Hivi ni biashara ipi kati ya hizi ambayo inatembea vizuri?

Bar uhakika watu wanalewa sana ....weka nakitimoto,nyama ya mbuzi,michemusho weka na mademu wakali mwezi mmoja tu ....utakuwa mbali sana
 
Usifanye biashara hizo ukitegemea faida haraka, tegemea pia hasara, na usitarajie itakulipa kwa kumpatia mtu mwingine asimamie sahau hilo, komaa mwenyewe, angalia jamii inayokuzunguka haina au haipati huduma gani kwa urahisi halafu angalia washindani wako wanafanyaje na wewe boresha zaidi, hakikisha kauli kwa wateja na siku zote kubali kujifunza, halafu utakutana na hasara hakikisha haukati tamaa angalia hasara imesababishwa na nini halafu wewe boresha
 
Angalia eneo ulipo kwa sasa chakula ni kipaumbele kwa wengi, fungua duka la vyakula mfano uuze mchele, ngano, maharagwe, kunde, njegere, unga( sembe na dona) , dagaa kauzu, mafuta ya kupikia ( alizeti, korie, safi, ) hapo unaweka na ya kupima hapa kwenye hii project komaa mwenyewe
 
Halafu angalia sehemu yenye salon za kike na kiume hilo eneo liwe na mwingiliano mkubwa tafuta binti mwenye mwonekano fungua duka lenye vitu vifuatavyo ( Chonga kabati ya alminium humo utaweka sabuni wanazopenda wanawake kuogea na kunawia usoni, body spray za akina dada, deodorant, lotion aina tofauti kiasi, cheni za shingoni, bracelets, saa za bei ndogo tu za ke na me, vikuku, shanga za wanawake) kwenye kabati umemaliza sasa utakuja kwenye shelves hakikisha unaweza pedi kama HC, softcare, pampas za watoto na pampas za watu wazima, ped kama always, halafu utakua na hanger uweke chupi aina mbalimbali za kike, boxa za kiume aina mbalimbali, brazia za wanawake size mbalimbali, weka pia vest za kiume mode mbalimbali, weka soksi aina mbali mbali, halafu maliza na tigo pesa na m pesa na airtelmoney, usisahau kuweka rasta aiana mbalimbali, hakikisha unauza kwa bei ya kawaida ili uwe kwenye mzunguko, biashara hii haifai uwe kijijini inafaa maeneo yenye watu hasa idadi kubwa wawe wapo vijana wa kike na kiume masister duu na mabrazamen, utaona maajabu
 
Back
Top Bottom