Hivi ndivyo unavyoweza kusoma Taarifa za Fedha na Kuanza Uwekezaji katika Soko la Hisa (Masoko ya Mitaji)

Emmanuel55

Member
Sep 27, 2016
6
11
Habari ndugu msomaji wa mtandau huu, karibu katika mfululizo wa makala zetu za kukuelimisha katika nyanja ya uwekezaji katika hisa. Leo ningependa kuzungumzia kuhusu namna na urahisi wa kusoma taarifa za fedha za Kampuni ambazo zimesajiliwa katika soko la hisa. Vile vile somo hili la leo litakusaidia kusoma taarifa za fedha za kampuni mbalimbali ambazo zipo katika soko la hisa na hata ambazo hazipo katika soko la hisa.

Taarifa za fedha za Kampuni ni muhimu katika kutoa mwanga kwa wawekezaji ili kutambua kampuni ambayo inafanya vizur na kampuni ambayo inafanya vibaya. Taarifa hizi hutolewa mara mbili kwa mwaka yaani kila baada ya miezi sita au kila baada mwaka mmoja kwa baadhi ya Kampuni na baadhi ya kampuni hutoa taarifa mara nne kwa mwaka (kila robo ya mwaka). Taarifa za fedha ni muhimu kwa mwekezaji kwa kuwa inamsaidia kujua Kampuni imepata faida kiasi gani, mauzo ya Kampuni, Madeni ya Kampuni n.k

Makala hii imekuja kwa ajili ya kutoa somo kwa uchache ili mwekezaji uweze kusoma taarifa za fedha za Kampuni ambayo unatarajia kuwekeza katika soko la hisa. Taarifa hizi zote uandaliwa kwa lugha ya Kingereza na kutumia misamiati ya kifedha na kuwa vigumu kwa baadhi ya watu kuzisoma na kuzielewa. Basi kupitia njia hii utaweza kusoma na kuelewa sehemu za taarifa muhimu ambazo zitakusaidia katika kufanya maamuzi sahihi ya uwekezaji wako.

Lengo langu ndugu msomaji na wewe mwekazaji ni kuweza kusoma taarifa za fedha za kampuni ili kuweza kufahamu kwa uchache kuhusu mwenendo wa kampuni ambazo zipo katika soko la hisa na kujua uwezo wao katika ufanyaji kazi. Na tutaangalia taarifa mbili za fedha nazo ni financial statement na statement of financial position.

Ni muhimu kufahamu baadhi ya maneno muhimu ambayo yanaelezea taarifa za fedha za Kampuni ili iwe rahisi kupata mwanga wakati wa usomaji wa taarifa za fedha za Kampuni.

Tuanze kwa kuangalia kwa taarifa za fedha ambazo zinaonyesha ikiwa Kampuni itakuwa imepata faida au hasara ( Statement of Profit and Loss).

Revenue/Sales
= Mauzo au mapato ya kampuni baada ya kuuza bidhaa au huduma ambayo kampuni inatoa. Katika taarifa za fedha huonyesha mauzo ya miaka miwili, ni muhimu kwako kulingnisha mauzo ya miaka miwili ikiwa yaneongezeka au yanapungua. Na katika kulinganisha utajua kwa kiasi kiasi cha mauzo kineongezeka au kupungua. Na kuweza kutambua kampuni imefanya vizuri kwenye mauzo kwa mwaka husika ukilinganisha na mwaka uliopita.

Cost of good Sold/Operating expense= Hii ni gharama ya bidhaa ambazo kampuni imeuza au gharama za uendeshaji wa shughuli za Kampuni. Kama mwekezaji ni vizuri ukalinganisha gharama za uzalishaji wa kampuni husika kwa kipindi cha nyuma na kipindi cha sasa. Ikiwa gharama zinaongezeka ni muhimu kuangalia ikiwa na mauzo pia yameongezeka au ikiwa Kampuni imefanya aina yoyote ya uwekezaji katika biashara ambao umeongezeka gharama.

Operating profit/Profit before tax and interest= Hii ni faida ghafi yaani faida ya kampuni kabla ya makato ya kodi na riba ya mkopo. Je faida ghafi ya mwaka husika ni kubwa au ndogo ukilinganisha mwaka uliopita. Na kama faida mwaka husika imeongezeka ukilinganisha na mwaka uliopita, basi ni ishara nzuri katika ukuaji wa kampuni.

Profit after tax and interest/Net Income= Faida ya Kampuni baada ya makato ya Kodi na riba. Hii ni faida baada ya kutoa kodi ya serikali pamoja na gharama za mikopo ya kampuni katika uendeshaji. Je faida imeongezeka ukilinganisha na mwaka uliopita? Je gharama za mikopo zimeleta athari katika ukuaji wa faida ya kampuni. Muhimu kufahamu kama faida imeongezeka ukilnganisha na mwaka mpya, kwa sababu sehemu ya faida hii ndio itaenda kwa wanahisa kama gawio katika kipindi cha mwisho wa mwaka au katika kipindi cha miezi sita.

