Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,510
- 28,417
Binafsi nafikiri hakuna sheria inayoamua juu ya hili...ila usipotegemea LOWASSA anaweza kuvunja hu utaratibu....
Jibu rahisi ni kwamba, waziri mkuu huchaguliwa na mtu mmoja (rais) na wengi huchagua yule anedhani anafanana nae kimtazamo, wakati rais wa nchi huchaguliwa na watu wengi(wnanchi) na wnanch wanapenda mabadiliko kwani uzoefu unaonyesha kila rais ansetoka madarakani huwa na mapungufu mengi hivyo kuhitaji mtu mpya wa kusahihisha na sio kuleta sura inayofanana kiutendaji na raisi aliyekuwepo madarakani.
Kwa mfao, huyo Lowassa unayemsema hawezi kuwa chaguo la wengi kutokana na kashfa zinazomkabili alipokuwa Waziri Mkuu wa Jk.
Ukiachilia Nyerere, hakuna waziri mkuu mwingine wa Tanzania ambae alifanikiwa kuja kuwa Rais wa nchi, kwa mfano Kawawa, Msuya, Salim, Warioba, Malecela, Sumaye, Sokoine, na kuna kila dalili kwamba at least kwa uchaguzi mkuu ujao 2015, CCM haitamsimamisha mgombea Urais kutokana na Mawaziri wakuu waliopita.
Sababu ya hili ni nini - je ni mpango maalum (kama vile unwritten principle) au huwa inatokea tu?
Sababu ya hili ni nini - je ni mpango maalum (kama vile unwritten principle) ......?
hahahahaa kama aliweza kulia machozi bungeni, IKULU SI ATAENDA KUOMBOLEZAThe weakest PM in the history of this country.
Kilichotokea ni kwamba licha ya juhudi za Kambarage za kumweka Salim kama mgombea mwaka 1985, forces za CCM zilimshinda Mwalimu, hasa upande wa Zanzibar. Mwaka 1995 ndio alikataa wazo la kujaribiwa tena. Tunamsema sana mwalimu kwamba alikuwa dictator na mambo kama hayo lakini tunasahau kwamba Mwalimu hakuwa mtu wa kulazimisha kila jambo, vinginevyo viongozi waliomfuatia wangekuwa na fursa katika nyakazi zile za Nyerere, hakuna ambae angewazuia kuweka mtu wao.Mkuu mbona Salim alishurutishwa mara mbili na Kambarage, lakini aka-decline offer - wengine siwezi kuwazungumzia.
Nadhani kuna watanzania wengi wenye uwezo wanaoweza kuwa marais na si lazima mawaziri wakuu wa zamani. Simpo. Hakuna anayewazuia kama Nyerere hakuzuiliwa kwanini wao?
Unazungumziaje mawaziri wakuu wengi kuwa wakristo huku muislam akiwa wachache kama Rashid?
Ngoja na mimi nitoe mawazo yangu. Sababu ya kwanini mawaziri wakuu huwa hawa pewagi nafasi ya kupeperusha bendera ya chama kwenye chaguzi za uraisi ni kwa sababu mtu ukisha kuwa waziri mkuu tayari wapinzani wako wana assume utautafuta uraisi kwa hiyo wanajiandaa mapema. Kwa maana hiyo usikute hata sasa kuna watu washa jiandaa kupambana na Pinda iwapo ata gombea. Hii inatokana na mentality ya sisi wanadamu kuwa mtu akisha pata nafasi fulani hutaka cha juu zaidi na kwetu baada ya uwaziri mkuu ni uraisi (husikii mtu akililia au kugombania umakamo wa raisi kwa sababu ni nafasi isiyo na nguvu nyingi). Hii inamaana hata leo hii ikatokea bahati bin vuu mlala hoi kama mimi akateuliwa kuwa waziri mkuu tayari maadui au wataka uraisi wata assume moja kwa moja na mimi nitausaka uraisi. Hii nadharia si bure kwani mpaka sasa historia inaonyesha kila alieukwaa uwaziri mkuu kaishia kuutafuta uraisi (ukimuacha Kawawa na pia Sokoine aliefariki dunia kabla ya kupitia chaguzi kuu yoyote).
Kweli wewe mende0! Hilo la udini wako unalileta baada ya kuishiwa hoja. Nadhani kuna haja ya kujadili issues badala ya personalities otherwise kujadili watu kunawafaa wenye akili ndogo na mtindio wa mawazo so to speak. Jaribu kutumia ubongo kidogo uangalie hoja inataka nini. Kama una hoja ya udini peleka huko inakofaa lakini si hapa. Maisha mabaya ya watanzania hayaangalii dini. Ni kipofu na taahira anaweza kuunganisha hoja hii na udini. Pia ni muhimu kuficha ujuha kuliko kuuanika. Ni ushauri tu.
kwa hiyo umekubali mfumo kristo unafaa kutawala dunia nzima?