Hivi ni ukoo wetu tu tuko hivi au na wengine mna experience upuuzi kama huu?

Ukoo umeenda mbali, wengine tukikusimulia ya ndani ya familia ya ndugu wa tumbo moja, wazazi kupendelea waovu na kuungana nao kuhujumu wengine wanaoonekana "wanajidai wako vizuri" hutakaa uamini. Tenda wema uende zako.
 
Dunia ina mambo sana hii!
 
Ndo maana sisi wajanja tumeshaligundua hilo tunasaidia ukweni zaidi kuliko kwetu
 
Miaka kadhaa iliyopita ndugu yetu katika ukoo alipata ajali mbaya ya barabarani na ilihitajika matibabu ya dharura lakini yenye umakini, na kama mnavyojua matibabu ya umakini kwa nchi hii ni yakulipia. Ndugu tulikusanyana ili kila mtu aweze kutoa mchango wake kufanikisha matibabu hayo.

Michango ilikua ya kusuasua sana, na kwakweli kasi ya utolewaji wake ilikua hailingani na mahitaji ya udharura ya mgonjwa, kwani baada ya muda mrefu wa kikao na kuhamasishana bado hela zilizopatikana zilikua kidogo na zisingeweza kufanya mgonjwa apelekwe theater.

Nilipoona mambo yako hivyo na hisia za maumivu anazopata mgonjwa nikaanza kujitolea kutangaza kuchangia kiasi kikubwa, baada ya sekunde chache nikaungwa mkono na ndugu wengine watatu waliochangia kiasi kikubwa na baada ya muda mfupi pesa ya matibabu ikapatika.

Siku ileile nikapata wito kutoka kwa mama yangu mzazi kua kesho yake niende kwake ananiita, na mimi nikaamua kwenda siku ileile bila kusubiri kesho. Nilipofika alinionya sana kwa kitendo nilichofanya cha 'kutangaza' kutoa pesa vile mbele ya kikao japo kilikua cha wanandugu. Akanambia watu sio wazuri mwanangu japo ni ukoo wenu, na maneno meengi ambayo niliona kama maneno ya kizee tu. Risala ilikua ndefu na yenye kunisisitiza lakini mimi nilimsikiliza Bi mkubwa kama ada tu huku yakiingia sikio moja na kutokea jingine

Wiki moja baadae nilishangaa baada ya kukutana hospitali(mgonjwa alikua kashafanyiwa oparation) na mmoja kati ya wale ndugu waliotoa mchango mkubwa, akaniambia baba yake hakufurahishwa na kitendo cha yeye kujitolea 'hadharani' kutoa mchango. Akamwambia bora angefanya siri au angelipa moja kwa moja hospitali kimyakimya. Japo sikumwambia kua na mimi nilikabiliwa na hali kama yake lakini wote tukakubaliana kua wazazi wanazeeka na visheria vyao ambavyo havisaidii jamii.

Miezi kama kumi na nane baadae nilipatwa na mshituko. Nilikua naongea na dada yangu binamu ambae alinimwagia maelezo meengi kuhusu tukio lile la kuchanga siku ile. Eti watu hawakulipokea vizuri japo walijifanya wameshangilia tulipokua tumetangaza michango yetu. Dada binamu akaanza kunitajia kwa majina ndugu ambao wanauwezo kuliko hata sisi tuliotoa michango mikubwa lakini kila mmoja alikua anasubiri atoe kiasi kilekile ambacho watu wote watapangiwa kutoa! Akanihadithia na maneno watu waliyokua wanayasema pembeni na baada ya kikao eti tunajifanya tunaazo na mengine mengi ya kebehi na kuvunja moyo sana!

Kipindi kirefu kilikua kimepita toka mchango ule na yale mazungumzo na dada binamu lakini kwakweli niliumia sana kwa maneno yale na nikiri yaliniathiri sana na yalinibadilisha kabisa mtazamo na approach yangu kwenye shughuli za kifamilia. Nilikua nahisi watu hawaoni mahitaji ya watu kwenye ukoo lakini unashangaa huyo unaedhani anauhitaji badala akufuata umpe ramani za michongo ya town yeye anakusema unapofanya kitu positive! Najiuliza hivi ni ukoo wetu tu ndio tuko hivyo au ndugu zangu nanyie mshawahi ku experince kitu kama hicho?
Tenda wema uende zako
 
Mie naona yote sawa, hujaosea ila mzazi wako yupo sahihi, binafsi katika mambo kama hayo huwa napenda kutoa kile tulichoamriwa tutoe kwa pamoja halaf baada ya hapo ndio nitamfata muweka hazina, nimueleze katika kile kinachodaiwa mie nitatoa kiasi fulani ila asitangaze kuwa nimetoa mie, maana tumefundishwa tukitoa msaada tutoe kwa kificho kias kwamba kama umetoa na mkono wa kulia basi hata mkono wa kushoto usijue nadhani hili allah aliweka mahsusi kwakuwa anatujua viumbe wake, wengine wana chuki, husda, choyo na kadhalika...

Ila jambo zuri ni kuwa umetoa kwa nia ya msaada si maomesho ama sifa km watu wanavyojadili atakulipa mungu, next time usifanye hivyo chief, we chunguza kuna kipindi ukitaka kufanya jambo zuri kama likienea kwa kila mtu basi kuna asilimia kubwa ukafeli...
 
