Hivi Tanzania daima wana uhusiano na Gazeti la Hoja?

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Nimesoma habari kuu ya leo kutoka Tanzania daima nimeona kuna mahala imeandikwa kwamba Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo Ndugu Absalom Kibanda jana alidhaminiwa na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Hoja Ndugu Yasin Sadiq.

Sehemu ya gazeti inasomeka hivi "Hata hivyo, katika hatua isiyo ya kawaida, huku wakijua kwamba bado ana dhamana, polisi walimzuia tena Kibanda akiwa na mawakili wake Nyaronyo Kicheere na Juma Thomas, wakamlazimisha awe na mdhamini mwingine kwa kiasi cha sh milioni tano. Mhariri Mtendaji wa gazeti la Hoja, Yasin Sadiq, alimdhamini ". Binafsi nimekuwa nikiyasoma magazeti yote mawili na nilichogundua ni kuwa kila gazeti lina itikadi zake zinazopinganza na lenzake. Hoja siku zote wanawatetea watuhumiwa wa Ufisadi na limekuwa likiponda hata Makala zinazochapishwa na Tanzania daima.

Mfano kuna kipindi Naibua Mhariri Mtendaji wa Tanzania daima ndugu Ansbert Ngurumo akiwa Uingereza (Hull University) kimasoma alichafuliwa na Gazeti la Hoja kwamba anaiponda serikali ya JK kwa kuwa alitoswa kwenye uteuzi wa Ukuu wa Wilaya. Lakini nimeshangaa sana kusoma kuwa Jana Mhariri Mtendaji wa Hoja amemdhamini Mhariri wa Gazeti pinzani lake katika kesi yake ya Uchochezi inayomkabili.

Source:
Siri yafichuka kukamatwa kwa Kibanda
 
Na Saeed Kubenea alivyomdhamini juzi nalo linauhusiano na Tz Daima? Jitizame upya tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom