Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

kwakweli hata mimi hilo suala linanikera sana, yaani ndani mna samaki, kuku, pweza, harage sukari, unga, mchele na mboga zote ndani ya friji, na ukimjibu pika chochote atakuambia chochote ndo chakula gani. Na pia unaweza mwambia pika mchicha, unarudi kazi unakuta matembele.
 
Kuwaza Cha kupika huwa ni kazi ngumu hata kukiwa na kila kitu, nakumuuliza mume nikujua anapenda nini kipikwe nisije kupika kitu asichokipenda. So kusaidiana mawazo kuhusu msosi ni Jambo zuri na linapunguza mzigo kwa mpigaji na njia rahisi ni kuwa na ratiba ya msosi

Mimi nina ratiba ya misosi:-

1.J3 -Ugali
2.J4 -Tambi
3.J5 -Wali
4.ALH-Chips
5.IJM -Ndizi/Nyama
6.JMO-Ugali
7.J2- Pilau
 
Hahahah kweli sema sometime miyeyusho sana hilo swali 😝

Nilichojifunza wanawake kufanya jambo bila kumuuliza MZEE wanaona kama alitafanyika vyema kwahiyo anauliza kupata mawazo yako,kwa kifupi kama hawaamini mawazo yao! kweli swali la mizinguo kila kitu kipo lakini hajui cha kupika wakati kile ambacho kipo ndani kinaliwa ndio maana kimenunuliwa.
 
Nilichojifunza wanawake kufanya jambo bila kumuuliza MZEE wanaona kama alitafanyika vyema kwahiyo anauliza kupata mawazo yako,kwa kifupi kama hawaamini mawazo yao! kweli swali la mizinguo kila kitu kipo lakini hajui cha kupika wakati kile ambacho kipo ndani kinaliwa ndio maana kimenunuliwa.
Hahahahah ndio hivyo man, hawajiamini hawa watu. Anataka approval yako sema ndio wake wazuri sana maana huwa wanaomba ushauri kwenye mambo mengi zaidi. Sio wale wakurupukaji
 
Hapo nilipopakoleza hapo pamenichekesha sana.

Kwa hiyo wataka kusema kuwa, eti kuwaza utapika nini hiyo ni kitu kigumu kuliko hata kupeleka rockets kwenye orbit ya sayari ya Mars ??

Yaani unamaanisha kuwaza utapika nini ni kitu kigumu kuliko kukabiliana na GENETICS ENGINEERING, PHARMACOLOGY au PURE MATHEMATICS na ADVANCED PHYSICS za A-Level eeh?

Jamani tuwe serious jamani.

#justKidding
Ndio maana tunaitwa wanaume, tatizo lenu mnataka kujiona sawa na wake zenu, mwanaume ni strong mara zaidi, so ukiona we unamfananisha na wanaume its a point of weakness, ipo siku unaweza mwambia mbona hujifunzi useremala??? Acha fikra dhaifu. Hakuna kazi ngumu kama kumtreat mtu vizuri japo ni rahisi pia.
 
Swali Hilo halinipi shida maana inaonesha anakujali mpaka anakuita beby. Kuna wakati mwanamke anapika chakula halafu mwanaume anafika na kuonesha kutopendezewa na kilichopikwA. Hivo kuepusha hayo Ni Bora unaulizwa maana ukila unachojiskia hata amani inakuwepo
 
relax bro...calm down homeboy...easy easy home planet...chilling

Hilo swali ni linakukera kwa sababu ya frequency yake?? Je akiuliza mara moja kwa wiki will u complain??

Je tangu makuzi yako hujawahi kuulizwa au kusikia baba yako akiulizwa na mama yako??

Siku ya kwanza kuulizwa ulijisikiaje internal, annoy or not??

Je ukiwa na good mood/vibe afu ukaulizwa hilo what do you feel??

BTW ukitaka kujijua ww ni mtu wa aina gani go and look ur 20 yrs back na itakusaidia kutambua ur character.

Lastly tafuta article yoyote inayozungumzia mambo ya Emotional Intelligence it will help u.
Mtu anayepiga hata mkewe utamjua tu.
 
"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.
Inaonekana wewe mkeo unamuona kama hazimo ee, inaonekana wewe ni mtu anayeweka vitu moyoni na kuja kuongelea sehemu weak? Au nia yako ni nn? Badilisha mtizamo huo, kuwa a real man,penda familia yako, penda mkeo acha roho mbaya.
 
Kwahiyo j5 wali na j2 pilau hii inanikumbusha bweni
Mi sinaga ratiba siko bweni mkuu mi huwa na tabia kumpatia mke fedha kutosha wiki2
Mezani nakuta mapochopocho kiongozi

Huyo Ni Mimi lakini

Mimi lazima nijue ratiba za kula maana kama siku ni wali basi mchana napiga light food tu ,ila kama usiku ugali mchana nakula msosi heavy!!
 
"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.
Kwenye thread za watafiti kumbe na wewe umo? Vipi majibu yangu yalikufurahisha? Ukiona kuna thread unasoma halafu huwezi kuchangia, jua kuwa unasoma thread ambayo hustahili kuisoma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom