Hivi ni Kweli?

kamanzi

Senior Member
Oct 28, 2007
100
23
Jamaa yangu wa karibu alie Arusha ananiambia kwamba viongozi wengi wa CCM na serikali wameshafika kwa babu wa Loliondo kupata matibabu. Naambiwa hata mkwere na baadhi ya mawaziri wake wameshapatiwa huduma na babu na ndio maana baada ya tangazo la waziri wa afya kukataza matibabu ya babu, mkuu wa mkoa wa Arusha alisema haiwezekani kukatisha huduma. Hivi inawezekana haiwezekani kwasababu hata mkwere anaamini kikombe cha babu kitarefusha maisha yake? NAsikia hata mfipa nae si mzima, yawezekana wamekubali yaishe na kujisalimisha kwa babu Ambilikile? Hata babu alikaririwa na magazeti mengi akisema vigogo wanaenda kwake kwa siri. Wenye data, tafadhali wekeni wazi orodha ya vigogo hawa wanaojipatia huduma ya shillingi 500.
 
Soma magazeti ndugu mbona list zipo waziwazi tuu...Kumbuka mficha uchi azai na wengi wao wamejitaja na kuipongeza dawa ya babu ila kakobe anamwombea babu ashindwe katika jina la Yesu kwani kalimaliza kanisa lake...waumini wamehamia loliondo...!Mi nadhani Kakobe ndio ashindwe na kulegea kwa jina la Yesu na arudishe dhahabu za waumini wake alizozikusanya nazifanya utajiri wake.
 
Jamaa yangu wa karibu alie Arusha ananiambia kwamba viongozi wengi wa CCM na serikali wameshafika kwa babu wa Loliondo kupata matibabu. Naambiwa hata mkwere na baadhi ya mawaziri wake wameshapatiwa huduma na babu na ndio maana baada ya tangazo la waziri wa afya kukataza matibabu ya babu, mkuu wa mkoa wa Arusha alisema haiwezekani kukatisha huduma. Hivi inawezekana haiwezekani kwasababu hata mkwere anaamini kikombe cha babu kitarefusha maisha yake? NAsikia hata mfipa nae si mzima, yawezekana wamekubali yaishe na kujisalimisha kwa babu Ambilikile? Hata babu alikaririwa na magazeti mengi akisema vigogo wanaenda kwake kwa siri. Wenye data, tafadhali wekeni wazi orodha ya vigogo hawa wanaojipatia huduma ya shillingi 500.

kwani viongozi wa ccm ndo awastail kuumwa???na kama wanaumwa kwanini wasiende kupata dawa?we vp!
 
Kwenda kwa babu kusiwe issue jamani, ni tiba kule na wala si kwenda kuloga. Tusiwadhihaki Watanzania wenzetu wengi wanaokwenda kule kwa ajili ya matibabu, tuwaonee huruma na kuwasaidia pale inapobidi. Mtu yeyote yule anaweza pata shida ya maradhi ambayo yakamlazimu hata kwenda kwa babu katika kuinusuru afya yake.
 
Kuna jirani yangu alikunywa J2 iliyopita na alinihakikishia kuwa aliwana first lady na Magufuri kwa macho yake wakinywa baada ya kufika kwa helcopter na akanambia JK ataenda trh 25 mwezi huu!
 
mhhhhh watanzania wengi watapona.Kakobe ni msanii jamani naona mambo yake ya Nigeria yamefifia kapoteza waamini kibao anaganga njaa.Angekuwa kweli anaponya watu kwa nguvy ya Mungu asingemdhihaki mchungaji babu kwa vile nae anaponya kwa nguvu za Mungu.hapo kuna jambo na nimeelewa nguvu halisi za Kakobe..kapoteza sadaka zake nne nk.BIg up sana wachungaji wa KKKT kwa kuunga mkono na kukiri kunywa kikombe mkapona.
 
Back
Top Bottom