Hivi si mliambiwa muache kujilinganisha na nchi ambazo hazitoi takwimu za kirusi!

Upande wa kaskazini kuna sauti zishaanza kusikika za kutamani kuomba msamaha.

[https://res]

Na WINNIE ATIENO

WAWEKEZAJI katika sekta ya utalii wamemsihi Rais Uhuru Kenyatta angilie kati na kusuluhisha utata wa usafiri wa ndege kati ya Kenya na nchi jirani ya Tanzania.

Wawekezaji hao wanashtumu serikali ya Kenya kwa kuwalazimisha raia wa nchi jirani ya Tanzania kuwekwa karantini ya lazima kila wanapoingia nchini kufuatia janga la corona.

Kupitia muungano wa wadau wa utalii nchini yaani Shirikisho la Utalii la Kenya – Kenya Tourism Federation – wawekezaji hao walisema Kenya haifai kuwahukumu Watanzania kutokana na hatua yao ya namna wanavyokabiliana na janga la Covid-19.

“Tumewakosea wenzetu Watanzania na tunafaa kutafuta suluhu kwa sababu tukiendelea kuwatenga na kuwatema nje ya orodha ya raia wa nchi kadhaa ambao wanakubaliwa kuingia humu nchini Kenya bila vikwazo kama vile karantini, basi mzozo huu utaendelea na huenda hata wakafunga mipaka yao,” alisema mwenyekiti wa muungano huo Bw Mohammed Hersi.

Bw Hersi alionya kuwa huenda mzozo huo ukatokota zaidi baada ya Tanzania kupiga marufuku kampuni tatu za ndege za humu nchini.

“Hatua ya kuwatenga watanzania kwenye orodha ya raia wanaoruhusiwa nchini bila vikwazo ndio imetuletea balaa hii, hatuwezi kwenda kwa jirani zetu tunavyotaka ilhali hatutaki waje kwetu. Kainaya ni kwamba malori na mabasi yanapita mipakani bila vikwazo vyovyote,” aliongeza.

Bw Hersi alisema sekta za utalii, biashara na usafiri wa ndege zitabeba msalaba wa mzozo huo.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya Waziri wa Utalii na Wanyamapori, Najib Balala kusisitiza kuwa raia wa nchi ambazo ziko katika hatari ya maambukizi ya corona ikiwemo Tanzania watawekwa karantini ya lazima wanapowasili humu nchini.

Bw Balala alisema raia hao watawekwa karantini ya lazima ya siku 14 kulingana na mwongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Waziri huyo alisema Kenya itaendelea kudumisha usalama wa watalii katika juhudi za kuimarisha sekta ya utalii.

Nchi hizo zimekuwa kwenye mzozo kuhusiana na swala la virusi vya corona huku Tanzania ikisisitiza imekabiliana na janga hilo.

Bw Balala alisema mipaka ya Kenya ingali imefungwa lakini watalii wanaoingia humu nchini kupitia viwanja vya kimataifa vya ndege ni sharti wafuate kanuni za afya ili kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.

“Mipaka yetu ya barabara bado imefungwa lakini viwanja vyetu vya ndege viko wazi kwa watalii wa humu nchini na wale wa kimataifa kuzuru. Lakini tuna aina mbali mbali ya wageni; kuna wale wanaotoka nchi hatari zaidi, za maambukizi ya wastani na wale ambao wanatoka sehemu ambazo ziko shwari. Wale wanaotoka nchi ambazo zimetajwa hatari na WHO watawekwa karantini ya lazima kwa siku 14, ” alisisitiza Bw Balala ambaye alikuwa akijibu maswali kutoka kwa wawekezaji wa sekta hiyo kupitia mawasiliano ya mtandaoni
 
Mumesahau saa hizi hawachati wapo lockdown wamejificha wanaogopa kirusi mpaka saa 11 alfajir kikiondoka watatoka kukujibu
tatizo hua wanajibu kishabiki tu na wala si kwa point, unadhani hawaujui uhalisia wa mambo? wakenya wapo tofauti na sisi, watz tupo wazi sana kuelezea uhalisia tofauti na hawa ndugu zetu wanaficha aibu ya taifa lao akati behind the scene wanaumi
 
