Hivi nchi hii inaongozwa kwa sheria au kwa kushtukiza?

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,861
18,285
Mara tu Rais Magufuli alipoapishwa kuwa rais wa tano wa Tanzania alianza kutembelea ofisi na taasisi mbalimbali za serikali kwa mtindo wa kushtukiza huku akiwasimamisha kazi baadhi ya watendaji na kutoa maagizo kadhaa kwa watendaji hao. Aidha, Rais alipomuapisha Waziri Mkuu, kiongozi huyo mpya naye akaiga mtindo wa bosi wake?.kila kukicha yu kiguu na njia akivizia taasisi na mashirika kadhaa ya serikali kwa mtindo wa KUSHTUKIZA. Mawaziri, makatibu, wakuu wa mikoa na wilaya nao hawajaachwa nyuma kwa kushtukiza. Hii sasa imekuwa ndiyo staili mpya ya uongozi?.kwamba ili uonekane unafanya kazi sharti ushtukize watu na kuwakurupua kwa lengo la kutafuta kiki na uhalali wa nafasi unayoshika!

Sio nia yangu kupinga aina hii ya utendaji kwa kuwa kila kiongozi ana mbinu zake za kujitngaza kwa wananchi, ila natoa angalizo kwamba sheria na tataratibu za kiuongozi na usimamizi wa mambo ya serikali sharti zifuatwe. Hatuwezi kuendesha nchi kienyeji kana kwamba sheria hazipo. Kabla sijaenda mbele naomba turejee nyuma hadi kwenye meli ya wachina. Meli ile ilikamatwa kwa kukurupuka lakini mwisho wa siku serikali ilishindwa kesi na kulazimika kulipa mamilioni ya shilingi za walipa kodi kama fidia ya samaki waliopotea na meli iliyoharibika baada ya kuegeshwa baharini kwa muda mrefu.

Tutumie uzoefu huu kama mwalimu kwa lengo la kuepuka kuja kuiingiza nchi katika kesi zisizokuwa na msingi na hivyo kupoteza fedha za watanzania. Hawa watumishi wa umma wanaosimamishwa kazi ovyo bila kufuata taratibu, kanuni na sheria za utumishi watakuja kuisababishia serikali hasara ambayo kila mtanzania atabaki kinywa wazi. Kusema hivi sio kwamba nawatetea mafisadi bali nasisitiza kwamba sheria na taratibu za utumishi sharti zifuatwe katika kumsimamisha au kumuachisha mtumishi wa umma kazi. Nasema haya nikiwa na kumbukumbu kwamba serikali hushinwa 99% ya kesi kutokana na kuchukua maamuzi ya kukurupuka.

Naomba turejee kwenye dira ya uongozi na utawala bora pasipo kumuonea mtu wala kumtetea muovu au fisadi yeyote anayetaka kuliangamiza taifa. Hivi mnadhani ni kwanini fisadi Chenge na mafisadi wenzake hawakamtwi na kufikishwa mahakamani kwa ufisadi wao wanaoufanya kila kukicha? Tatizo ni ukosefu wa USHAHIDI usioacha shaka. Unaweza ukaona kabisa mtu fulani ni fisadi lililokubuhu lakini ukakosa ushahidi wa kumfikisha mahakamani au ukampeleka mahakamani na akashinda kesi misa ya kwanza. Hii ndio sababu watu kama Zombe na Prof Mahalu walishinda kesi zao saa 1 asubuhi licha ya kwamba tuhuma zao zilikuwa wazi kabisa.

Hivyo ndugu zangu, tuache kuchukua maamuzi ya kukurupuka tusije kuiingiza nchi katika hasara inayoweza kuepukika. Sheria na taratibu lazima zifuatwe kabla ya kuchukua maamuzi kishabiki, huku ukishangiliwa na wananchi ambao wengi wao ni mbumbumbu na wasiojua sheria.

:yield:
 
Hivi unajua maana na madaraka ya Raisi. Hakuna sheria hata moja inayomtaka Raisi amtaarifu mtumishi yeyote wa umma juu ya ziara au ujio wake. Ana uhuru wa kuingia ofisi yoyote ya serikali wakati wowote ule.
Hizi '' surprise visits '' zitakuwa nyingi tu. Mpaka mnyooke.
 
Kwani kufanya kwa kushtukiza ni kuvunja katiba? Kuna sheria gani inakataza kufanya jambo kwa kushtukiza? Ngoja majipu mtumbuliwe kwa kushtukiza tu.
 
Watanzania mnajema nyie? kama mnajua sheria Nchi ingeoza hivi? mwacheni MAGUFULI AFANYE KAZI.Watu wakati wanajenga mabondeni mlikuwa hamjui kuwa ni kosa kisheria? watu wanapo kwepa kufanya manunuzi kisheria hawajui sheria kuwa akijulikana atafukuzwa? anapo chelewa kuja kazini hajui kuwa kisheria ni kosa? ACHENI HIZO
 
Watanzania mnajema nyie? kama mnajua sheria Nchi ingeoza hivi? mwacheni MAGUFULI AFANYE KAZI.Watu wakati wanajenga mabondeni mlikuwa hamjui kuwa ni kosa kisheria? watu wanapo kwepa kufanya manunuzi kisheria hawajui sheria kuwa akijulikana atafukuzwa? anapo chelewa kuja kazini hajui kuwa kisheria ni kosa? ACHENI HIZO

hao watu wanaojenga mabondeni si wanapewa vibali na maofisa ardhi? kumbe hata wewe unajua kuwa tatizo la nchi hii ni mfumo halafu unajitoa akili.
 
hao watu wanaojenga mabondeni si wanapewa vibali na maofisa ardhi? kumbe hata wewe unajua kuwa tatizo la nchi hii ni mfumo halafu unajitoa akili.
Kwani wale waliobomolewa pale Mkwajuni walikuwa na vibali? Au unaropoka tu
 
hao watu wanaojenga mabondeni si wanapewa vibali na maofisa ardhi? kumbe hata wewe unajua kuwa tatizo la nchi hii ni mfumo halafu unajitoa akili.
Kwa hiyo unataka waachwe?
 
potelea mbali acha tuendekama hamna sheria kwanza.....maanasheria zilifuatwa sana uongozi uliopita yan ulikuwa unaogopa hata kumuuliza mtu kwa nini umejenga hapa?........zilisaidia nini sasa?......
 
Hujui unalichokandika ww.
Tangu uhuru mmeongozwa kwa sheria hyo unayoitaka ww lakn matokeo yake ni yapi?
Kila kukicha unaozo unaongezeka sasa hzo sheria zna faida gani?

Kama shtukizaya Magufuli imekuathiri kwa namna moja ama nyingne hyo utakula na wa kwenu. Sisi tunahitaji kuona nchi inapiga hatua kimaendeleo. Hizo haki peleka kwa mkeo na kwa wakwe zako
 
hao watu wanaojenga mabondeni si wanapewa vibali na maofisa ardhi? kumbe hata wewe unajua kuwa tatizo la nchi hii ni mfumo halafu unajitoa akili.

hayo ndo matatzo ya kukurupuka unaandika bila uchunguzi.
 
hao watu wanaojenga mabondeni si wanapewa vibali na maofisa ardhi? kumbe hata wewe unajua kuwa tatizo la nchi hii ni mfumo halafu unajitoa akili.

Tatizo lenu vijana mmeza tu eti mfumo! sheria za Nchi hii ni nzuri sana hazina tofauti yoyote na Uingereza bali watu ndio wajinga.dawa ya kuwatia ufahamu upya ni kama JPM anavyo fanya. Kosa la kijinga unaondoka sasa wakishaona kumbe jamaa hatanii watu wanakaa kwenye mstarina ndio inakuwandio tabia yetu.
 
Pole fisadi zamu yenu kulia sasa na sisi tucheke...yaani tuko hapa wote tazania lakini wengine wanaishi kama wako mbinguni,kwa ajili ya kuwanyonya wezao alafu unajifanya nchi haiendeshwi kwa sheria peleka ufisadi huko na usaa lazima mtumbuliwe tu..
 
kwali hali ya utendaji wa taifa hili ilipofikia utendaji wa jpm ni sahihi kabisa. unafikiri anakwenda bila taarifa za mahali husika. jpm is the right man, at the right time, taking the right steps. hatuongozwi na malaika, makosa ni sehemu ya mwanadamu.
 
mtaisoma namba mwaka huu.
mchukie msichukie,hapa ni kushtukiza tu hadi majipu yapone.
Prezdaa Magu piga kazi na tumbua majipu yote.
 
Back
Top Bottom