Earnings per share
Hiki ni kiasi ambacho kimepatikana toka kwa kampuni baada ya kutoa gharama zote na kulipa kodi. Ili upate earnings per share utachukua faida ya kampuni utagawanya na idadi ya hisa zote ambazo kampuni inamilikiwa. Kiasi hiki kikiwa kikubwa inamaanisha na gawio linaweza kuwa kubwa. Kwa maana rahisi kila hisa moja imeweza kutengeneza faida ya shilingi ngapi.

Dividend per share
Ni gawio la faida ambayo imetokana na uzalishaji wa Kampuni husika. Na gawio hutolewa ikiwa Kampuni itakuwa imepata faida na wanahisa wamepitisha kiasi cha gawio kwa kika hisa moja. Na gawio hupatikana kwa kugawa kiasi cha faida ambayo imeidhinishwa kutolewa kwa wanahisa na idadi ya hisa amabazo zinamilikwa na wanahisa.

Sehemu ya Pili tutaangalia kuhusu Hali halisi ya Kampuni katika uendeshaji wake hasa Katika Mali, Madeni na uwezo wa kujiendesha katika Mtaji. ( Statement of Financial Position )

Assets
Hii inahusisha mali zote ambazo Kampuni inamiliki pamoja na Mashine na Vifaa vyote ambavyo Kampuni inamiliki vile vile kiasi cha Fedha ambacho inamiliki pamoja bidhaa zilizo stoo ikiwa Kampuni inajihusisha na Uzalishaji.

Current Assets
Hapa tunaangalia mali ambazo Kampuni inamiliki, ambazo zipo katika mfumo wa fedha au ni rahisi kuzibadili kuwa fedha. Mali hizi zinajumuisha fedha ambazo zipo benki, malighafi za kampuni ambazo zipo stoo, na bidhaa ambazo zimezalishwa zipo stoo.

Fixed Assets
Hiz ni mali za Kampuni ambazo hazihamishiki kwa rahisi ambazo Kampuni husika zinamiliki kwa mfano Mashine, Majengo n.k. Ikiwa kampuni imamiliki majengo, mitambo ya uzalishaji au kitu chocho kisichohamishika hivyo vyote ni sehemu ya mali za kampuni.

Equity
Hii inaonyesh Mali/Mtaji wa Kuendeshea Kampuni ambao unatokana na wamiliki au wanahisa wa Kampuni. Mtaji huu mara zote unatakiwa kuwa mkubwa kuliko Mtaji unaotokana na Mikopo ya Kampuni. Na hii kama mwekezaji inakusaidia kujua kwa kiasi gani Mtaji wa Kampuni unatokana na Fedha za wawekezaji na Sio mikopo. Na ikiwa sehemu kubwa ya mtaji inatokana na fedha za wawekezaji ni ishara nzuri katika ukuaji wa Kampuni.

Liabilities
Katika taarifa fedha hii inaonyesha madeni ambayo Kampuni inamiliki kama madeni ya muda mfupi na madeni na muda mrefu. Kama mwekezaji inatakiwa kutambua kwa kiasi gani Kampuni inamiliki madeni ya muda mrefu na muda mfupi. Je madeni haya ni zaidi ya mali ambazo Kampuni inamiliki na yanaweza kuleta athari katika utendaji wa Kampuni na kuathiri faida ya Kampuni.

Current liabilities
Haya ni madeni ya muda mfupi ambayo kampuni inayamiliki na ambayo yanatakiwa kulipwa katika kipindi cha muda mfupi. Madeni haya yanahusisha malighafi zilizonunuliwa kwa mkopo au mikopo ya kampuni ambayo inatakiwa kulipwa ndani muda mfupi.

Long term liabilities
Haya ni madeni ambayo ni ya muda mrefu, kwa katika kipindi cha muda mrefu kampuni itakuwa katika mpango wa kuendelea kuyalipa. Madeni haya yanaweza kuwa mikopo mikubwa katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kampuni.

Nikutakie wakati mwema, na kukaribisha kuendelea kujifunza zaidi kupitia makala zangu
 
Kama unahitaji ufafanuzi zaidi tiririka sehemu ya comment hakikisha unabofya vote kupigia kura chapisho hili
 
This nmeipenda mnooo kwan niko kweny hatu a ya awali ya kusoma zaid maana ya hisa kabla sijaanza kuwekeza nashukulu san kwa hii taarfa ndugu nakuomba utoapo taarfka nyingne pls Fanya namna nijue nko tayal kujifunza hata km unaandaa semina or kun wasap group niko tayal
 
Back
Top Bottom