Viongozi wote wa Dini iwapendeze kuteua siku maalum kwa ajili ya kumlilia Mungu aliponye taifa kwa yanayoendelea

Isalu

JF-Expert Member
Nov 3, 2022
504
664
Kwa hali ilivyo nchini mwetu namna viongozi wetu wanavyoiendesha nchi, Kwa mikataba ya vificho yenye kuliingiza taifa kwenye hasara mfano ikiwa kuibinafsisha bandari yetu ambayo ni nguzo kuu ya uchumu wetu,na mikataba mingine mingi yenye agenda za Siri tusiyoijua.

Iwapendeze viongozi wetu wa dini zote kuteua siku maalum kwa ajili ya kuliombea taifa,kengele makanisani zipigwe mara 3 kuashiria msiba na maombolezo kwa haya yanayoendelea nchini.

Nimejaribu kufuatilia pia bungeni namna pia msukuma na wenzake bungeni wanavyolipigia debe suala la kuibinafsisha bandari na ziara yake ya Dubai akiwa na kamati ya Mbarawa ambao ni hao hao wanaitumbukiza nchi shimoni.

Na inaashiria kabisa wameandaliwa kwa kazi hiyo kupiga debe kwa kisingizio cha kutuwakilisha wananchi kupitia bunge.

Itoshe kuishia hapa Maana napata maumivu makubwa kushuhudia mambo haya ya hovyo yanayotendwa na watu tuliowaamini na kuwapa dhamana ya kuiongoza nchi.

Ninaomba tumlilie Mungu peke yake ndiye wa kutujibu dhidi ya watesi wetu hawa, tulionao kwenye nchi hii yetu nzuri tuliyopewa na Mungu wetu.
 
Anayeweza kufanya hivyo kwa Uthubutu ni Sheikh Ponda tu. Na labda Askofu Mwamakula.
 
Kwani tatizo lipo kwa shetani au mafisadi hata tuombe vipi kama watu hawabadiliki ni hawabadiliki tu.
 
Pole sana, unateseka ukiwa wapi ?

20230602_010910.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom