Hivi ni Malipo yapi yalilipwa Tz bila malalamiko?

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205

Sina uhakika na yale ya shanga ya wakati wa Mangungu.

1. Labda nianzie ya wastaafu wa EAC(1977:-() leo ni zaidi ya miaka 34 bado wazee hawa wanalala barabarani kushinikiza malipo yao - tunaambiwa wenzao wa nchi nyingine wamelipwa siku nyingi zilizopita.

2. Fidia za upanuzi wa barabara, viwanja vya ndege n.k. Lazima usikie malalamiko yasiyoisha..

3. Wahanga wa mabomu ya Mbagala -ndiko haswa shida ziliko. Wakati serikali inafunga/hitimisha, wahanga wanasema mambo bado mabichi.

4. Nakumbuka waliopisha wawekezaji Kibamba na kwingineko. Kesi hazijaisha..

5. Pensheni za huko NSSF na PPF usiseme…malalamiko hayaishi

6. Karibuni tumesikia makaburi ya Kiyeuyeu tuliambiwa wamelipwa 5m lakini wenyewe wanasema bado -vipi?

HEBU TUTAFAKARI SHIDA NI NINI?

Hivi kwa nini malipo yatusumbue sisi watanzania tu?

Wapi tumepinda????

:thinking:
 
Back
Top Bottom