Hivi ndivyo jinsi majirani zetu wanavyotuongelea kuhusu Corona

Spain walilia wakisema “ wakati gonjwa lipo kwa jirani zetu Italy tulijua ni ngumu kufika kwetu” ila leo ndani ya saa 24 wameripoti vifo 700+

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kwahiyo tunaweza kusema kwamba pamoja na ujuzi na uelewa wa hao wenzetu ila walifanya ujinga? maana Spain ni hivyo hivyo na marekani ni hivyo hivyo.
 
Eburu Presenter: Kauli ya Rais kuwa tuchape kazi, corona ni kitu cha kawaida, Mungu atatuongoza. Kauli ya Rais Magufuli imestua hata Shirika la Afya Duniani. Tanzania ni majirani zetu, ugonjwa ukisambaa Tanzania Kenya hatuwezi kuukwepa.

Ki historia Tanzania ni kama nchi inayoongozwa na Mwalimu Mkuu ambae anafanya maamuzi yote. Kwakufupi Magufuli anatuambia fanyeni yenu na mimi ninapiga mziki nikiwa ninafanya yangu. Lakini haya yataishia kwenye kilio.

Hata kama tunamtegemea Mungu tuwe na busara, huwezi kufanya maamuzi ya ovyo ukitegemea Mungu atakulinda.

View attachment 1405938
sisi watanzania hatuna chochote cha kujifunza kutoka kenya si hiyo corona wala chochote, kwa mtindo ule wa askari kupiga watu hovyo ndo kupambana na corona? halafu mleta mada jitafakari.
 
Huko Dar Korona imeahatinga uswazi. Sijui mpaka sasa idadi ya maambukizi mpaka sasa itakuwa ngapi lakini ipo kwenye mia kadhaa au zaidi.

Endeleeni kujidanganya na kufanganyika na takwimu za umi mwalimu. Watanzania mmetelekezwa muwe kafara.
 
Kama kweli wanafanya kazi zao ipasavyo, walitakiwa watupe mapema alert kuhusu huu ugonjwa. Acha waungane na utopolo wenzao kujifungia ndani. Labda itawasaidia maana Italy na Spainna hata US haijabadili mambo.
Shirika la Afya Duniani inawezekana lisiwe na wataalamu wa afya,ila ipo hivi,mashirika mengi ya umoja wa mataifa huwa yanafeli.
 
Ninyi akina nani hamna taarifa? Unajua kinachokera, ni pale kudhani kila kitu lazima tuwe replica wa wengine; tena si kwa corona tuu bali kila jambo linalo amliwa na viongozi lazima mlibeze na kushadadia yale yanayoamliwa na nchi jirani. Serikali inyo mipango yake tumieni akili. Na nikuhakikishie, watu wa aina yako, katu, ushauri wenu hautokuja kusikilizwa kwa lolote. Kwa sasa mnatamani maambukizi yawe kama 100,000 mpate cha kusema, ila ujue hautashuhudia hiyo namba, ili ifikie, utakuwa ulishaondoka.

Mawazo ya kipuuzi kabisa.

Mambo kama haya hatarishi kwa watu hayawezi kufanywa tu kwa hisia za watu eti hawataki kuiga toka nchi zingine.

Huwezi kuhatarisha maisha ya raia zako kwa kujiona wewe unajua zaidi ya wengine wanaofuata taratibu ambazo zilishathibitishwa kisayansi.

Hakuna anayeombea waTanzania wakumbwe na janga kama hili, lakini mitizamo ya kishamba kama hii ni kukosa heshima za uongozi.
Kwako wewe unaona kukusanyika makanisani, misikitini na kwingineko ni sawa tu eti kwa vile hatutaki kuiga watu wengine? Hii ni akili ya namna gani.

Mungu atatulinda. Tutaekana na janga, ili mkidhi haja zenu za kujipa sifa kuwa 'mlijua' huu ugonjwa hauwezi kuwashambulia waTanzania.

Haya nyinyi mliyajulia wapi? Mnazo sayansi zenu za kipekee?

Bure Kabisa.
 
Uliyeleta post hii utakuwa kwenye siku zako umeshindwa kumpa burudani Mme wako
Si busara kumshambulia mleta post. Ameleta kitu kama kilivyo, hajaongeza neno.Shughulika na facts. Unaongelea masuala ya kimaumbile ambayo wewe mwenyewe, dada zako, mama yako wanapitia. Nashangaa Polepole kukulipa zuzu kama wewe. Kilangila.
 
Nawashangaa mnaomshambulia mleta mada. Aliyoandiika ndiyo yaliyosemwa. Sikilizeni hiyo clip kwanza. Kilangila.
Kenya Leo wamefika wagonjwa 81
Rwanda wamefika 70
Sisi 20
Sioni msaada wa lockdown hapo.
Halafu mleta mada acha ujinga,ulitaka Rais aseme watu wasifanye kazi wakae tu wanaisubiri corona?
Kwani korona inakuletea chakula nyumbani?
Italy watu wamefungiwa ndani kila siku wanakufa zaidi ya 800 sisi wapiga misele tumezika mmoja tu.
ia
 
Eburu Presenter: Kauli ya Rais kuwa tuchape kazi, corona ni kitu cha kawaida, Mungu atatuongoza. Kauli ya Rais Magufuli imestua hata Shirika la Afya Duniani. Tanzania ni majirani zetu, ugonjwa ukisambaa Tanzania Kenya hatuwezi kuukwepa.

Ki historia Tanzania ni kama nchi inayoongozwa na Mwalimu Mkuu ambae anafanya maamuzi yote. Kwakufupi Magufuli anatuambia fanyeni yenu na mimi ninapiga mziki nikiwa ninafanya yangu. Lakini haya yataishia kwenye kilio.

Hata kama tunamtegemea Mungu tuwe na busara, huwezi kufanya maamuzi ya ovyo ukitegemea Mungu atakulinda.

View attachment 1405938
Nasoma comment za wachangiaji kwakweli nachoka tu.
Watanzania sisi bado hatujaelewa hivi virus na huu ugonjwa.
Italy,Spain,America ni mataifa ambayo hayakua yameelewa hili tatizo kama tulivyo sisi watanzania na uongozi wetu.
China,Taiwan,Japan,Rwanda,Kenya na Uganda wameulewa ugonjwa huu mapema sana.
Sisi tutaelewa kwa mifano!!!
Wakati utafika tutajiweka lock down wenyewe bila amri ya mtu...Lkn wakati huo tutakua tumechelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila mtu atumie njia zake kupambana yaani washindwe kuwashangaa Italy na Spain ambao wamefungia watu ndani lakini daily wanazika watu 700+ waje kutushangaa Tanzania ambao tukifungiwa ndani tu kwa siku moja tunakufa kwa njaa wala sio corona.
Acha ku-justify ujinga wewe! Hao Italy na Spain walichukua hizo hatua wakati gani?! Yaani nchi imeshaarika vya kutosha ndo unajifanya kuchukua hatua ndo unadhani itasaidia?!

Nani amesahau Donald Trump alivyokuwa analeta mzaha wakati ugonjwa ulipolipuka kule China, Italy na Iran hadi majuzi tu kufikia kutangaza eti chloroquine inatibu korona!

Leo hii quarantine isipofanya kazi US ndo useme "mbona wameweka quarantine na bado wanakufa" wakati alianza kufanya mzaha tangia mwanzo!!

Ghala la mbegu unalifunga kwa makufuli manene manene na kuweka walinzi nje halafu useme mbona makufuli hayakusaidia panya wasile mbegu wakati uliwafungia na panya ghalani?!

Nchi zote ambazo zilifanya mzaha mwanzoni ndiyo zinaumia zaidi hivi sasa including hizo Italy na Spain! Labda kama hufahamu, hadi wakati Italy mambo yapo tete, Spain walikuwa wanaendelea kujazana viwanjani huku wakiamini Italy na Spain ni mbali sana!

Halafu hizi justification za kufa njaa ni justifacation za hovyo kabisa!!

Tanzania hadi kesho watu wanajazana misibani, kwenye maharusi, kwenye nyumba za ibada n.k! Unataka kusema kote huko watu wanaenda kutafuta pesa ya kula?!

Ukifika Ferry watu wanajazana kwenye minada ya samaki wakati majority si wanunuzi wala wachuuzi!!!

Hata kama si kwa coronavirus, ipo wakati Afrika itakuja kuangamia kutokana na ujinga wetu huku hata wale wenye uelewa wakiendelea ku-justify ujinga!
 
Eburu Presenter: Kauli ya Rais kuwa tuchape kazi, corona ni kitu cha kawaida, Mungu atatuongoza. Kauli ya Rais Magufuli imestua hata Shirika la Afya Duniani. Tanzania ni majirani zetu, ugonjwa ukisambaa Tanzania Kenya hatuwezi kuukwepa.

Ki historia Tanzania ni kama nchi inayoongozwa na Mwalimu Mkuu ambae anafanya maamuzi yote. Kwakufupi Magufuli anatuambia fanyeni yenu na mimi ninapiga mziki nikiwa ninafanya yangu. Lakini haya yataishia kwenye kilio.

Hata kama tunamtegemea Mungu tuwe na busara, huwezi kufanya maamuzi ya ovyo ukitegemea Mungu atakulinda.

View attachment 1405938
Mbona kwao corona imeua mmoja mpaka sasa ila askari wameua watatu,nani hafai kati ya corona na serikali hapo?

macson
 
Wamefanya lockdown lakini wagonjwa hadi sasa wako 81,Tanzania no lockdown tuna wagonjwa 20,think big mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Lockdown anywhere must be lockdown everywhere.
Hawa Kenya hawajafanya lockdown ya masaa 24.
Walijaribu mwanzoni siku ya kwanza waliambulia virungu,ndipo wakaja na lockdown ya usiku.Lakini shughuli za binadamu ziko zaidi mchana kuliko usiku.
Je slums kama Mathare pale Nairobi lockdown inawezekana kweli?
Je mbona katika nchi zinazotii amri ya lockdown katika dunia Kenya haipo kwenye ramani?
Kanuni mmoja ya lockdown inayotumika nchi mmoja yawezekana isiwe effective kwenye nchi nyingine.
 
Kila mtu atumie njia zake kupambana yaani washindwe kuwashangaa Italy na Spain ambao wamefungia watu ndani lakini daily wanazika watu 700+ waje kutushangaa Tanzania ambao tukifungiwa ndani tu kwa siku moja tunakufa kwa njaa wala sio corona.
Hapo ndio unaona ujinga wa majirani na watz wanaoipinga serikali kwenye corona.

macson
 
Tumeshapima wangapi Tanzania? Uwezo wetu ni kupima watu wangapi kwa siku? Siajabu Kuna walio RIP kwa corona lakini hatua taarifa zao.
Sasa taarifa usiyoijua wewe ya nini? Kuna wangapi wanakufa vijijini huko kwa njaa na wewe haujui na wala hauna mpango wa kujua,unataka tufe kwa njaa ndani kisa tunaogopa corona ambayo serikali imejitahidi kutoa elimu na kuchukua hatua mbalimbali kuwakinga wananchi wake?!

macson
 
Back
Top Bottom