk, mauaji ya hovyo, ni kwa vile viongozi wetu na walinzi wetu wa amani ndiyo wanaoongoza mauaji, wanachukua viwanja hovyo. Kuna mheshimiwa pamoja na kujiuzulu wadhifa wa uwaziri, amepewa eneo la Magereza Morogoro anajenga kitu chake. Nafuu hata aliyeteka eneo la wazi la pwani yetu.
Tumwombe Mungu atusaidie kuwaadhibu hawa jamaa maana sisi wametushinda. Hatuwezi kugoma, hatuwezi kuandamana na wala kuwapiga. BASI TUTUMIE IBADA NA MAOMBI KWA DINI ZOTE