Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,053
Jamani hivi nchi hii tutafika wapi?
Huyu mtoto alipata adha ya kuungua ndani ya nyumba siku nne zilizopita na kuletwa hospitali ya mkoa wa Kagera pale Bukoba mjini. Na hata sasa bado yupo hospitali.
Lakini mama wa mtoto analia kabisa maana hajapata matibabu yoyote kwa mwanae mbali ya kupewa asprin tu kila siku.
Kidonda cha huyu mtoto kinaonyesha kuwa huyu mtoto kichwa kinaweza hata kuoza kwa jinsi kidonda kilivyo hoi. Huwezi kuvumilia kumuangalia mtoto huyu kwa hata dakika tano kwa hali aliyonayo.
Mama wa mtoto anasema hata hali ya chakula anachokipata kwa ajili ya kulisha mwanae ni ugali tu na maharage yasiyo na chumvi.
Hivi hii ndiyo kikwete amekuwa akijisifia kuwa afya imeboreshwa nchini?
Nenda uangalie na uchafu ulivyosheheni hospitali pale hapo utaelewa ni nini kinaendelea.
Jamani mtoto huyu asaidiwe. Yeye ni kama watoto wengine wa mafisadi. anahitaji dawa. Anahitaji msaada wa kila aina. Na hapo ndipo tusimame kuwaambia watanzania, afya imeboreshwa. La sivyo huu ni utapeli wa kisiasa kwa watanzania.