Miaka kadhaa iliyopita ndugu yetu katika ukoo alipata ajali mbaya ya barabarani na ilihitajika matibabu ya dharura lakini yenye umakini, na kama mnavyojua matibabu ya umakini kwa nchi hii ni yakulipia. Ndugu tulikusanyana ili kila mtu aweze kutoa mchango wake kufanikisha matibabu hayo.

Michango ilikua ya kusuasua sana, na kwakweli kasi ya utolewaji wake ilikua hailingani na mahitaji ya udharura ya mgonjwa, kwani baada ya muda mrefu wa kikao na kuhamasishana bado hela zilizopatikana zilikua kidogo na zisingeweza kufanya mgonjwa apelekwe theater.

Nilipoona mambo yako hivyo na hisia za maumivu anazopata mgonjwa nikaanza kujitolea kutangaza kuchangia kiasi kikubwa, baada ya sekunde chache nikaungwa mkono na ndugu wengine watatu waliochangia kiasi kikubwa na baada ya muda mfupi pesa ya matibabu ikapatika.

Siku ileile nikapata wito kutoka kwa mama yangu mzazi kua kesho yake niende kwake ananiita, na mimi nikaamua kwenda siku ileile bila kusubiri kesho. Nilipofika alinionya sana kwa kitendo nilichofanya cha 'kutangaza' kutoa pesa vile mbele ya kikao japo kilikua cha wanandugu. Akanambia watu sio wazuri mwanangu japo ni ukoo wenu, na maneno meengi ambayo niliona kama maneno ya kizee tu. Risala ilikua ndefu na yenye kunisisitiza lakini mimi nilimsikiliza Bi mkubwa kama ada tu huku yakiingia sikio moja na kutokea jingine

Wiki moja baadae nilishangaa baada ya kukutana hospitali(mgonjwa alikua kashafanyiwa oparation) na mmoja kati ya wale ndugu waliotoa mchango mkubwa, akaniambia baba yake hakufurahishwa na kitendo cha yeye kujitolea 'hadharani' kutoa mchango. Akamwambia bora angefanya siri au angelipa moja kwa moja hospitali kimyakimya. Japo sikumwambia kua na mimi nilikabiliwa na hali kama yake lakini wote tukakubaliana kua wazazi wanazeeka na visheria vyao ambavyo havisaidii jamii.

Miezi kama kumi na nane baadae nilipatwa na mshituko. Nilikua naongea na dada yangu binamu ambae alinimwagia maelezo meengi kuhusu tukio lile la kuchanga siku ile. Eti watu hawakulipokea vizuri japo walijifanya wameshangilia tulipokua tumetangaza michango yetu. Dada binamu akaanza kunitajia kwa majina ndugu ambao wanauwezo kuliko hata sisi tuliotoa michango mikubwa lakini kila mmoja alikua anasubiri atoe kiasi kilekile ambacho watu wote watapangiwa kutoa! Akanihadithia na maneno watu waliyokua wanayasema pembeni na baada ya kikao eti tunajifanya tunaazo na mengine mengi ya kebehi na kuvunja moyo sana!

Kipindi kirefu kilikua kimepita toka mchango ule na yale mazungumzo na dada binamu lakini kwakweli niliumia sana kwa maneno yale na nikiri yaliniathiri sana na yalinibadilisha kabisa mtazamo na approach yangu kwenye shughuli za kifamilia. Nilikua nahisi watu hawaoni mahitaji ya watu kwenye ukoo lakini unashangaa huyo unaedhani anauhitaji badala akufuata umpe ramani za michongo ya town yeye anakusema unapofanya kitu positive! Najiuliza hivi ni ukoo wetu tu ndio tuko hivyo au ndugu zangu nanyie mshawahi ku experince kitu kama hicho?
Ombeni mfunge kuondoa hiyo laana.Unaweza ukawa tajiri lakini ukawa mfungwa ktk mambo muhimu kiasi kwamba huna uhuru hata na mali zako.Anahitajika mtu asimame kuwaokoa ninyi ktk giza hilo.Kataeni muanze kutoka ktk wimbi hilo muifikie nchi ya ahadi.Zoezi la kutoka si lelemama.Inahitajika uvumilivu pia usiwe na hasira.
Hayo yapo kwenu tu mkuu.
 
Dah sawa mkuu
 
Sesten Zakazaka

Nimegundua kunamatatizo mengi katika jamii zetu kwenye mambo kama haya.

1. Watu wana ubinafsi sana.Mtu anaumwa, inawezekana akafa, mchangounahitajika, watu wanajisuasua wakatihela wanzo, etikisa wasitoe zaidi ya wengine.

2. Watu wana kutegeana sana. Kila mtu anamuangalia mwenzake atoe.

3. Watu wana unafiki sana. Ukitoa kwa siri watakuambia toa wazi watu wajue,uhamasishe. Ukitoa wzi watakuambia toa kwa siri, si vizuri kujionesha.

4. Watu wana kijicho sana. Ukitoa kiasi kikubwa wanaona wivu kwa nini umetoa.

5. Watu wana dharau sana. Usipotoa kiasikikubwa wanakudharau kwamba umefulia.

Kwa hiyo wewe toa tu akili zako zitakavyoona sawa.
 
Wivu wa kimaendelea na kupenda misifa isiyokuwa na maana kwa koo nyingi ni tatizo kubwa sana rafiki na m2 mwingine baki ni bora kuliko ndugu wanafiki sana
 
Back
Top Bottom