Hivi ni Dowans peke yake au......................?

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,304
Mtu yeyote akitaja neno Dowans basi waliopo karibu watakunja nyuso zao na kusema kila aina ya ubaya kwa kampuni ya dowans. Nafahamu kuwa mchakato wake haukuwa wa wazi lakini swali je hayo makampuni mengine ya kufua umeme kama IPTL, SONGAS na mengineyo yalifuata taratibu zote za kisheria bila kuhusisha ruswa kwenye mikataba yao na Tanesco? Ikiwa hivyo basi tuna haki ya kuisakama Dowans na wale wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine na Dowans. Lakini ikiwa makampuni mengine yaliyosalia ukiitowa Dowans pia na yenyewe yamejaa usanii na mikataba yake haikuwa na tija na iliingiwa kwa hila basi sisi "Watanzania" ni wanafiki! Wanafiki na tuna sababu za nyuma ya pazia kuisakama Dowans!

Kuna habari nimepata kuzisikia kuwa Dowans ndio kampuni pekee inayochaji "capacity charges" kuliko makampuni mengine Dowans wanalipwa 152 mil per day, Songas over 250 mil per day na IPTL kwenye 300 mil per day.

Nadhani imefika wakati tujaribu kutafuta ukweli na kuyachambua makampuni yote yanayofua umeme tusiwe waitikia kiitikio "kolasi" na pili tuache unafiki kama kuna makampuni zaidi ya moja yanayohusika na hila basi yakemewe yote kwa nguvu zote yasishambuliwe makampuni baadhi kwa sababu ya hila na chuki binafsi huku mengine yakiendelea kutunyonya.


Kabla ya kuwakilisha na kukaribisha hoja napenda kukoselewa na kuelimishwa hayo ni maoni yangu binafsi na figures nilizotoa ni just round figures sina source ikiwa kuna mtu ana source itakuwa kafanya jambo la maana akituletea source ya charges zinazolipwa na Tanesco kwa makampuni husika.

Nawakilisha.....
 
Great Thinkers naomba tupasue mbongo zetu I smell something fishy here..................
 
Great Thinkers naomba tupasue mbongo zetu I smell something fishy here..................
Mdau, kwa ujumla mikataba yote ya kufua umeme ni ya kifisadi na ina lengo la ku-siphon pesa za walipa kodi kupitia TANESCO. Kama wanazo pesa za kulipa hizo "capacity charges", yaani malipo bila ya kuzalisha umeme, kwa nini wasiipe TANESCO ikanunua mitambo na kuiendesha yenyewe na kukwepa hizo capacity charge. Ufisadi TANESCO ulianza zamani katika enzi ya Mwinyi ilipoletwa IPTL (JK akiwa Waziri wa Nishati), akaja Mkapa na Makaburu wake wa sijui Solution what?, na JK anaendeleza libeneke na Richmond/Dowans. TANESCO ni mateka wa mafisadi.
 
Mdau, kwa ujumla mikataba yote ya kufua umeme ni ya kifisadi na ina lengo la ku-siphon pesa za walipa kodi kupitia TANESCO. Kama wanazo pesa za kulipa hizo "capacity charges", yaani malipo bila ya kuzalisha umeme, kwa nini wasiipe TANESCO ikanunua mitambo na kuiendesha yenyewe na kukwepa hizo capacity charge. Ufisadi TANESCO ulianza zamani katika enzi ya Mwinyi ilipoletwa IPTL (JK akiwa Waziri wa Nishati), akaja Mkapa na Makaburu wake wa sijui Solution what?, na JK anaendeleza libeneke na Richmond/Dowans. TANESCO ni mateka wa mafisadi.

Swali langu mkuu ni kwanini Dowans na si IPTL na kina SONGAS? yaani sipati jibu kuna taarifa ya kamati ya bunge kusikitishwa/kushituka kusikia capacity charges zinazolipwa na Tanesco kwa Songas lakini ile issue iliisha "jukwaju"

""You pay 6bn/- whether you buy their electricity or not, this is a lot of money, if you can buy Songas it means there will be no capacity charges and you will make a lot of money," Mr Serukamba said, supported by others. Tanesco's Acting Managing Director, Mr Steven Mabada told the MPs that the high capacity charges by Songas, which ends after 20 years were a result of previous contracts and that Tanesco's hands were tied. The MPs also queried why Songas claimed that it has been making a loss but was ready to continue with the contract for the next 20 years and asked Tanesco who are also shareholders in Songas whether they were aware of what was going on in the gas company. Tanesco's Board Chairman Mr Peter Ngumbulu said because they were shareholders, they were represented by Chief Finance Officer in the Songas board meetings but they were not sure exactly whether it was true that Songas has been making losses all along.

Songas generates 180 megawatts (MW) of power for Tanesco which is approximately 30 per cent of Tanzania's electricity needs." Source: MPs shocked

Ukija kwenye IPTL ni hayo hayo swali kwanini Dowans peke yao? kama kuwalipua nadhani tungeanza na wa awali au tunaanza wa misho wakati mpaka kumfikia wa kwanza? Nahisi kuna kitu si bure....
 
Back
Top Bottom