Kuna siku nili wa challenge wa kenya waliopo humu JF , una jua sayansi haidanganyi eh ... Hapa Tz tuna alot of kenyans to mentions fews francis kahata, joash onyango, beatrice ndungu, farook shikalu.... Iv mfano mtu kama kahata ligi ilipo simama tu ali rejea kenya Je mlishampima nankusema jamaa ni positive na corona ?
Juzi kati ali rudi tena kenyaa akitokea Tz je mlimpima mkamkuta na corona ? .....
Mtagundua serikali yenu ina leta biashara chafu ya kuchafuana vitu ambavyo sio vizuri
 
Mbona hamsikii
Naona hadi viongozi wenu akili zao zimeanza kurudi.













Hon Sonko, Tanzania hakuna Covid19, kama ingalikuwepo basi watoto wa shule za (vidudu pre-unit, kindergartens mpaka vyuo vikuu) zilizofunguliwa mapema June 2020 ungekuwa maelfu wanaumwa, wamekufa, Hospital zingejaa wagonjwa wa Covid19, makaburi yangalionekana kila pahala kwani ni kabila moja tu linachoma wafu wao(Hinduism)!!!! Miracles never ended with Old Testament!!! Usafi Wa Tz wanazingatia kama wizara ya afya inavyoelekeza lakini jua fika hata kabla ya kula chakula(ugali, nyama) kwa mkono lazima kunawa (else) amaa utaharisha, (cleanliness) usafi ni muhimu.
 
Waache wale misaada yao kwanza sisi tunasonga mbele.....corrupt leaders wamepata mradi

Yaonekana viongozi(mafisadi) ndani ya system wanaingiza nchini mwao vitu ambavyo vinasambaza Covid19 hasa barakoa(masks), dawa wanazonyunyuza(spraying), chemical reagents ambazo zimechanganywa na wadudu, ili tu viongozi wazidi kula hela za misaaaaaaada!! Tanzania ilipiga marufuku kupokea misaaada kuhusu uzuiaji wa Covid19 kutoka nje ya Tz, ilipiga marufuku in applying any type of chemicals from any foreign country including China!!! What was the result “NO COVID19” au cha mtoto au mjukuu wa Coronavirus.
 
Hon Sonko, Tanzania hakuna Covid19, kama ingalikuwepo basi watoto wa shule za (vidudu pre-unit, kindergartens mpaka vyuo vikuu) zilizofunguliwa mapema June 2020 ungekuwa maelfu wanaumwa, wamekufa, Hospital zingejaa wagonjwa wa Covid19, makaburi yangalionekana kila pahala kwani ni kabila moja tu linachoma wafu wao(Hinduism)!!!! Miracles never ended with Old Testament!!! Usafi Wa Tz wanazingatia kama wizara ya afya inavyoelekeza lakini jua fika hata kabla ya kula chakula(ugali, nyama) kwa mkono lazima kunawa (else) amaa utaharisha, (cleanliness) usafi ni muhimu.
We ilo li nchi ninka watu ma zwazwa yaan hawajui hata kufanya cause -effect, if -then argument waache walinde corona
 
Hawa wapuuzi walikua wakimchafua sana Magufuli na watanzania, leo bila kujijua wanamsafisha na kumpamba, kweli dunia duara

Unaemtukana leo, kesho utatumia nguvu hizo hizo kumsujudia
The false of today is the truth of tomorrow,
 
Tunaishukuru intelejensia ya Tanzania.
Waliicheza vyema kete ya korona.
Mpaka leo naamini kwa Afrika Mashariki Tanzania tunajielewa kiusalama zaidi( korona ni ajenda ya siri kubwa tofauti na watu tunavyoichukulia na kuisikia)

Wakenya hamna tatizo tatizo lipo kwa viongozi wenu wanawatumia kama madaraja kwa masilahi yao na wazungu kunyonya rasilimali zenu kwa ajenda ya korona!

mwisho: Tuipende Afrika kwa maendeleo ya kizazi chetu kijacho.
 
Back
Top Bottom